Specifications za Tigo Kitochi 4G

Specifications za Tigo Kitochi 4G

Za kuambiwa changanya na zako
Hako ka zuri kukafanya kitoch tu vipi ukaaji wake na chaji?
Ukaaji wa battery ni wa kawaida.
Mimi hapa nimeandika kwa tecno T402 yenye thamani ya sh 30,000 lakini nainjoi kutumia, chaji inakaa siku 3. Lakini haka kadudu nimenunua jana nikachaji, na sasa hivi nimekachomeka chaji tena.

nimenukuu kutoka kwa mdau huko juu.
 
radika mMmi binafsi chaji yake haijamaliza masaa 48, kwenye ukaaji wa chaji kuna udhaifu kidogo. Mimi kitecno changu hapa huwa kinakaa na charge siku tatu huku nasoma mtandaoni, nachezesha nyimbo na wakati fulani kusikiliza radio.

Ila kwa ujumla bei yake ni rafiki kwa sababu haka kasimu kana ofa. Yaani badala ya kununua modem kwa 30,000/=, chukulia umenunua modem kwa 48,000 yenye uwezo wa kupiga simu, kusoma sms na GB za bure mwaka mzima.

Ila nasisitiza kukatumia kana ugumu kidogo.
 
Ipo hivi.

Unaponunua simu toka mtandao husika like Tigo, Voda nk. wanakupa offer ya GB, Sms and dakika. Hii offer inaweza kuwa activated hata kwenye line yako ya siku zote so no need kwa wao kukupa line mpya unless ukihitaji.

Inawezekana vipi kuunga hii offer kwa line ambayo haikuwa katika simu? Jibu ni kwamba wanatumia IMEI za simu husika then mteja atapewa maelekezo ya kutuma Sms kwa service provider kuomba hiyo offer na pindi wakiconfirm IMEI yako ipo katika offer watakupa hiyo offer yako na kama umeshapata pia watasema kama imeshatumika au Ssmu yako haipo katika hiyo offer.

So hizo IMEI ni deal sana, get them Generate, Tweak and use on other sim cards to get same offer at your own risk.

Wasalaam.
 
Smart Guy, Ni simu za Kai os, aka firefox os za zamani, kama unataka simu serious achana nazo os yake ni nzito na haipo optimized kwenye hizo simu, browser yake pia haifai kwenye hizo simu, naona wametoa ucweb inasaidia kidogo ila still bado. Mfano kwenye simu yangu hata freebasics hawaitambui.

Kama unataka kutumia kama jina lake lilivyo kitochi na kuifanya iwe 4G modem sio mbaya inakubali vyote USB tethering na Wi-Fi hotspot,

Ukaaji chaji kama unaitumia kama kitochi kwa kuweka network edge na kuzima data inakaa na chaji siku kadhaa kama vitochi vyengine ila kama unatumia na 4G ama 3G na data ipo on inakaa na chaji kama smartphone nyingine inaweza hata isimalize siku matumizi yakiwa makubwa.

Uzuri wake ni operating system mpya hivyo kuna updates za mara kwa mara na mambo mapya yanaongezwa.
 
Mr Easy, Samahani naomba nikuulize, naweza kufungua Word Document au PDF files kupitia hiyo simu, na vipi kuhusu Word na Adobe Reader, naweza ku-install kutokea kwenye app store yao? Pia naomba kufahamu kama ina slot ya kuweka Memory Card.
 
homomorphism Kule nyuma nilisema haka kasimu kana tabia zote za familia ya Tecno, inawezekana wanajuana au wameshea mzazi mmoja (joking)

Yaani kuna muda unataka ufanye jambo fulani, lakini unakasubiria kenyewe mpaka kajifikirie kwanza. Yaani mfano ulikuwa ndani huko, sasa unataka kurudi home screen ili labda upige namba fulani, kenyewe kanazira mpaka kajifikirie wee!

Nimecheki kwenye store yao (Play store kwa lugha yetu wa Android) wana PDF ipo ila sijaijaribu ila nadhani inafungua.
Labda tuhitimishe hivi; usinunue hii simu kwa lengo la kupata huduma kama za smartphone, hakikisha una smartphone yako ndio ununue hiki kitu.

Hiki kisimu kinamudu vyema majukumu ya
1. Kupiga, kupokea na sms
2. Tochi
3. Kama modem
4. Kikokotoo
5. Radio na muziki
 
Sauda, Mimi ninayo Nokia 8110 4G inatumia same os Kai, ila bei ni ndefu kidogo. Pia ipo Nokia 2720 flip na Nokia 800 tough zote zina Kai os lakini bei pia ipo juu kidogo zote ni zaidi ya laki 1.

Na Kai os wanalenga sana mitandao ya simu, na sio watengeneza simu, simu zao nyingi ni order za mitandao.
 
Sauda, Hakuna, hata hizo unazoziona za elfu 50 mitandao ya simu wanazisubsidize ndio maana unaziona bei rahisi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom