Spika Ndugai: Lissu asubiri Muziki wangu

Spika Ndugai: Lissu asubiri Muziki wangu

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,494
Reaction score
12,465
Hii ni Katika ule muendelezo wa kauli ya Spika kumtaka lissu arejee nchini kutokana na kwamba hana kibali cha kuishi nje ya nchi,la sivyo atajikuta yupo nje ya uwanja.sasa hivi spika anasema "Lissu asubiri muziki wangu" huku TL naye akijibu mapigo "usijaribu kuuzima moto kwa petroli,utapotea"
Je,nini kitatokea Lissu ataucheza muziki wa Spika au Ndugai atapotea kwa moto wa petroli wa TL? usikose toleo lijalo....
Screenshot_20190122-060311.png



====

Dar es Salaam. Hatma ya ubunge wa Tundu Lissu itajulikana kuanzia Januari 29 wakati Job Ndugai atakapovaa “joho” la uspika kuongoza Mkutano wa 14 wa chombo hicho cha kutunga sheria.

Ndugai amemtaka Lissu arejee nyumbani kuendelea na majukumu yake ya kuwawakilisha wananchi wa Singida Mashariki, akisema hana kibali baada ya mbunge huyo kutoa tamko mwishoni mwa wiki akituhumu kuwepo na mpango wa kumvua ubunge.

Lissu yuko nchini Ubelgiji kumalizia matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 akiwa ndani ya gari, nje ya makazi yake Area D mjini Dodoma, ikiwa ni saa chache baada ya kuhudhuria kikao cha Bunge.

Baada ya shambulio hilo la Septemba 7, mwaka juzi alipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kabla ya kusafirishwa kwa ndege kwenda Nairobi, Kenya usiku wa siku hiyo.

Mkutano huo wa 14 wa Bunge la Kumi na Moja utaanza Januari 29, siku saba kuanzia leo, pamoja na mambo mengine unatarajiwa kupokea ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), aliyehojiwa jana na Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge.

Majibizano kati ya Lissu na Spika Ndugai yamekuwa yakipamba moto siku hadi siku tangu alipotoa waraka alioupa jina la “Baada ya Risasi Kushindwa, Sasa Wanataka Kunivua Ubunge”. Katika waraka huo, Lissu anatuhumu uongozi wa Bunge na Serikali kuandaa mpango huo, jambo ambalo Ndugai amesema “ni uzushi”.

Jana, Mwananchi ilimuhoji tena Spika Ndugai kuhusu madai ya Lissu kuwa anafahamu taarifa za matatizo yake na kwamba alishiriki katika hatua za awali za kumuwezesha kupata matibabu, jambo ambalo alikubaliana nalo.

“Alipopata matatizo wote tulishuhudia na Bunge lilitimiza wajibu wake katika zile saa chache ambazo ni muhimu katika kuokoa maisha yake. Na hilo lilifanikiwa. Tunatambua kwamba mwenzetu aliumizwa na alikuwa hospitalini,” alisema Spika Ndugai.

“Ila sasa hivi tunavyoongea ametoka hospitali yuko huko aliko. Inaelekea ameruhusiwa. Amekuwa akitumia mwanya huo kuzunguka na kuchafua sifa ya nchi yetu. Kwani nani amempa ruhusa?

“Sasa nimwambie tu kwamba sisi tunamuhitaji maana mpaka sasa hajawahi kuniandikia chochote mimi kama kiongozi wake bungeni na wala daktari wake hajasema kitu. Kwa maana hiyo, mimi namuhesabu kama ni mtoro.”

Alipoulizwa sababu za muhimili huo kushindwa kumuhudumia Lissu licha ya familia yake kuandika barua mara nne, Ndugai alijibu kwa kifupi: “Hayo ya nyuma tuyaache. Atakapokuja mwenyewe tutayazungumza.”

‘Nilienda BBC nikitokea hospitali’

Lakini Lissu, ambaye alihojiwa na Shirika la Habari la Uingereza (BBC) katika kipindi cha Hard Talk kilichorushwa jana alikuwa na majibu ya hoja za Spika.

Alisema kama Spika anataka kujua vizuri hali yake, hahitaji kwenda Ubelgiji bali wapo madaktari ambao Ndugai aliahidi kuwapeleka Nairobi kumuona, lakini hajafanya hivyo.

“(Madaktari) Wakifika Ubelgiji, hawahitaji hata kuzungumza na mimi, wataonana na madaktari wangu na kuzungumza hali yangu na hapo Spika atakuwa na nafasi ya kusema nimepona au la,” alisema mwanasheria huyo.

“Mimi niliumizwa mguu na kiunoni, sikupigwa risasi kichwani, kwa hiyo naweza kuzungumza. Nilikwenda BBC nikitokea hospitalini na nikarudi hospitalini mpaka sasa. Kwa hiyo asiseme nimepona wakati yeye si daktari,”alisema Lissu.

Katika kipindi cha Hard Talk kilichorushwa jana, Lissu alihojiwa na mtangazaji Steve Sackur kuhusu kuihusisha Serikali na shambulio dhidi yake, kukubalika kwa Rais, kuongezeka kwa makusanyo ya kodi na wimbi la viongozi wa upinzani kujivua uanachama na kuhamia CCM.

“Sikiliza Steve, mimi ni mnadhimu wa upinzani, mimi ni kiongozi wa Bunge. Ninaishi kwenye nyumba za Serikali zinazolindwa saa 24, siku saba za wiki. Siku ya shambulio ilikuwa mchana wakati wa chakula nikiwa natoka bungeni,” alisema Lissu kujibu swali kuhusu tuhuma zake dhidi ya Serikali wakati inawezekana washambuliaji walimfuata kwa sababu ni maarufu.

“Washambuliaji walikuja na bunduki kwenye makazi ya viongozi wa Bunge, akiwemo Naibu Spika. (Wakati huo) hakukuwa na ulinzi wowote katika geti wala popote.”

Kuhusu kukubalika kwa Rais Magufuli na wapinzani kuhamia CCM, Lissu alisema hiyo ilikuwa katika mwaka wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Tano, lakini baadaye kura za maoni zilioonyesha umaarufu umeshuka na hata makusanyo yameshuka, huku akituhumu kuwepo kwa matumizi ya fedha kushawishi wabunge na madiwani kuhamia chama tawala.
 
Hii ni Katika ule muendelezo wa kauli ya Spika kumtaka lissu arejee nchini kutokana na kwamba hana kibali cha kuishi nje ya nchi,la sivyo atajikuta yupo nje ya uwanja.sasa hivi spika anasema "Lissu asubiri muziki wangu" huku TL naye akijibu mapigo "usijaribu kuuzima moto kwa petroli,utapotea"
Je,nini kitatokea Lissu ataucheza muziki wa Spika au Ndugai atapotea kwa moto wa petroli wa TL? usikose toleo lijalo....
View attachment 1001634
Hahaha walahi ndungayi anaendeshwa na jpm walahi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni Katika ule muendelezo wa kauli ya Spika kumtaka lissu arejee nchini kutokana na kwamba hana kibali cha kuishi nje ya nchi,la sivyo atajikuta yupo nje ya uwanja.sasa hivi spika anasema "Lissu asubiri muziki wangu" huku TL naye akijibu mapigo "usijaribu kuuzima moto kwa petroli,utapotea"
Je,nini kitatokea Lissu ataucheza muziki wa Spika au Ndugai atapotea kwa moto wa petroli wa TL? usikose toleo lijalo....
View attachment 1001634

Kauli za Ndugai hazina weredi wowote! Ni kama kauli za hawara aliyefumaniwa. Ni udhaifu juu ya udhaifu.
 
Siasa za visasi, zitaisaidia nini Tanzania na watu wake??!!
 
Lissu hawezi kufikia uwezo wa Kujieleza wa Sultan Seif Sharif Hamad

Lissu hawezi kufikia umaarufu wa Sultan Seif kimataifa

Lissu hawezi Kuwa Na Wafuasi wengi wa kufikia Sultan Seif

Lakin Sultan Seif kaanza kuzunguka kimataifa kwa robo karne (1992-2017) akichafua Taifa Kwenye macho ya Mabeberu
Kama kuna kitu kafanikiwa Sana Basi Ni mambo Mawili tu

1) Kumaliza soli Za Viatu

2) kUjaza mihuri Kwenye hati yake ya kusafiria
 
Tundu Lissu asijiingize kwenye ngonjera hizi za kipuuzi.

Kama kweli ananuia kugombea uongozi wa juu, itakuwa ni kujipotezea malengo kujibishana na watu hawa.
Ni wakati wa kujiwekea malengo katika jitihada zake za kufikia azma yake. Kujibizana na hawa kwa wakati huu hakuwezi kabisa kuwa ni mojawapo ya malengo yake.

Angalia sasa, hata watu wa Mwananchi wameweza kutambua 'triviality' ya jambo lenyewe. Itakuwaje Lissu asilione hivyo!
Epukana kabisa na wanaotafuta kuvuruga malengo uliyojiwekea.
 
Kuna maisha nje ya siasa na ubunge,kuna utu na ubinadamu.Vyeo ni zawadi ya maisha isiyodumu.Lakini wema na utii kwa hisia za maumivu ya wengine hudumu dahari kwa dahari.

Madaraka hulevya kuliko kiriba cha mvinyo,na mning'inio wa madaraka hukawia kuondoka mpaka pale utakapohuhudia madaraka hayapo katika mikono yako.

Huyu alipaswa kuonyesha muhimili wa bunge ni eneo la kujitegemea bila kufuata midundo ya Serikali,lkn yeye sasa anatuonyesha wazi kuwa kuna mahali anatumwa.Mbunge wa bunge lako aliyepigwa risasi wakati wa vikao vyako,hujamtibu kwa mujibu wa sheria,hujamjulia hali wala kumpa pole,leo unaibuka kumshambulia??

Kweli wote tu wa chama kimoja,lakini nadhani tunatofautiana katika utu na kuhimili madaraka.Inasikitisha sana,huyu anadhani ubunge ndio maisha,kumbe kuna maisha kabla na baada ya ubunge.Wakati akiwa muhifadhi wa Wanyamapori,wengine walikuwa kwenye hii tasnia muda.Kutoka kwenye uhifdhi mpaka Uspika anaona kawa mkuu wa pepo.Alijisemea Iron Smith "You can remove a person from a bush,but you can not remove a bush's mentality from a person".

Alikuwepo Samuel,mbabe na jeuri,aliitikisa serikali na kashfa ya Richmond,kwa visasi vya madaraka,akatuchepushia mchakato wetu wa Katiba Mpya kwa ahadi za kesho,akiwa Urambo anaomba kura za mkewe,alituhakikishia yule wa Monduli si wa kumpa dhamana maana ana afya mgogoro.

Haikupita miaka miwili,alisafirishwa daraja la kwanza katika ndege kwenda kwenye matibabu,akiwa kwenye daraja la juu la kifahari la ndege,kwenye mvinyo na huduma za VIP,lakini alirudi chini ya "boot" la ndege,si tena kama abiria,bali kama "mzigo".Na juu la kasha lililohifadhi mwili wake,alifunikwa na gunia ili asitoe harufu,na juu palikuwa na maandishi "These are the remains of Mr S.J.S".Yaani haya ni mabaki ya S.J.S.

Yaani hakuwa yule tena aliyeondoka kwa daraja la kwanza,bali mabaki na masalia yaliyokuwa treated kama mzigo,wakati anaondoka alipita eneo la Wageni maarufu VIP,lakini wakati wa kurudi,alipitishwa eneo la mizigo,ambapo alichanganywa na mizigo kama TV,radio na makasha ya bidhaa mbalimbali.

Huu ndio mwisho wa kila binadamu,licha ya kiburi na majigambo yetu ya vyeo na mali.Sisi tutakuwa mabaki,na tutaoza,huku nyuma,yatazungumzwa yale tuliyowahi kuwafanyia wenzetu wakati tukiwa hao.

Tuandae kesho yetu iliyo njema,itakayobaki katika maandishi na kumbukumbu bora kwa ajili ya uzao wa viuno vyetu.Tusiwaachie watoto visasi vinavyotokana na sisi kununua "chuki ya kijamii".

Hii ni aina ya chuki ambayo mtu huitengeneza kwa kumchukia mtu mmoja ambaye ana mtiririko wa watu wanaomuonea huruma hata kama hawajuani,yul ni msumbufu sana,alitupa shida,na hata mie nilimuona kama "kikwazo",lakini kwa sambulizi lile,nami nilijiweka katika nafasi yake,na niliingiwa na huruma.Huruma inayoweza kumeza itikadi na mlengo wangu wa kisiasa.Ninaamini,kabla ya itikadi na mlengo wa kisiasa,kuna utu na maisha yanayoakisi ubinadamu.

Hata Simba humuonea huruma ndama wa nyumbu aliyetoka kuzaliwa,huruma kwa wanyama wasio na utashi,na sawa na ukatiri wa binadamu aliyepewa akili na utashi.Mungu atusaidie
 
Back
Top Bottom