Spika Ndugai ana personality disorder?

Spika Ndugai ana personality disorder?

Nisaidie wapi umewahi kumkosoa JPM,niwekee link tu nitaamini maneno yako!
Nimsaidie,JPM ameleta utamaduni wa kutengana kiitikadi kiasi cha kutotaka kusaidiana wakati wa dhiki( kuita wasaliti waliokwemda Kisongo kwa Lema), kuchepusha rambi rambi, kutimua wasiomkubali ndani ya ccm.
Hayo ni baadhi,orodha ni ndege.
 
He he heee.
Wananchi wa Congwa wananufaikaje na Mbunge wao?
 
Ingekuwa kibajaji yupo upinzani na amemwita mbunge wa ccm mwizi,chapchap ingeitwa kamati ya maadili na kumfungia miezi kumi
 
Nilikuwa napita tu kuelekea ghetto ndipo nikasikia huo mzozo bungeni .... Ghafla nikasikia "Mnyika mwizi". Hee nikashishikwa na butwaa gani hadi bungeni mtu anshindwa kupambanua maneno ya kuongea na kujikuta ameropoka km malaya wa kimboka anamwita mwenzio mwizi halaf anakingiwa kifua na spika halaf aliyekashifiwa ndo anafukuzwa tena km mbwa. Maana askar walikuwa wanagewa maneno ya kashfa na spika ili mradi tu wamuondoe mnyika kiudhalilishaji na wala c km inavyotakiwa kwa mbunge. Kwa kweli inatia huzuni na mm kwa mtazamo wangu watanzania hatuna spika na yule mbunge aliyesema mwizi uwezo wake wa kufikir n mdogo sana
 
heshima inapewa anayestahili kwanza. Mtoto mdogo hawezi bishana na mtu mzima halafu ajitetee hajapewa heshima ndo maana anabishana. Ukiheshimu kiti cha spika nacho kitakuheshimu
Mtu anakuwa mtu mzima tu endapo ana busara.
 
Diagnosis;
Schizophrenic with delusion of grandeur
Ni ugonjwa wa akili unatibika baada ya therapy ya muda mrefu
 
Spika kuambiwa fala kwenye mic ni kosa la jinai lakini Mnyika kuitwa Mwizi kwenye mic hiyohiyo spika anasema hana muda wa kusikiliza kila kinachosemwa mara maneno hayako kwenye hansard ila fala aliyasikia typical double standard benaviour!
Mkuu kwa maelezo yake maana yake ni kwamba kuna utoto mwingi sana katika jengo muhimu nchini mwetu. Too bad.
 
Kwa Maoni Yangu ni Kuwa Wabunge wetu wanaiga Tabia za Mabunge ya Nje! Katika Mabunge ya Nje yenye nidhamu ni Bunge la Senate la Marekani (sio house) Na katika Mabunge yenye zomea zomea nidhamu mbaya ni mabunge ya Uingereza na South Afrika. Ila yote yale yasio na nidhamu na Hili la Mfano, US Senate, wanayofanana ni Pale ambapo Speaker akimwambia mtu Muda Umeisha, wabunge asilimia kubwa tu wanamia Dakika Kama moja Kumalizia. To me ningekuwa Speaker hili huwa nalichukia sana. Ni bora uombe mheshimiwa naomba kwa dakika moja nihitimishe! Akisema sawa hitimisha Akisema hapana kaa chini!

Swala la Juzi!

MNYIKA: Myika ni Kijana Mahiri sana, Swala la Kuitwa ni Mwizi alikosema, Ila alishamtibua Ndugai kwa Kuwa Ndugai alishamwambia ameeleweka Mnyika yupo tu! Lile lilikuwa ni Kosa! Kwa hiyo isingelikuwa ni Hii Kuitwa Mwizi, Mnyika hili la kupitiliza muda au kufanya Arguments na Speaker analifanya. Na anatakiwa aidhibiti hiyo hulka. In short ni Tabia mbaya! Siwezi kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa ilihali nataka afanikiwe!

NDUGAI: Ndugai ni Mtu Mzuri sana kwa Upande wangu, Ila yeye bila kujua ana Mizaha isiyoeleweka Vizuri, na anaonyesha Ushabiki ambao kwa Kiongozi Mkuu wa Bunge kunawafanya Wahuni kama lusinde kufikiri wamepewa impunity kutumia lugha chafu kudhalilisha etc. Na kama mkimsikiliza lusinde akianza alikuwa akijigamba atamfanya mbunge fulani ajinyee nguoni.
Swala Lingine kuhusu Ndugai ni kuwa anahama kutoka Mzaha kwenda kwenye ghadhabu ghafla bila nitice au dalili. Mimi nilishamsoma kuna sauti fulani akianza kuitoa Nasema oh shit. Mimi Ningeshauri, Mimi ningeshauri aache utani mwingine, na Pia ikibidi Mbunge atoke nje amwambie atoke kwa hiyari yake na kama akikataa ndio atumie askari. Pili asitamke adhabu akiwa na hasira, amtoe nje ili apate muda wa kurejea na kutafakari kilichotokea.

KIFANYIKE NINI: Mh Ndugai Arejee Adhabu ya Mnyika mimi bado naona Mnyika ana kosa, Lakini Pia lusinde na aliyemuita Mnyika ni Mwizi wanastahili kupewa adhabu kwani Wamemdharau kwanza Mnyika, Pili Speaker na Tatu Bunge lenyewe. Kuhusu Ester Bulaya mimi sioni Kosa Lolote alilolifanya kwa Kuwaashiria Wabunge wa Upinzani watoke nje!
Kuhusu Halima Mdee mimi naona ni Uchungu, Wanaonewa Nje wanaonewa Bungeni, Yeye tu Juzi alilazimishwa kuomba Radhi, lakini anaona Mwenzake Kaitwa Mwizi Speaker hana habari! So ali act out of Pain na Wamama wako defensive! Hata kama Mbunge wa CCM akionewa utaona wamama wa CCM wakimtetea! Na walipotoka kule nje Halima hakuongea kitu! Anyway Ester na Halima hawana Kosa la Kustahili adhabu.
 
Diagnosis;
Schizophrenic with delusion of grandeur
Ni ugonjwa wa akili unatibika baada ya therapy ya muda mrefu
Us. Wanaita Bipolar ie Watu wawili wanaopeana zamu ndani ya mtu mmoja! Na zamu zinabadilishwa bila notice
 
Ingekuwa kibajaji yupo upinzani na amemwita mbunge wa ccm mwizi,chapchap ingeitwa kamati ya maadili na kumfungia miezi kumi

lusinde mimi ningekuwa Bungeni ningemfunza adabu, Maneno yake ya kanga za mitaani yasiyo na substance sawa! Lakini anitamkie maneno yasiyo na heshima kama kuniambia ati atanifanya ninyee nguo! Nangoja Bunge linaisha, kisha namfuata, nakata bonge la mtama! Akiwa anaenda chini Nakumba mkofi wa Machoni, Akitua chini nakwatua bonge la mteke linatua pale south kwa chief Butelezi, Akiinuka nachota ndoo! Kisha akiwa chini akiomba poo huku mkono mmoja kashika chini na mwinhine kaninyooshea kusihi namuuliza kule ndani sikukusikia vizuri ulikuwa ukisema?

Just kidding, but who knows that might help!
 
Spika kuambiwa fala kwenye mic ni kosa la jinai lakini Mnyika kuitwa Mwizi kwenye mic hiyohiyo spika anasema hana muda wa kusikiliza kila kinachosemwa mara maneno hayako kwenye hansard ila fala aliyasikia typical double standard benaviour!
mbaya sana, myika alipoomba aliyesema yeye mwizi atoe ufafanuzi speaker akadai hana masikio ya kusikia huku na huku lkn baada ya myika kutolewa nje na huku kukiwa na ninong'ono mingi bado aliweza kutambua sauti ya bulaya na mdee.
 
Spika kuambiwa fala kwenye mic ni kosa la jinai lakini Mnyika kuitwa Mwizi kwenye mic hiyohiyo spika anasema hana muda wa kusikiliza kila kinachosemwa mara maneno hayako kwenye hansard ila fala aliyasikia typical double standard benaviour!
CCM inalaana
 
Hivi vispika vya Tanzania vinaendeshwa na mihemko ya kichama, vinaona kama vyenyewe ndivyo vina haki ya kuongoza na kusema lolote wakati wowote na siyo wengine. Na trend hii ndiyo inaanza kushamiri humu hasa mods wa jf wanavyotupiga ban na kufuta maoni ya member ambao tuko against na matakataka ya hawa watesaji. Nawasilisha
 
Back
Top Bottom