Spidi ile JK wanamkimbizia wapi..!?

Si tumeambiwa yuko mlimani anauza sura? Au ni mwanae manake kuna wakati ananyanyuka na Presidential convoy!!!!!
 
kupanda mlima hadi kileleni ni siku tano (kwedna na kurudi). Kupanda nusu ni siku tatu (kwenda na kurudi)

atafika mbele ya mandara hut ni safari ndefu
Alikuwa zaidi anazindua program....ya wanawake, yeye si mpandaji kwa siku zote tatu za ziara yake K'njaro.
 
Zile gari zimetoka moshi kumuwahi kumchukua airport hapa dar, amerudi jioni hii
 
Huyu jamaa kesha toka moshi?

Nasikia jana alikuwa himo akikagua magodown ya mahindi ya watu binafsi akiwa na mrema, mrema akamwambia hayo magodown ndo yanasafirisha mahindi kwenda kenya. Je kwani ya serikali hayapo akayakague? Kama hayapo basi ayatengeneze ili akapate kuyakagua
 
Hivi kuna watu waalikuwa wanaamini kuwa bwamkubwa kapanda mlima hadi kileleni..!? Kweli humu kuna ma-greti sinkers.
 
Mkeshaji,

Unasema msafara umepita kwa speed isiyo ya kawaida kwani standard ya speed kwa msafara wa Prez ni ngapi km/hr?

Na je huo ulikuwa unaenda kilometa ngapi wka saa?
Mkuu ile spidi ya leo mi huwa naionaga kwenye motor racing championship tu.
 
Speed 160km/hr umewezaje kumuona aliye ndani ya gari kama ni JK???
 
Hapana hakupanda juu zaidi ya Marangu geti kuu

Ni ukweli kwamba Mheshimiwa Rais alikuwa mgeni rasmi jana kuwatakia kila jema wapanda mlima Kilimanjaro kutetea haki za akina mama, na sherehe hii ilifanyika Marangu gate, na hivyo hakupanda mlima. Picha za Mheshimiwa akipunga bendera kuanzisha safari, na akiwahutubia wapandaji hizi hapa chini (Source: michuziblogspot.com).



 
Mkuu kwani ilikuwa Rais akutane na madaktari?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…