Spika Ndugai ana personality disorder?

Spika Ndugai ana personality disorder?

Hapa kuna kudharaulika kiti cha spika. Spika ni mtu mkubwa saba katika hii nchi, anashikilia moja ya mihimili mitatu ya dola. Hata kama wewe ni mpinzani na kuna kitu kimekukera heshimu tu kiti cha spika. Kiti cha spika kikiheshimika hata anayekalia kiti hicho atajiheshimu. Linganisha na enzi za Pius Msekwa na Samuel Sitta, kiti cha spika kiliheshimika na spika hakuwa na tatizo na wabunge. leo hii mtu anatukana mubashara bungeni eti spika ni fala au sijui nini... Mara mwingine anakataa kutii amri ya spika mwenye mamlaka yake unategemea nini? Spika nae ni mtu na ana mihemuko yake, lazima afure pale kiti chake kinapodharauliwa. Kwa Suala la Mnyika juzi hekima tu ingetumika. Mnyika angekaa tu kimya kama alivyoamriwa wala asingetakiwa kutoka nje. Tena pale amri ya kutoka nje angejongea mwenyewe nje nani angemgusa? Angeonesha ana hekima na kila mtu angekuwa upande wake. Lakini kwa sasa mtu yeyote anayemtetea mnyika ni kwa sababu tu ya mihemukio ya kisiasa, kiukweli mnyika alidharau kiti cha spika.
Umesomeka Mkuu
Heshima kwenu,
Nimeangalia kwa makini clip inayoonesha Spika wa Bunge la Jamuhuri Mh. Job Ndugai akigombana na mbunge wa Kibamba Mh. John Mnyika. Nimetumia neno kugombana kwa kuwa kwa dhahiri Mh. Spika alikuwa na jazba. Aliamuru Mh.Mnyika atolewe nje na Segeant at Arms na asitie mguu bungeni wiki nzima. Kwa jinsi ilivyo nimeona kuwa hata kama Mh. Mnyika alikuwa na kosa, Mh. Spika hakutakiwa kuwa 'personal' kwenye matamshi yake. Naomba nitumie kimombo kodogo.
Personality refers to a distinctive set of traits, behaviors, styles and patterns that make out character or individuality.
How we perceive the world, our attitudes, thoughts and feelings are all part of our personality. People with healthy personalities are able to cope with normal stresses and have no trouble forming relationships with family, friends and co-workers.
What is a personslity disorder? Those who struggle with a personality disorder have great difficulty dealing with other people. They tend to be inflexible, rigid and unable to respond to changes and demands of life.
Julai 29,2015,Mh. Ndugai akiwa mgombea katika jimbo la Kongwa, alimpiga mgombea mwenzake rungu la kichwa mpaka akazimia. Mgombea huyo alilazimika kulazwa. Kama Mh. Mnyika angekuwa karibu na Mh.Ndugai, angepata kilichompata mgombea yule wa CCM. Pamoja na Mh. Kibajaji kumwita Mh. Mnyika mwizi, Mh. Ndugai hakujali, alikuwa na 'usongo' na Mh. Mnyika.
Bunge lenye kuvutia linahitaji Maspika wenye vichwa vilivyotulia. Hata Mh. Tulia, Naibu Spika, naye hutumia nguvu nyingi kuzima hoja zinazoichoma serikali. Waendesha vikao vya Bunge nao wanahitaji kupimwa kama wana 'disorder' yoyote.
Napenda kuwasilisha.
 
Kumbuka aliyesema mnyika mwizi sio spika. vilevile si kila aliyesikia sauti hiyo alijua nani kasema. Cha msingi utaratibu ungefanyika kufuatilia sauti ilitoka kwa nani, kwa teknolojia tuliyonayo angejulikana tu. Isingekuwa busara hata kidogo kusitisha shughuli zingine za bunge na kuanza kufuatilia nani kasema maneno yale.
Na ilposikika sauti ya "atolewe nje huyo" Supika alisikia, na akaamuru mubunge atolewe!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Na alisema Dont dare me Mnyika akajibu am not daring you! Akasema ,"Toeni huyu mtu nje" sio Mtoeni Mheshimiwa Mnyika no! Halafu akawaita Wale askari , "Nyie askari gani nyie?"
Kwa kweli una masikio mazuri.
uko sahihi, Spika nae hakutakiwa kufika huko alikofika. Lakini kwa vile naye ni binadamu hakuwa na jinsi. Saikilojia yake ilimsuta kabisa kwamba kadharaulika na hana mamlaka yanayo heshimika. Kawaida tatizo la kisaikolijia huja na jawabu lake, alichokifanya yeye ni kujaribu kuridhisha nafsi yake kama kujifariji. Ni watu wawili tu kati ya kumi wangeweza kukaa kimya baada ya tukio lile. Spika si wakulaumu, hakuwa na namna nyingine ya kufanya
 
Kwann usidhani saikolojia pia ndiyo iliyomhukumu Mnyika?Au ni spika peke yake ndiyo mwenye moyo wa nyama?Unadhani ni wangapi kati ya kumi wangekaa kimya kuitwa mwizi tena kwa kutajwa jina?
 
UKISOMA VIZURI DSM 5 UTAGUNDUA KWA KIFUPI HAKUNA MTU ASIE NA PERSONALITY DISORDER

YASOMENI MAANDIKO .
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Na alisema Dont dare me Mnyika akajibu am not daring you! Akasema ,"Toeni huyu mtu nje" sio Mtoeni Mheshimiwa Mnyika no! Halafu akawaita Wale askari , "Nyie askari gani nyie?"
Halafu baada ya wabunge kutoka,akasema Lusinde kiboko,amewakimbiza wapinzani wamekimbia!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kwann usidhani saikolojia pia ndiyo iliyomhukumu Mnyika?Au ni spika peke yake ndiyo mwenye moyo wa nyama?Unadhani ni wangapi kati ya kumi wangekaa kimya kuitwa mwizi tena kwa kutajwa jina?
Fikiria pia ni kiongozi gani angefurahia anaowaongoza kutotii amri zake na kumdharau?
 
Hapa kuna kudharaulika kiti cha spika. Spika ni mtu mkubwa saba katika hii nchi, anashikilia moja ya mihimili mitatu ya dola. Hata kama wewe ni mpinzani na kuna kitu kimekukera heshimu tu kiti cha spika. Kiti cha spika kikiheshimika hata anayekalia kiti hicho atajiheshimu. Linganisha na enzi za Pius Msekwa na Samuel Sitta, kiti cha spika kiliheshimika na spika hakuwa na tatizo na wabunge. leo hii mtu anatukana mubashara bungeni eti spika ni fala au sijui nini... Mara mwingine anakataa kutii amri ya spika mwenye mamlaka yake unategemea nini? Spika nae ni mtu na ana mihemuko yake, lazima afure pale kiti chake kinapodharauliwa. Kwa Suala la Mnyika juzi hekima tu ingetumika. Mnyika angekaa tu kimya kama alivyoamriwa wala asingetakiwa kutoka nje. Tena pale amri ya kutoka nje angejongea mwenyewe nje nani angemgusa? Angeonesha ana hekima na kila mtu angekuwa upande wake. Lakini kwa sasa mtu yeyote anayemtetea mnyika ni kwa sababu tu ya mihemukio ya kisiasa, kiukweli mnyika alidharau kiti cha spika.

So kuheshimu kiti ni pamoja na kusikiliza kila anachosema spika?? Why, kwa sababu yeye ni malaika?? Au kwa sababu yeye ni ccm??
Acha unazi, unadhani kauli ya mwizi ingetolewa na mpinzani hali ingekuwaje???
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Spika kuambiwa fala kwenye mic ni kosa la jinai lakini Mnyika kuitwa Mwizi kwenye mic hiyohiyo spika anasema hana muda wa kusikiliza kila kinachosemwa mara maneno hayako kwenye hansard ila fala aliyasikia typical double standard benaviour!
Kumtetea Ndugai kwa kilichotokea ni kuzidi kulidhalilisha Bunge. Ndugai sio Mungu ni binadamu wa kawaida sana, heshima ya ninadamu hatokani na cheo chake, bali inatokana na matendo yake. Jambo muhimu lililopaswa kufanywa na Spika mwenye hekima na anayestahili kuheshimiwa, ilikuwa ni kusymphathy na Mnyika, kwa sababu hata kama Ndugai hana masikio mia,lakini tusi lililoelekezwa kwa Mnyika kwamba ni mwizi "lilisikika mno". Kwa hiyo ambacho angefanya, hata kama hapendi, angeahidi kufanyika kwa uchunguzi kuona ni nani kamtukana, basi, hapo Mnyika na wabunge wengine wangeridhika na shughuli zingeendelea kama kawaida.

Spika mwenye hekima na akili, angetambua mapema kwamba mzungumzaji aliyekuwa akiendelea kuzungumza (kibajaji) alikuwa ameishalitibua Bunge upande wa wapinzani, kwa hiyo alichokifanya dhidi ya Mnyika kilipokelewa kama mkakati wa kishetani wenye dhamira wa kuwadhalilisha wabunge wa upinzani, jambo ambalo sio rahisi kuvumiliwa. Sasa wewe unataka Spika Ndugai avumiliwe kwenye mazingira kama haya? Ndugai anapaswa kuonyeshwa na kuelezwa wazi wazi kuwa alikosea, tena sana!
 
uko sahihi, Spika nae hakutakiwa kufika huko alikofika. Lakini kwa vile naye ni binadamu hakuwa na jinsi. Saikilojia yake ilimsuta kabisa kwamba kadharaulika na hana mamlaka yanayo heshimika. Kawaida tatizo la kisaikolijia huja na jawabu lake, alichokifanya yeye ni kujaribu kuridhisha nafsi yake kama kujifariji. Ni watu wawili tu kati ya kumi wangeweza kukaa kimya baada ya tukio lile. Spika si wakulaumu, hakuwa na namna nyingine ya kufanya

Kwa logic yako, Mnyika nae ni binadamu na usimlaumu kwa kutaka alie mwita mwizi awajibishwe tena bila miasira.
 
Fikiria pia ni kiongozi gani angefurahia anaowaongoza kutotii amri zake na kumdharau?

Kufurahishwa au kuchukizwa na reaction yako ni kipimo cha ustahimiivu na ukomavu wa kiongozi!Spika ana disorder,mara ngapi Tulia Ackson ameoneshwa dharau lakini kabaki kwenye utulivu ma kutumia sheria kuwachapa waliomdharau?Ndugai ana disorder,ndio maana alimpiga fimbo kicjwani mwenzake mpaka akazimia!
Ninachokipinga kwako ni kutoa excuse kwa Spika kwa kupanic wakati huo huo ukizuia hiyo excuse isitumike kwa Mnyika!
Nasema Mnyika alikosea lakini Spika alikosea zaidi!Mpaka akatoa adhabu ambazo hana mamlaka nazo,kumhukumu mtu kutohudhuria vikao wiki nzima si mamlaka yake!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Ndungai simwelewagi toka amzimishe na rungu mwenzie
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kwa logic yako, Mnyika nae ni binadamu na usimlaumu kwa kutaka alie mwita mwizi awajibishwe tena bila miasira.
Kufurahishwa au kuchukizwa na reaction yako ni kipimo cha ustahimiivu na ukomavu wa kiongozi!Spika ana disorder,mara ngapi Tulia Ackson ameoneshwa dharau lakini kabaki kwenye utulivu ma kutumia sheria kuwachapa waliomdharau?Ndugai ana disorder,ndio maana alimpiga fimbo kicjwani mwenzake mpaka akazimia!
Ninachokipinga kwako ni kutoa excuse kwa Spika kwa kupanic wakati huo huo ukizuia hiyo excuse isitumike kwa Mnyika!
Nasema Mnyika alikosea lakini Spika alikosea zaidi!Mpaka akatoa adhabu ambazo hana mamlaka nazo,kumhukumu mtu kutohudhuria vikao wiki nzima si mamlaka yake!

Sasa hapa mbona lawama zote zinaelekezwa kwa Ndugai?
Mara nyingine busara inabidi ifichwe ili mambo yasizidi kuharibika. Pia fahamu kwamba sehemu rasmi yenye mkusanyiko rasmi wa watu lazime kuwe na superior na subordinate. Kiti cha Spika kinaongozwa ma kanuni, sio busara. Spika alipomwambia mnyika azime mike na akae alipaswa atii pasipo kuhoji, maana ile ilikuwa ni amri ya spika kwenda kwa subordinate wake ambaye ni mbunge katika kikao cha bunge.
Kwa nini basi usimtendee kiongozi wako kinachostahili?
 
Wewe ni mgumu kuelewa na ngoja tu nikujibu hivyo hivyo!Unachosema hapa spika hapaswi kuwa na busara,cha msingi azijue kanuni!Lakini kumbuka pia katika kanuni,kuna kanuni ambazo zimempa yeye binafsi ya kutoa uamuzi kadri atakavyoona inafaa,sasa hapo kama hana busara tutegemee maamuzi gani?
Kwa mara nne nasema Mnyika alikosea,lakini spika alikosea zaidi!Kaonesha udhaifu mkubwa,kiufupi ni short tempered!Spika anajisahau na kujiingiza kwenye ushabiki,ili ujue alitoka nje ya mstari,angalia alivyomsifia Lusinde yeye ni kiboko mpaka amewakimbiza wabunge ukumbini!
Huu mjadala na wewe haufiki popote,nimeona comment yako moja juu kwamba uko hapa kumtetea spika so no matter what facts you get,bado utaendelea na kazi yako!
 
Hakika sijaona kosa alilofana spika Job Ndugai
 
Back
Top Bottom