Spika mstaafu wa Bunge la Kenya awaasa Wabunge na Spika Job Ndugai kuwa wasijisahau kwani kuna maisha baada ya siasa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
86,437
147,138
Spika mstaafu wa bunge la Kenya amewaambia wabunge wa Kenya mbele ya mgeni rasmi Spika wa Tanzania mh Job Ndugai kuwa waache kiburi na kujikweza kwani kuna maisha baada ya siasa.

Spika huyo mstaafu amewakumbusha wabunge hao kuwa wafuasi wao wanaowashangilia leo ndio hao hao watakaowatukana pindi watakapostaafu uongozi.

Spika mstaafu amesema ni miaka 15 sasa tangu aachane na siasa na jamii imempokea vizuri kwa kuwa hakuwa " Mjivuni" alipokuwa kiongozi wa umma.

Source: Citizen tv

Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom