Spika akalia kuti kavu

Leo ndio wamemuona hafai? Nawashauri wabunge wote wa CUF waendelee kuzipiga meza zao (kushangilia) kwa kila jambo linalosemwa na Spika ili kuwakomoa wapinzani. Mind you, CUF ni chama tawala.
 
Tanganyika ipo wapi wewe ? Unatafutwa kufungwa ? Lile ni bunge lilitokana na nchi mbili na baraza la Wawakilishi ni la nchi ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ,wakati mwengine jaribu kuandika kama mtu mwenye akili.

We mchoma makanisa ndo unalitambua hilo mbona kwenye mikutano yenu ya uamusho huwa hamyasemi?
 
naunga mkono hoja, apigwe chini

Tatizo lilipo ni kwamba endapo hiyo kura ikipigwa basi Spika au Mwenyekiti ataamua kutumia utaraibu wa kusema "NDIYOOOOOOOOO" au "HAPANAAAAAA"

Hiyvo katika BUnge letu ni kwamba wabunge asilimia kubwa ni wa CCM, na wataogopa kama kawaida yao kusema "HAPANAAA" kwa kuhofu kuwajiobishwa na vitisho vya LUKUVI.



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Hivi?? mbona naanza kusikia harufu ya Muungano kuvunjika?...au naota nini!!!!
 
Wamtoe tu ameshindwa kazi hata kabla ya hii ajali, hawezi kuhimili hoja nzito.. Anakimbilia kanuni hairuhusu na jambo hili liko mahakamani. Mtoeni haraka kabla hajaleta maafa zaidi.
 
for me ni bora huyu mama kuwa spika kuliko yule ayub ndugai...hili lijamaa ovyo sana linapokalia kiti,.mbabe,hakubali kushindwa
 
Huyu spika hafai, ni mbaguzi. Kila hoja itakayowasilishwa na upande wa upinzani atiikataa hata kama ina tija. Embu angalia alivyofanya jana. Alikataa hoja ya Hamad Rashid lakini akakubali ilipowasilishwa na gamba mwenzake. Spika huyu alaaniwe kwa kuendesha bunge kwa ubaguzi
 
Mh, hata mi nilimuona jana anavyowaka mara oh bado nafanya mawasiliano, labada hakuwa amepata habari za kuaminika au hakuna kifungu kinachomruhusu kuahirisha bunge kwa matukio kama hayo? manake pia nilimuona waziri Nchimbi ndiye aliyekuja kutoa hoja ya kuahirishwa kwa bunge.

Nazani hapa ilitakiwa busara tuu si vifungu...........yako mambo ambayo nazani yana ulazima wa kuamuliwa bira ya vifungu na naamini vifungu havitoi mwongozo kwa kila kitu.
 
Spika kung’olewa?

Baadhi ya wabunge wameanza kuwahamasisha wenzao kupiga kura ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge.
Wabunge hao walifikia hatua hiyo kwenye kikao cha dharura walichokifanya jana katika Ukumbi wa Pius Msekwa kwa lengo la kufanya maandalizi ya kwenda Zanzibar kuhudhuria msiba wa wenzao waliozama katika ajali meli ya Skagit.

Mbunge wa Mji Mkongwe, Muhammad Ibrahimu Sanya (CUF), alisema Spika Makinda hana utu ndiyo maana aligoma kuahirisha shughuli za Bunge ili kutoa nafasi ya watu kushiriki kwenye jambo hilo.

“Huyu Spika hatufai, yaani vifo vikitokea kwa watu wa Bara yeye ndiyo ataona kuna uzito…hapa alikufa Amina Chifupa tukaahirisha Bunge, sasa iweje wenzetu wamekufa kule Zanzibar yeye akatae kuahirisha shughuli za Bunge? Jamani tujipange kupiga kura za kutokuwa na imani naye, ameonyesha kushindwa kulihimili Bunge,” alisema.

Mbunge mwingine kutoka Zanzibar alisema hawaoni sababu ya kuendelea na mjadala wa bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa sababu wapiga kura wao ndio waliofariki dunia.

“Tuna raha gani ya kuendelea kujadili hotuba ya bajeti, huyu Spika tumedhihirisha hana uwezo wa kutuongoza, hatufai, waliokufa kule ni binadamu si paka wala wanyama,” alisema.

Chanzo:Tanzania daima
apigwe chini la sivyo aliombe taifa radhi na aache kupendelea magamba wa mapwepande
 
huyu mama asubiri kile kipindi cha wabunge wa East africa wakiomba kura ndo aanze kusema sirii minutes to explain yourself and sirii question ananiudhi na ubabe wake haki ya MUngu
 
Hii ndiyo athari za kuchagua watu kwenye ngazi mbali mbali za uongozi kwa ajili ya kutumika kwa maslahi ya wachache.Sote tunatambua jinsi huyu mama alivyochaguliwa kuwa Spika Kwa ajili ya kutumika na kundi dogo la Mafisadi wakisaidiwa na vyombo vya dola.Hakika ni aibu kwa mama wa umri huu kutumika kama zana fulani inayotupwa jalalani mara baada ya matumizi.Watanzania tumekuwa watu wa daraja katika dunia hii inapokuja jambo kubwa kama hili la ajali inayogharimu uhai wa Watu huku akina Makinda wakiona ni jambo la kawaida tu eti kwa vile halijawagusa waliowachagua kuwa Maspika.
 
Back
Top Bottom