Spika Ndugai: Lissu asubiri Muziki wangu

Guys you cant fight with your own shadow, lisu anapigana na kivuli chake mwenyewe, anapambana na taifa lake mwenyewe, watanzania tupo milioni karibia 55 kati ya hao robo tu ndo wanamuunga mkono lissu na robotatu hatukubaliani naye, so asidhani kuwa akirudi tutampa hata ubalozi wa nyumba kumi, in short hapo ndo keshajimaliza kisiasa. Mshuhudie lissu akirudi awe mwananchi wa kawaida sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1002791

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amesema atatoa ufafanuzi na maelezo kuhusu ubunge wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), Januari 31, mwaka huu. Katika hatua nyingine; mahojiano baina ya Lissu na mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Stephen Sackur yaliyofanyika juzi, yameendelea kuzua mijadala tofauti kwa baadhi ya wasomi nchini kudai kuwa hatua ya kiongozi huyo kuisema vibaya nchi yake ni ukosefu wa uzalendo.

Spika Ndugai aliliambia gazeti hili kupitia kwa Katibu wa Spika wa Bunge, Said Yakubu kuwa atatolea ufafanuzi kuhusu mbunge huyo siku tisa kutoka leo. “Spika amesema na unaweza kumnukuu kwamba atatoa ufafanuzi kuhusu masuala yote yanayohusu ubunge wa Lissu Januari 31, mwaka huu,” alisema. Yakubu alisema Spika amekia hatua hiyo ya kutoa ufafanuzi kuhusu hatma ya Mbunge huyo kutokana na hatua yake ya Mbunge huyo kuendelea na ziara katika nchi mbalimbali za Ulaya.

Hivi karibuni kulikuwa na uvumi kwamba Spika Ndugai anataka kumvua ubunge Mbunge wa Singida Mashariki kutokana na kutokuwepo bungeni tangu 2017 na hasa kutokana na kuanza kufanya ziara katika nchi za Ulaya. Awali katika mahojiano aliyofanya na vyombo vya habari, Spika Ndugai alisema hajui kama kuna mkakati wa kumvua ubunge, lakini kwenye hoja ya utoro alikiri kuwa ni kweli Lissu ni mtoro.

“Kila mtu anajua Lissu ni mgonjwa na anapata matibabu Ubelgiji, sasa ukisikia ametoka Ubelgiji na kwenda sijui Uingereza na Spika hana taarifa na analipwa mshahara, huyo mtu ni mtoro, mwambieni arudi nyumbani kama ameshapona,” alisema Ndugai. Katika mahojiani hayo, Spika Ndugai alisema Lissu anapaswa kutambua kuwa hana ruhusa ya kuzurura nje ya nchi. Mbunge Lissu aliondoka nchini Septemba 7, mwaka 2017 baada ya kupigwa risasi takribani 30 na watu wasiojulikana nyumbani kwake jijini Dodoma na kwenda kutibiwa Nairobi kwa miezi minne na baadaye alikwenda nje ya nchi kuendelea na matibabu.

Mbunge huyo alipelekwa Ubelgiji, Januari 6, 2018 kupata matibabu katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, Campus ya Gasthuisberg, mjini Leuven, nchini Ubelgiji. Awali Bunge na Serikali walisema hawakuweza kugharamia matibabu ya mbunge huyo kwa sababu hakufuata utaratibu rasmi wakati akisarishwa nje ya nchi kwa matibabu. Wasomi wampinga Katika hatua nyingine mahojiano baina ya Lissu na Sackur yaliyofanyika juzi katika kituo hicho cha habari, yamezua mijadala tofauti kwa baadhi ya wasomi nchini kudai kuwa hatua ya kiongozi huyo ni ukosefu wa uzalendo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili jana, Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Diplomasia Dk Bernald Achiula na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk Bansen Bana, walisema kimsingi hatua hiyo licha ya kwamba ni haki yake kikatiba kuzungumza, inamuondolea hadhi aliyokuwa nayo kwa Watanzania. Lissu ambaye ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani nchini, alialikwa na mtangazaji huyo katika kipindi cha Hardtalk. Katika mahojiano hayo Lissu alihojiwa kuhusu mambo mbalimbali likiwemo la kushambuliwa kwake, utendaji wa Rais John Magufuli, usimamizi katika Sekta ya Madini, ushoga na mengineyo, na alijikuta akishindwa kujibu maswali ya mtangazaji huyo na badala yake kumshambulia Rais Magufuli na serikali yake kwa kila swali alilokuwa akiulizwa. Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia Dk Achiula alimtaja mwanasiasa huyo kuwa ni mtu aliyekosa uzalendo kwa taifa lake kwa kushindwa kuchuja kauli zake mbele ya mataifa mengine ambayo kimsingi baadhi yao yanaweza kuwa na ajenda zenye mlengo wa chuki na Tanzania. “Si jambo zuri hata kidogo, ni sawa na mwanafamilia unatoa mambo ndani ya nyumba yako na kwenda kuyapeleka nje, kwa utamaduni wetu wanafamilia hata wakitofautiana hukaa chini na kuyamaliza, suala hili si zuri kiutamaduni bali hata kisiasa pia,” alisema Dk Achiula.

Alisema hata viongozi katika mataifa mengine ya nje si kwamba hawatofauti au hawana mambo wanayoyalalamikia ndani ya mataifa yao isipokuwa wanajua ni vipi wataweza kuyazungumza ila si kwa utaratibu alioutumia kiongozi huyo anayesika hapa nchini kwa kujenga hoja mbalimbali. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk Bana mbali na kusisitiza kuwa Lissu kakosa uzalendo kutokana na tukio hilo, na kwamba kwa kuwa pia amejinadi kutaka kuwania nafasi ya urais, anapaswa ajitathimini kama anatosha kutokana na hatua yake hiyo.

Alisema yeye kama kiongozi aliyejijengea imani kwa watu, alipaswa kuwa makini na si kuongea kama mamluki kwa kuzungumza maneno hayo ya kichochezi na kueleza nini malengo ya kauli hizo huku akisisitiza kwa kitendo hicho kiongozi huyo kajiondolea sifa za kuwa kiongozi. Dk Bana alisema hata viapo mbalimbali alivyoapa kiongozi huyo kikiwemo kiapo cha Ubunge, kinamtaka kuwa mzalendo na kwamba kwa hatua hiyo aoneshe wazi mahali ulipo uzalendo wake.
Nashindwa kumuelewa tundu lissu,kwani yupo kwenye matibabu au ziharani.huyu jamaa atakuwa anataka kutumiwa na ndio maana anachoulizwa yeye amemkazania rais magu na serikali yake ili asaidiwe na mataifa ya nje kupata uraisi.Lakini atambue hizo ndoto zake ni zake na wapigaji hela.Lakini sisi tunaotaka maendeleo hatutaki watu kama yeye.
 
Lissu hawezi kufikia uwezo wa Kujieleza wa Sultan Seif Sharif Hamad

Lissu hawezi kufikia umaarufu wa Sultan Seif kimataifa

Lissu hawezi Kuwa Na Wafuasi wengi wa kufikia Sultan Seif

Lakin Sultan Seif kaanza kuzunguka kimataifa kwa robo karne (1992-2017) akichafua Taifa Kwenye macho ya Mabeberu
Kama kuna kitu kafanikiwa Sana Basi Ni mambo Mawili tu

1) Kumaliza soli Za Viatu

2) kUjaza mihuri Kwenye hati yake ya kusafiria
Shit-hole
 
Pumba tupu.

Hata sijui ilikuwaje huyu jamaa akapata hicho cheo?Unaweza kuta hatujawahi kuongozwa na watu ambao siyo mamburulaz!
 
1548275398337.png
 
Spika naye kichwani hakuna kitu, anashindwa kuidhibiti serikali kwa matumizi mabovu ya rasilimali zetu anakazana na watu ambao kuhangaika nao hakutuongezei kitu kama Taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna maisha nje ya siasa na ubunge,kuna utu na ubinadamu.Vyeo ni zawadi ya maisha isiyodumu.Lakini wema na utii kwa hisia za maumivu ya wengine hudumu dahari kwa dahari.

Madaraka hulevya kuliko kiriba cha mvinyo,na mning'inio wa madaraka hukawia kuondoka mpaka pale utakapohuhudia madaraka hayapo katika mikono yako.

Huyu alipaswa kuonyesha muhimili wa bunge ni eneo la kujitegemea bila kufuata midundo ya Serikali,lkn yeye sasa anatuonyesha wazi kuwa kuna mahali anatumwa.Mbunge wa bunge lako aliyepigwa risasi wakati wa vikao vyako,hujamtibu kwa mujibu wa sheria,hujamjulia hali wala kumpa pole,leo unaibuka kumshambulia??

Kweli wote tu wa chama kimoja,lakini nadhani tunatofautiana katika utu na kuhimili madaraka.Inasikitisha sana,huyu anadhani ubunge ndio maisha,kumbe kuna maisha kabla na baada ya ubunge.Wakati akiwa muhifadhi wa Wanyamapori,wengine walikuwa kwenye hii tasnia muda.Kutoka kwenye uhifdhi mpaka Uspika anaona kawa mkuu wa pepo.Alijisemea Iron Smith "You can remove a person from a bush,but you can not remove a bush's mentality from a person".

Alikuwepo Samuel,mbabe na jeuri,aliitikisa serikali na kashfa ya Richmond,kwa visasi vya madaraka,akatuchepushia mchakato wetu wa Katiba Mpya kwa ahadi za kesho,akiwa Urambo anaomba kura za mkewe,alituhakikishia yule wa Monduli si wa kumpa dhamana maana ana afya mgogoro.

Haikupita miaka miwili,alisafirishwa daraja la kwanza katika ndege kwenda kwenye matibabu,akiwa kwenye daraja la juu la kifahari la ndege,kwenye mvinyo na huduma za VIP,lakini alirudi chini ya "boot" la ndege,si tena kama abiria,bali kama "mzigo".Na juu la kasha lililohifadhi mwili wake,alifunikwa na gunia ili asitoe harufu,na juu palikuwa na maandishi "These are the remains of Mr S.J.S".Yaani haya ni mabaki ya S.J.S.

Yaani hakuwa yule tena aliyeondoka kwa daraja la kwanza,bali mabaki na masalia yaliyokuwa treated kama mzigo,wakati anaondoka alipita eneo la Wageni maarufu VIP,lakini wakati wa kurudi,alipitishwa eneo la mizigo,ambapo alichanganywa na mizigo kama TV,radio na makasha ya bidhaa mbalimbali.

Huu ndio mwisho wa kila binadamu,licha ya kiburi na majigambo yetu ya vyeo na mali.Sisi tutakuwa mabaki,na tutaoza,huku nyuma,yatazungumzwa yale tuliyowahi kuwafanyia wenzetu wakati tukiwa hao.

Tuandae kesho yetu iliyo njema,itakayobaki katika maandishi na kumbukumbu bora kwa ajili ya uzao wa viuno vyetu.Tusiwaachie watoto visasi vinavyotokana na sisi kununua "chuki ya kijamii".

Hii ni aina ya chuki ambayo mtu huitengeneza kwa kumchukia mtu mmoja ambaye ana mtiririko wa watu wanaomuonea huruma hata kama hawajuani,yul ni msumbufu sana,alitupa shida,na hata mie nilimuona kama "kikwazo",lakini kwa sambulizi lile,nami nilijiweka katika nafasi yake,na niliingiwa na huruma.Huruma inayoweza kumeza itikadi na mlengo wangu wa kisiasa.Ninaamini,kabla ya itikadi na mlengo wa kisiasa,kuna utu na maisha yanayoakisi ubinadamu.

Hata Simba humuonea huruma ndama wa nyumbu aliyetoka kuzaliwa,huruma kwa wanyama wasio na utashi,na sawa na ukatiri wa binadamu aliyepewa akili na utashi.Mungu atusaidie
So poignant really!

Aisee...wewe kichwa chako kina Madini
 
Nashindwa kumuelewa tundu lissu,kwani yupo kwenye matibabu au ziharani.huyu jamaa atakuwa anataka kutumiwa na ndio maana anachoulizwa yeye amemkazania rais magu na serikali yake ili asaidiwe na mataifa ya nje kupata uraisi.Lakini atambue hizo ndoto zake ni zake na wapigaji hela.Lakini sisi tunaotaka maendeleo hatutaki watu kama yeye.
= Ziarani
 
Kabla Lisu hajaucheza huo mziki si ajabu ukawa hoi kitandani kwa kuumwa ...Wanadamu tunaijua kesho yetu ? Hiki kiburi cha uzima ni cha nini Ndugai ?

Sina mengi ila Ndugai ya Mungu mengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndungai pole naona umekubali kutoa ushuhuda wa ile mzizima1, umeshindwa kujizuia. Mwaka huu wa Ajabu kila tamko na wazo linalotoka kwa spika Ndungai Ni la kuudhi na kushtua wananchi.KWAN UKIKAA KIMYA KAMA ULIVYOKUA KIMYA KUHUSU MATIBABU YAKE KUNA SHIDA GANI? Ndugai unaudhi wana nchi🙂🙂🙂🙂 Ambao ndio watakupokea ukistafu.
...hivi vituko vya hadh ya Mwendokasi
 
Back
Top Bottom