Spika Ndugai awashukia wasomi nchini, asema anajua watamshambulia katika mitandao

Spika wa Bunge Job Ndugai amesema anakerwa na kada nne ambazo zinatukuza usomi wao mbele ya Watanzania wasiopenda kujikweza.

Amezitaja kada hizo ni wahasibu, wahandisi, mawakili na madaktari wa kusomea ambao amesema kila mtu anataka kuanza na kutukuza kisomo chake wakati si lazima iwe hivyo.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo, Jumatano, Septemba 1, 2021 bungeni katika kipindi cha mjadala wa hoja za wabunge kuhusu muswada wa mabadiliko ya sheria mbalimbali uliowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi.

Amesema anajua atashambuliwa na mawakili mitandaoni lakini anataka kujua iwapo hawaoni aibu kujiita ni wasomi wakati nchi ina wasomi wengine.

“Najua watanishambulia katika mitandao, ..ah lakini huo ndiyo ukweli nani asiyekuwa msomi katika nchi hii, au wengine hawajasoma, kwani hamuoni aibu fulani hivi kujiita wasomi wakati kuna wengine katika nchi hii wamesoma,” amehoji Ndugai.

Spika amesema; “kuna wakati nitahitaji mnishauri kuhusu hili la wanasheria kujiita wakili msomi, huu ni utaratibu fulani ulioanzishwa na wenzetu Waingereza wa kutukuza baadhi ya kada,’’

Ndugai amezitaja kada nne zinazompa shida na anawashangaa kuona wakitukuzwa kuliko wengine licha ya wengi kuwa ni wasomi.

Kada hizo ni wahasibu, wahandisi, mawakili na madaktari wa kusomea ambao amesema kila mtu anataka kuanza na kutukuza kisomo chake wakati siyo lazima iwe hivyo.

Kuhusu mawakili amehoji kama wakibaki na neno la wakili watapungukiwa kitu gani huku akiweka wazi kuwa neno msomi linawaongezea kitu gani kwa Watanzania wasiopenda kujikweza katika mambo mengine.

Kwa kada alizozitaja Spika, mawakili hujiita wakili msomi, wahasibu hupenda kuanza na neno CPA, wahandisi hutumia neno la ‘Engineer’ na waliosoma shahada za uzamivu (PhD) majina yao huanza na neno Dk

View attachment 1920134
Ndio kazi aliyotumwa na wapiga kura wake?
 
Ni kweli ila hii ni Africa wengi hujitukuza na kutaka kutukuzwa mimi hawanipi shida maana hawana cha kuniambia.

Hizo Kada hapo juu ni Kada za watoto wa maskini walio wengi, mtoto wa tajiri anasomea biashara, uchumi nk na hana mda wa kutafuta law school au cpa Ili aajiriwe.

Technically huwa nawapuuza ni watu wasio na pesa,mchukue Dr mpe vihela akuuguze uone anavyopaparika.Hao wahandisi ndio kabisaa njaa tupu.
Mkuu upi sawa?
Mhandisi, muhasibu hawawezi kujiajiri ?
Hawawezi kusajili kampuni zao na kujiendeshea biashara zao?
Mwanasheria hawezi kujiajiri, mkuu unawadisi vibaya hao wasomi uchwara. Yani umewakanyaga na tope.
 
Ndugai yupo sahihi katika hili, ni ushamba sana kutambulisha watu kwa kutanguliza Dr, Professor, Injinia katika shughuli. Waafrika tupunguze ulimbukeni kwa title za kwenye makaratasi ya darasani tu.
 
Ndugai yupo sahihi katika hili, ni ushamba sana kutambulisha watu kwa kutanguliza Dr, Professor, Injinia katika shughuli. Waafrika tupunguze ulimbukeni kwa title za kwenye makaratasi ya darasani tu.
Mkuu mbona ndugai na wale mazuzu wenzie wanapenda kuitwa mheshimiwa.........aache wenge, na sisi tutumie title zetu, hatujamtuma kukwepa umande, wakati wenzie wakienda shule yeye alienda kukusanya ubuyu....
 
Ni kasumba za kishamba tu.
Kama umewahi kutazama mijadala ya Seneti au bunge la wawakilishi Marekani hawana haya mambo ya kuitana honourable, hata spika wanamuita madam Speaker, Mr. Chairman n.k
Mkuu mbona ndugai na wale mazuzu wenzie wanapenda kuitwa mheshimiwa.........aache wenge, na sisi tutumie title zetu, hatujamtuma kukwepa umande, wakati wenzie wakienda shule yeye alienda kukusanya ubuyu....
 
Ni ushamba au ulimbukeni tu, unakuta kwenye shughuli ya harusi mtu anatambulishwa Injinia Architect Dr Kalubandike Juma!
Mi nakubaliana nae, ni suala la mentality tu, kwani hata wagunduzi wengi katika fani mbalimbali waliopo nchi za ughaibuni tunawaona kila siku wakofanya mambo makubwa bila kujitwisha vilemba vya ukoko. Hivyo tuzo za udaktari ndizo pekee huwa nazikubali, kwani kila Mtu amesoma kwa nafasi yake mpaka tupo wengi mitaani wenye madigirii ya kila fani hadi bodi ya mikopo inadhindwa kutuhudumia waliopo vyuoni.
 
Back
Top Bottom