Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge

Ushauri wangu kwa Ndugai, kutokana na kusumbuliwa mara kwa mara na magonjwa, angeomba kupumzika ili imjenge kiafya na kuisimamia afya yake vyema, aachane na mambo yanayoweza kumletea msongo wa mawazo kwa namna moja ama nyingine kwa afya yake na familia yake.
 
Pole mkuu PM hizi ni changamoto katika kazi lazima zitokee ili kukuimarisha kama utazimudu lakini kama zikikumudu hilo ni tatizo tena linaweza kuwa janga.

Kwa jicho la tatu naona hili linaweza kuwa janga kwako sababu umegusa pembe kuu mbili na uhakika pembe hizo zilijadili ile makala yako nakuhitimisha kwa kukuonyesha nini thamani ya pembe

Naamini wewe si mwanachama wa chama chochote cha upinzani labda uwe umejiunga juzi ila kwa kujumuishwa kuwa wewe ni kada wa upinzani na si mwanahabari huru tambua kuna mazito

Sikuombei mabaya ila tambua kuna nia mbaya juu yako hivyo pambana haswa kwa umakini Mungu akusaidie.
 
heading ni swali, na aulizaye hutaka kujua. hata hivyo, bunge letu lina utendaji usio ridhisha. limejaa ushabiki wa kichama na kuwa mtetezi wa kila mswaada uletwao na serikali, badala kuwa wawakilishi wa wananchi ktk kuisimamia serikali. linajidhalilisha, halidhalilishwi.
 
Mimi simlaumu spika kwani kiswahili cha Mayala ni cha kitanzania na spika amefanana sana na Nkurunzinza kwa hiyo labda hajaelewa maana ya kujipendekeza.
 
Hakuna cha ajabu hapo, cha msingi tupate tafsiri ya neno " linajipendekeza "
Tujue maana yake,ni dhihaka, kejeri, matusi , dharau, au vinginevyo, Pia maudhui ya makala yake, tusianze kupiga ramli hovyo
 
Tatizo ni kwamba mkuu Paskali kaongea UKWELI mtupu, na kama mjuavyo ukweli unauma. Hivi huyu ndugai anafikiri vipi? Mbona yeye alimpiga mtu na fimbo kidogo amuue na hakuna sheria yeyote aliyochukuliwa?
 
Back
Top Bottom