Special Thread : Kutakiana usiku mwema na asubuhi njema.

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,404
24,988
Habari wanaJF na wanaChitchat kwa ujumla wake.


Kama familia moja inapofika usiku ni kawaida kutakiana njozi njema na usingizi mwema huku tukimuomba mola atuepushe na hila zote za mwovu shetani bila kujali imani kwani sote twaamini katika MUNGU, vivyo hivyo hata tunapoamka tunatakiana asubuhi njema na baraka za siku nzima katika majukumu yetu ya kila siku.


Tutumie uwanja huu kumtakia baraka yule umpendae.
 
Ni kweli chakii kuamka asubuhi mzima sio alarm wala juhudi binafsi, ni kujaliwa na Mungu.

Binafsi, nikutakie usiku mwema na wanachama wote wa JF. Kikubwa tuendelee kuwa watu wa shukrani na kudumisha upendo huku tukiendelea kuliombea taifa letu.
 
No kweli chakii kuamka asubuhi mzima sio alarm wala juhudi binafsi, ni kujaliwa na Mungu.

Binafsi, nikutakie usiku mwema na wanachama wote wa JF. Kikubwa tuendelee kuwa watu wa shukrani na kudumisha upendo huku tukiendelea kuliombea taifa letu.
Amen mkuu Samaritan, tunapaswa kufunga na kuiombea nchi, mafundisho ya imani yanatufunza hivyo mkuu!


Nikutakie usiku mwema pia kiongozi,
 
Back
Top Bottom