Bepari, jee na wewe uu mmoja wa hao wanao amini hivyo?, ana umejikuta umeingia kwenye mtego wa panya unaowanasa waliomo na hata wasiomo.Which happens to be the truth, good morning...
Mr.Mak, haya ni maneno ya busara sana.naomba wabadilishe heading waseme Dodoma hearing and Dar hearing. Ninachoomba wanasiasa wa ccm+cdm+cuf+... wasijifanye hiyo ni isue yao bali hii ni isue ya watanzania wote. watu waache ushabiki, maana ushabiki utapoteza dhana nzima ya watu wote kuhusishwa na matokeo yake yatachukuliwa mawazo ya Makamba+Slaa+Lipumba+Mrema+Dovutwa+... halafu wasema wananchi wote mawazo yao yamesikilizwa.
Rweye, don't be too negative kwenye jambo lenye manufaa kwetu, hata kama cut and paste toka kwa jirani, hiyo hiyo cut and paste unaiboresha ili ifiti kwenye mazingira yako.Wenye vurugu ni wao wenye kuleta mswada feki..kwanza wanatuletea mswada wa kenya ..hapa ni kenya ama ni Tz? Je sisi wakenya ama sisi ni wa Tz ? Tunataka muswada utungwe na wa Tz wenyewe na utoke Tz,..full stop, vinginevyo hii ni vita Murra!
Lakini kwanini kila pale watanzania wanapotaka haki zao wanahusisha na vyama vya upinzani? kuna mtu anafikiria Tanzania ya leo ni ile ya CCM fasiiiiiiiiiiiiii sana hadi watu wanaanguka chini kwa kushangilia? Kama kila siku watahusisha na vyama vya upinzani kamwe hawatafika mbali hiyo yote yanafanywa na watanzania walioamua kuondokana na upuuzi.
Jana nimepitia taarifa ya habari ya saa 2usiku, ukiangalia chanzo cha kutokuelewana kati ya wakuu wa kikao kile na watoa hoja/maoni ni baadhi ya maswali waliyouliza watoa hoja ya kutaka kujua zaidi undani wa ule mswada, kwa mfano, Dkt Slaa aliuliza swali la kutaka kujua aina ya muungano uliopo kwa sasa ivi kati ya Tanganyika na Z'bar. Hapo ndo yakaibuka majibu yenye jazba ambayo yaliashilia kuegemea upande wa chama tawala. Dodoma nako vurugu zimeanza pale wanafunzi waliokuwa na hamu na shauku ya kutaka kuchangia walipokosa nafasi ya kuingia ndani ya ukumbi kwani ulikuwa mdogo kitu ambacho kilikuwa hakina tija sana badala kwani ya viongozi wa kikao hicho kuona kuwa ukumbi hautoshi wangetafuta njia mbadala ya kuendesha mkutano huo aitha kwa kutafta sehemu ya wazi au wangetumia ukumbi wa chuo kikuu cha Dodoma lakini badala yake wanafunzi hao wakafukuzwa kwa kupigwa mabomu na polisi!, JAMANI, yan mpaka hatua hii ya kutaka kupanga mipango jinsi ya kuiongoza nchi hii bado tuu tunakatazwa kua tusitoe maoni yetu! HAKIKA haitakubalika! wakatae wakubali MSWADA huo ulotolewa bado tuna walakini nao, kwa nini watulazimishe kupitisha sheria mbove hivoooo???? Wasivilalamikie vyama vya siasa kwa namana yoyote ile, wanachotakiwa kujua ni kuwa UOVU na HILA zao sie wananchi tushazigundua!!.
Kuna mwelekeo wa kupanga kuhusisha ukosoaji wa mswada huu na Chadema. Serikali na ccm wanatumia mbinu hii kukwepa hoja zinazokosoa mswada huo.
Jana mkuu wa mkoa wa Dodoma alidai waliozuiwa nje ya bunge walikuwa ni wanafunzi wa udom ambao waliletwa na Chadema. Lakini siyo wote walikuwa wanafunzi na wanachama wa Chadema. Tambwe hiza alizomewa Karimjee wakadai ni Chadema. Lakini hata ccm walimzomea!
Kama nia ya serikali na ccm ni kuupitisha huo mswada ulivyo basi watatumia kisingizio hicho cha kijinga kuupitisha, wakidhani wanakomoa Chadema. Wakifanya hivyo watahatarisha Amani.
Kwanaza ni kweli kwamba huo mswada umekaa vibaya na mapungufu mengi mno. Pili, ni dharau kubwa sana kwa watz ambao siyo Chadema kuwaona kwamba hawana akili ya kuona yaliyomo kwenye huu mswada.
Tatu, basi hata kama mko sahihi kwamba ni wanachama wa Chadema pekee wenye akili na uwezo wa kuchambua uzuri na ubaya wa huu mswada, wao pia ni watz hivyo wana haki ya kusikilizwa.
Nne, kukataa hoja kwa sababu humpendi mtoa hoja ni kusokota sayansi mantiki. Shuhulikia hoja usimshuhulikie mtoa hoja!