Spika Makinda awatoa nje wabunge kwa kuongea!

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,981
144,283
Spika Makinda ameamuru kutolewa nje kwa wabunge wawili kwa kuongea bungeni.

Hata hivyo,TBC 1 hawakuonyesha wabunge husika walioagizwa kutoka nje.Sasa sijui kama kweli walitoka au laa kwasababu TBC hawakuonyesha ama wakitoka nje au wakikaidi.Spika alisisitiza kwa kumuagiza askari awatoe nje.Tatizo camera za TBC zilikuwa zinamuonyesha spika tu badala ya walioagizwa kutoka nje!
 
WanaJF,

Wabunge wetu wamekosa maadili! Leo hii katika kipindi cha Hoja za Serikali Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi toka Bungeni Dodoma, Mheshimiwa spika Anna Makinda amelazimika kuwaambia kwa ukali waheshimiwa wabunge kuacha kupiga kelele na kuwa makini na kile kinachosemwa.

Mheshimiwa Spika Anna Makinda alilazimika kuwatoa nje kwa kumwambia Sanjenti wa Bunge kuwatoa nje Mheshimiwa Mariam na mwenzake waliokuwa wakiongea kwa sauti na kusababisha maingiliano na hoja zilizokuwa zinatolewa na Mheshimiwa Mbatia aliyekuwa anawashangaa wabunge wa CCM wanaosema elimu inayotolewa ni bora wakati Mheshimiwa Rais Kikwete akiwa mjini Mbeya alikiri kuwa elimu inayotolewa ni dhaifu!

Pia katika hali isiyo ya kawaida, inayoonyesha na kuthibitisha uvunjifu wa maadili na kutokuwa na heshima sehemu za kazi, TBC1 wamemwonyesha Mheshimiwa Komba akiwa anabofyabofya simu yake bungeni na kutabasamu wenda kutokana na alichokuwa akikiandika au kilichomfanya abofye simu yake na kusahau kilichompeleka Bungeni!

Nini umuhimu wa Bunge kuwa na kamati ya maadili ya Bunge?
 
Spika Makinda ameamuru kutolewa nje kwa wabunge wawili kwa kuongea bungeni.

Hata hivyo,TBC 1 hawakuonyesha wabunge husika walioagizwa kutoka nje.Sasa sijui kama kweli walitoka au laa kwasababu TBC hawakuonyesha ama wakitoka nje au wakikaidi.Spika alisisitiza kwa kumuagiza askari awatoe nje.Tatizo camera za TBC zilikuwa zinamuonyesha spika tu badala ya walioagizwa kutoka nje!

Pengine niwa wabunge wa ccm ndo maana TBC wakachengesha camera wangekuwa wa CHADEMA wangekomaa nao
 
Hivi inakuwaje TBC peke yake ndio inarusha live kipindi hicho cha Bunge ?

.....ni sheria ama ni kitu gani hasa ?
 
Spika Makinda ameamuru kutolewa nje kwa wabunge wawili kwa kuongea bungeni.

Hata hivyo,TBC 1 hawakuonyesha wabunge husika walioagizwa kutoka nje.Sasa sijui kama kweli walitoka au laa kwasababu TBC hawakuonyesha ama wakitoka nje au wakikaidi.Spika alisisitiza kwa kumuagiza askari awatoe nje.Tatizo camera za TBC zilikuwa zinamuonyesha spika tu badala ya walioagizwa kutoka nje!

Safi sana, walkuwa wanapiga kelele wakati mijadala inaendelea.
 
Kamilisha habari kwani hili ni jukwaa la mambo ya maana na yenye uhakika kwa kina.
 
Watakuwa wa magamba au waliberali ndo maana tbccm haijawaonyesha. Wangekuwa makamanda wangeoshwa mpaka wanatoka mlangoni
 
kasema mh.Mariam na mwenzako tokeni nje... sasa sijui ni Mariam nani... tutajua tuu sasa hv
 
Maccm yanataabika sasa! Yanachukua chao mapema

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hivi na CCM wanavuruga bungeni?

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Hivi inakuwaje TBC peke yake ndio inarusha live kipindi hicho cha Bunge ?

.....ni sheria ama ni kitu gani hasa ?

Nadhani Warioba kaliona hilo kwenye Ibara hii ya 30.-(1) Kila mtu anao uhuru wa-
(a) kutafuta, kupata na kutumia habari na taarifa na
kusambaza taarifa hizo; na
(b) kuanzisha vyombo vya habari na njia nyingine za
upashanaji wa habari bila kujali mipaka ya nchi.
(2) Vyombo vya habari vitakuwa huru na vile vile vitakuwa na:
(a)haki ya kupata, kutumia na kusambaza habari na taarifa
wanazopata;

kwa kuwamirikisha uhuru huu kwa TBC peke yake baada ya hii rasimu kupitishwa haita kubarika tena.
 
Back
Top Bottom