Spika Ndugai: Lissu asubiri Muziki wangu

Ndugai mjinga sana anavyomsakama Lissu ndivyo anavyozidi kumuongezea credit na mbumbumbu waanza kuhisi kitu katika kushambuliwa Risasi Lissu watu wanakonet dot tu
 
index.jpg

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amesema atatoa ufafanuzi na maelezo kuhusu ubunge wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), Januari 31, mwaka huu. Katika hatua nyingine; mahojiano baina ya Lissu na mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Stephen Sackur yaliyofanyika juzi, yameendelea kuzua mijadala tofauti kwa baadhi ya wasomi nchini kudai kuwa hatua ya kiongozi huyo kuisema vibaya nchi yake ni ukosefu wa uzalendo.

Spika Ndugai aliliambia gazeti hili kupitia kwa Katibu wa Spika wa Bunge, Said Yakubu kuwa atatolea ufafanuzi kuhusu mbunge huyo siku tisa kutoka leo. “Spika amesema na unaweza kumnukuu kwamba atatoa ufafanuzi kuhusu masuala yote yanayohusu ubunge wa Lissu Januari 31, mwaka huu,” alisema. Yakubu alisema Spika amekia hatua hiyo ya kutoa ufafanuzi kuhusu hatma ya Mbunge huyo kutokana na hatua yake ya Mbunge huyo kuendelea na ziara katika nchi mbalimbali za Ulaya.

Hivi karibuni kulikuwa na uvumi kwamba Spika Ndugai anataka kumvua ubunge Mbunge wa Singida Mashariki kutokana na kutokuwepo bungeni tangu 2017 na hasa kutokana na kuanza kufanya ziara katika nchi za Ulaya. Awali katika mahojiano aliyofanya na vyombo vya habari, Spika Ndugai alisema hajui kama kuna mkakati wa kumvua ubunge, lakini kwenye hoja ya utoro alikiri kuwa ni kweli Lissu ni mtoro.

“Kila mtu anajua Lissu ni mgonjwa na anapata matibabu Ubelgiji, sasa ukisikia ametoka Ubelgiji na kwenda sijui Uingereza na Spika hana taarifa na analipwa mshahara, huyo mtu ni mtoro, mwambieni arudi nyumbani kama ameshapona,” alisema Ndugai. Katika mahojiani hayo, Spika Ndugai alisema Lissu anapaswa kutambua kuwa hana ruhusa ya kuzurura nje ya nchi. Mbunge Lissu aliondoka nchini Septemba 7, mwaka 2017 baada ya kupigwa risasi takribani 30 na watu wasiojulikana nyumbani kwake jijini Dodoma na kwenda kutibiwa Nairobi kwa miezi minne na baadaye alikwenda nje ya nchi kuendelea na matibabu.

Mbunge huyo alipelekwa Ubelgiji, Januari 6, 2018 kupata matibabu katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, Campus ya Gasthuisberg, mjini Leuven, nchini Ubelgiji. Awali Bunge na Serikali walisema hawakuweza kugharamia matibabu ya mbunge huyo kwa sababu hakufuata utaratibu rasmi wakati akisarishwa nje ya nchi kwa matibabu. Wasomi wampinga Katika hatua nyingine mahojiano baina ya Lissu na Sackur yaliyofanyika juzi katika kituo hicho cha habari, yamezua mijadala tofauti kwa baadhi ya wasomi nchini kudai kuwa hatua ya kiongozi huyo ni ukosefu wa uzalendo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili jana, Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Diplomasia Dk Bernald Achiula na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk Bansen Bana, walisema kimsingi hatua hiyo licha ya kwamba ni haki yake kikatiba kuzungumza, inamuondolea hadhi aliyokuwa nayo kwa Watanzania. Lissu ambaye ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani nchini, alialikwa na mtangazaji huyo katika kipindi cha Hardtalk. Katika mahojiano hayo Lissu alihojiwa kuhusu mambo mbalimbali likiwemo la kushambuliwa kwake, utendaji wa Rais John Magufuli, usimamizi katika Sekta ya Madini, ushoga na mengineyo, na alijikuta akishindwa kujibu maswali ya mtangazaji huyo na badala yake kumshambulia Rais Magufuli na serikali yake kwa kila swali alilokuwa akiulizwa. Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia Dk Achiula alimtaja mwanasiasa huyo kuwa ni mtu aliyekosa uzalendo kwa taifa lake kwa kushindwa kuchuja kauli zake mbele ya mataifa mengine ambayo kimsingi baadhi yao yanaweza kuwa na ajenda zenye mlengo wa chuki na Tanzania. “Si jambo zuri hata kidogo, ni sawa na mwanafamilia unatoa mambo ndani ya nyumba yako na kwenda kuyapeleka nje, kwa utamaduni wetu wanafamilia hata wakitofautiana hukaa chini na kuyamaliza, suala hili si zuri kiutamaduni bali hata kisiasa pia,” alisema Dk Achiula.

Alisema hata viongozi katika mataifa mengine ya nje si kwamba hawatofauti au hawana mambo wanayoyalalamikia ndani ya mataifa yao isipokuwa wanajua ni vipi wataweza kuyazungumza ila si kwa utaratibu alioutumia kiongozi huyo anayesika hapa nchini kwa kujenga hoja mbalimbali. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk Bana mbali na kusisitiza kuwa Lissu kakosa uzalendo kutokana na tukio hilo, na kwamba kwa kuwa pia amejinadi kutaka kuwania nafasi ya urais, anapaswa ajitathimini kama anatosha kutokana na hatua yake hiyo.

Alisema yeye kama kiongozi aliyejijengea imani kwa watu, alipaswa kuwa makini na si kuongea kama mamluki kwa kuzungumza maneno hayo ya kichochezi na kueleza nini malengo ya kauli hizo huku akisisitiza kwa kitendo hicho kiongozi huyo kajiondolea sifa za kuwa kiongozi. Dk Bana alisema hata viapo mbalimbali alivyoapa kiongozi huyo kikiwemo kiapo cha Ubunge, kinamtaka kuwa mzalendo na kwamba kwa hatua hiyo aoneshe wazi mahali ulipo uzalendo wake.
 
Nchi hii kuna wasomi kwani??, Wasomi mwenyewe ndo hao wachumia tumbo wanaojiita maprofesa uchwara, Au ndo hao wenye PhD lakini kutamka intaprentinyuwaaaa wanashindwa?...

Kwaiyo Lisu angekufa ndo angekuwa mzalendo? Pumbav zao hao wasomi uchwara.
 
Hawa wasomi ucharwa na spika wa Bunge kuhusu "utoro na uzururaji wa Lissu", wangejua nchi zote za continental Europe ulaya magharibi zinatosha kuenea ndani ya nchi moja ya DR Congo na bado nafasi inabaki. Maana yake ulaya hiyo kieneo ni ndogo.

Hivyo Mh.Tundu Lissu kutoka nchi moja kwenda nyingine kwa treni ya raha tupu (luxury) zenye mwendo kasi wa 200 kph haziathiri hali yake ya kuwa bado mgonjwa anayeendelea kusubiri mlolongo wa upasuaji na tiba ya mama -cheza za kisasa ambazo hazipo Tanzania.

Nitabandika video ili kuelewesha wasomi ucharwa naongea nini.
 
hao wahadhiri wanafikiri kwa kutumia matak*! yaani mtu amepona chupuchupu kuuwawa na utawala (ushahidi wa kimazingira unaonesha hivyo na hakuna ushahidi mwingine wowote), kisha akapata platform ya ku protest (ambayo hapa nchini imeminywa) alafu wanategemea aipambe serikali ya magufuri?? pumbavu kweli hao.
Hakuna sehemu Lisu alipoikandia Tanzania, bali ameeleza ukweli wa kile kinachofanywa na utawala wa Magufuri, kama hao wanaojiita 'wasomi' hawawezi kulielewa hilo basi ni mambumbumbu wa kutupwa.
 
WANAFIKI na unafiki wao uliokithiri.

View attachment 1002791

Back
Top Bottom