Ahsante sana Mwalimu Kashasha, haka kasimu kama lengo lako ni kupata MB chukua, ila kama ni good performance soma maoni yangu.
1. Matumizi yake ni magumu kidogo. Mfano back button tuliyoizoea haina kazi hiyo. Badala yake home button (kitufe chekundu/cha kukatia simu) ndio ina kazi hiyo. Ukiandika 0754 333 333 ukitaka kwenda home na uandike namba nyingine, hakuna shortcut mzee, futa moja moja.
2. Ina OS ya upweke inaitwa KiOS, zile apps ulizosikia redioni kama Facebook, Whatsapp nk ndio hizo hizo. Store yao ina apps ambazo wame-recommend udownload hizo tu. Hakuna sehemu ya kusearch ili udownload unazotaka wewe, ukidownloadia nje kwenye browser haziwezi kufunguka. (Hizo Facebook na Whatsapp inawezekana waliwafauta wahusika wenyewe akina Mark na kuwekewa direct).
3. Facebook yake huwezi kubadilisha picha ya profile wala kupost kwenye news timeline, unapakia vizuri tu but ukifika hatua ya "done" cursor inapotea, hata ukiscroll inakuwa haikolezi maandishi ulipofikia ili ubofye. Labda utumie Facebook kwa kutumia kivinjari.