Spika Ndugai aache kupotosha umma kwamba ajira zinatolewa kwa upendeleo wa kikabila na kikanda

Kwa ratio hiyo sioni tatizo hapo. Kumbuka kanda ya ziwa ndio kanda yenye mikoa mingi na watu wengi kwahivyo ata namba ya wahitimu lazima iwe kubwa kulinganisha na kanda zingine.
Unachoongea siyo kweli. Walimu hawapigiwi kura bali ni qualification.

Random sampling:

Wanafunzi wa vyuo vikuu kwa miaka mingi:

1) Kagera
2) Kilimanjaro
3) Mbeya
4) Iringa

Uwiano huo huo unauona kwa wakufunzi.

Kwenye population, mikoa ya kanda ya Ziwa ina-count 10% ya population yote.
 
Kwenye hili kama hujamuelewa Ndugai utakuwa na chuki zako tu binafsi, huyu Mzee sijawahi kuwa kwenye mstari wake ila aliyosema ni mnufaika wa hizi dili za ajira ndio ataona Ndugai anabutua mpira wao. Tunajua na ushahidi upo ajira hizi zilikuwa tayar zishapata watu kabla ya maombi na hapa kuna kundi la wahuni walikuwa wanaenda kujaza vijana wao wa kusifu na kuabudu.
 
Kwa wabunge ndio wapeleke watu wa kuajiriwa? Je namna ya kuwapata huko kwenye majimbo yao, utaratibu upo? Hapa sio kuzalisha tatizo juu ya tatizo. Na je, taarifa za wanaofaa kuajiriwa toka kwenye majimbo ziko wapi? Kati ya jambo la hovyo ni hili. Athari zake ni kubwa mno ikiwa ni pamoja na kuruhusu rushwa kutembea zaidi. Kazi ya bunge ni kutunga sheria na kusimamia serikali. Haya ya kupeleka waajiriwa ni ujinga mwingine wa bunge letu.
Nchi iongozwe kwa taratibu, na taratibu za kuajiri watu zipo. Haya mambo ya maeneo haya yakiendelezwa muda si muda tutaibua vita ya kikanda ama kijimbo. Tuache vigezo vilivyopo vitumike na anayevifikia apate ajira. Kama vina kasoro basi virekebishwe, nje ya hapo kuna janga kubwa linainyemelea nchi.
Mhe. Ndugai amenena jambo la muhimu sana kwa Taifa letu, jambo ambalo wengi walilifumbia macho lkn lina hatarisha umoja wa taifa letu nalo ni mgawanyo wa ajira na nafasi za uteuzi serikalini ulio sawia na wa haki, kimaeneo na hata kiimani, sio sahihi kujaza ktk utumishi wa umma watu wa aina mmoja halafu wengine wengi wakatupwa nje, hilo sio sahihi kabisa kwa ustawi na uzalendo wa taifa letu, lazima jambo hilo.litazamwe kwa kuzingatia sifa, usawa wa maeneo na hata usawa wa imani zote kushiriki ktk ujenzi wa taifa lao utaleta na kuimarisha uzalendo.

kama tuna bisha kauli ya Mhe. Spika nashauri kila taasisi ya Serikali ifanye utafiti kubaini ukweli, na utaona kuna aina ya watu fulani ndio wame hodhi karibu nafasi zote ktk taasisi za serikali.
 
Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amepotosha umma mchana kweupe kudai ajira za ualimu zilizopita zilitolewa kwa misingi ya kikanda na ukabila kwa sababu ukiachilia mbali jina moja lililojirudia kila ukurasa, mchakato wa ajira zilizopita ulifanyika kwa haki na kila mwenye sifa alipata nafasi ya kuajiriwa.

Pia soma > Spika Ndugai: Ajira ziwe zinazingatia usawa wa Kijografia

Katika hatua nyingine Job Ndugai anauliza wabunge kama wapiga kura wa majimbo yao waliajiriwa kwenye ajira zilizopita. Ebu tujiulize, wapiga kura anaowasema Job ndugai ni akina nani..? Je, ni watanzania? Kama ni watanzania walitokea wapi kama sio huko huko majimboni anakokusema spika Ndugai?

Je, Spika Ndugai ana majina mfukoni ya vijana wa jimbo lake waliompigania kwenye uchaguzi anaotaka kushinikiza waajiriwe?

Nauliza hivi kwa sababu kabla mchakato wa ajira kutangazwa baadhi ya wabunge walichukua majina ya vijana majimboni kwao kwa madai kwamba wanaenda kuwapigania wapewe kipaumbele cha ajira kwa kisingizio kwamba wanajitolea. Kwa hiyo inawezekana Spika Ndugai nae yupo kwenye kundi hili ndio maana anapiga kelele ili ajenda yake ifanikiwe.

Na, kama ajira zilizopita anasema zilikuwa zimegubikwa na ukabila mbona hakusema kipindi hicho anakuja kulisema hilo leo?

Kwa kipindi chote ambacho ajira zimekuwa zikitolewa enzi za magufuli spika Ndugai alikuwa kimya wala hatukusikia akiagiza kamati za kisekta kufanya uchunguzi lakini leo kwenye utawala wa Rais Samia anaibuka na kudai kamati hizo zifanye kazi yake. Je hiki ni kielelezo kwamba Spika Ndugai alimwogopa magufuli na anamchukulia poa Rais Samia?

Kimsingi kelele za spika ndugai zimebeba ajenda binafsi nyuma yake na kama Tamisemi watazisikiliza zitakuja kuharibu mchakato wa ajira kwa sababu kama yeye amekuja na kigezo cha ukabila, mwingine atashauri kigezo kiwe umri na mwingine anaweza kushauri kigezo kiwe ni rangi nyeupe, mwisho wa siku vigezo vinakuwa vingi kuliko ajira zenyewe.

Kwa hiyo ni vyema Tamisemi mkafanya kazi yenu kwa vigezo mlivyojiwekea ili kila mwenye sifa aajiriwe as long as amehitimu mafunzo ya ualimu na ana vyeti halali lakini kutaka kusikiliza kila anachosema mwanasiasa ndio kiwe mtakuja kuharibu mchakato mzima kwa sababu wanasiasa naturally ni wabinafsi ambao kazi yao kubwa ni kulinda maslahi yao hasa ya kibunge.
ndugai anaumwa pale tu bungeni anawabunge fake aliowaingiza kilaghai sasa anauhalali gani kuzungumzia hayo
 
...

Huo mseto umuhimu wake unaonekana leo? Spika alikuwa wapi wakati Jpm anaweka watu toka Kanda moja?
Wewe kipindi JPM anafanya hayo uliyaona na je ukikuwa na ujasiri wa kuyasema hadharani achilia mbali hapa nyuma ya keyboard? Kila jambo na wakati wake na kukwepa hatari ni bora kuliko kuikabili bila silaha kwa kigezo cha ujasiri.
Kuna muda inabidi umpe adui nafas akushambulie ila ukiibuka unampasua vizur kabisa.
Muache Ndugai na wenzake waseme yaliyojificha.
 
Back
Top Bottom