Hapa kuna kudharaulika kiti cha spika. Spika ni mtu mkubwa saba katika hii nchi, anashikilia moja ya mihimili mitatu ya dola. Hata kama wewe ni mpinzani na kuna kitu kimekukera heshimu tu kiti cha spika. Kiti cha spika kikiheshimika hata anayekalia kiti hicho atajiheshimu. Linganisha na enzi za Pius Msekwa na Samuel Sitta, kiti cha spika kiliheshimika na spika hakuwa na tatizo na wabunge. leo hii mtu anatukana mubashara bungeni eti spika ni fala au sijui nini... Mara mwingine anakataa kutii amri ya spika mwenye mamlaka yake unategemea nini? Spika nae ni mtu na ana mihemuko yake, lazima afure pale kiti chake kinapodharauliwa. Kwa Suala la Mnyika juzi hekima tu ingetumika. Mnyika angekaa tu kimya kama alivyoamriwa wala asingetakiwa kutoka nje. Tena pale amri ya kutoka nje angejongea mwenyewe nje nani angemgusa? Angeonesha ana hekima na kila mtu angekuwa upande wake. Lakini kwa sasa mtu yeyote anayemtetea mnyika ni kwa sababu tu ya mihemukio ya kisiasa, kiukweli mnyika alidharau kiti cha spika.