WanaJF,
Wabunge wetu wamekosa maadili! Leo hii katika kipindi cha Hoja za Serikali Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi toka Bungeni Dodoma, Mheshimiwa spika Anna Makinda amelazimika kuwaambia kwa ukali waheshimiwa wabunge kuacha kupiga kelele na kuwa makini na kile kinachosemwa.
Mheshimiwa Spika Anna Makinda alilazimika kuwatoa nje kwa kumwambia Sanjenti wa Bunge kuwatoa nje Mheshimiwa Mariam na mwenzake waliokuwa wakiongea kwa sauti na kusababisha maingiliano na hoja zilizokuwa zinatolewa na Mheshimiwa Mbatia aliyekuwa anawashangaa wabunge wa CCM wanaosema elimu inayotolewa ni bora wakati Mheshimiwa Rais Kikwete akiwa mjini Mbeya alikiri kuwa elimu inayotolewa ni dhaifu!
Pia katika hali isiyo ya kawaida, inayoonyesha na kuthibitisha uvunjifu wa maadili na kutokuwa na heshima sehemu za kazi, TBC1 wamemwonyesha Mheshimiwa Komba akiwa anabofyabofya simu yake bungeni na kutabasamu wenda kutokana na alichokuwa akikiandika au kilichomfanya abofye simu yake na kusahau kilichompeleka Bungeni!
Nini umuhimu wa Bunge kuwa na kamati ya maadili ya Bunge?