PostGE2025 Special Thread: Kauli Tata za Rais Samia katika hotuba zake

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Tonny Kapola Gas Station

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2025
Posts
361
Reaction score
944

1. "Oktoba 29 tulitumia nguvu kubwa Kwa sababu ya Vurugu, mlitaka tutumie nguvu ndogo ili iwaje"

2. "Waliohamasisha maandamano Oktoba 29 ni Kwa sababu ya shida za maisha, na walifanya hivyo ili Watanzania wanunue bando wawaangalie ili walipwe"

3. "Kuna watu tunawaambia waje mezani kwenye Maridhiano Ila wao wanajifanya kutaka kutupangia kwamba Hadi tufanye kitu Fulani ndio waje, Niwaambie tu Serikali yangu haitapangiwa Wala kuamrishwa na Watu , Serikali ya wanafunzi na waalimu ndio itakayopangiwa na siyo Serikali yangu"

4. "Wapinzani walihamasisha maandamano Kwa sababu waliishiwa Pawa"

5. "Mnalalamika Vijana wenu wameuliwa, kwanini hamkuwazuia wasiende?"

6. "Vurugu za Oktoba 29 zililenga kuiangusha Dola, walishindwa"

7. "Nasikia Kuna lingine wamepanga kukifanya December 9 , Niwaambie tu na Hilo halitafanikiwa hata kidogo"

8. "Mimi ndio Rais wa Tanzania na Serikali ninayoiongoza inafanya Kazi, uwe unaitambua au huitambui Ila Ndiyo Serikali na Mimi ndiyo Rais.
 
Hiyo namba 2 ni kauli ya Rais kweli au?
 
Ameshawapa ushahidi ICC kwamba yeye ndiye kaagiza mauaji.
 
Kuhusu TEC/Dini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kwa namna moja au nyingine taasisi za dini zimejiingiza kwenye Mkumbo

Akizungumza katika Mkutano na Wazee wa Dar es Salaam, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema tunasema Tanzania haina dini lakini Watanzania wana dini za madhehebu mbalimbali, hata hivyo Kikatiba na Sheria za nchi hakuna dini na dhehebu lolote limepewa uwezo wa'kuover ride' madhehebu mengine

"Viongozi wa dini msijivishe majoho ya kwamba nyinyi ndio mnaweza 'kuover run' nchi hii, hakuna! Tutakwenda kwa kwa Katiba na Sheria ya Nchi hii. Hatutaendeshwa na madhehebu yoyote ya dini, madhehebu ya dini na wafuasi wao!" Amesema Dkt. Samia

Ameongeza, "hakuna 'over riding' hapa! Kwamba "mimi dini yangu ndio itaover ride Tanzania na tamko nikilitoa ndio hilo hilo". Hata wenyewe wanatofautiana, mimi toka nimekaa matamko 8 yametolewa na TEC, lakini ukienda chini chini wenyewe wanapingana, matamko yale hayafanyi kazi vizuri"
 
Your browser is not able to display this video.


“Tunaapa kuilinda nchi hii na mipaka yake, kulinda usalama wa raia na mali zao. Na katika hali hiyo, nguvu inayotumika inaendana na tukio lililopo.” - Rais Samia Suluhu akizungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam
 

"Haya [yaliyotokea Oktoba 29] hayakuwa maandamano, zilikuwa ni vurugu zilizoandaliwa kwa madhumuni maalumu." - Rais Samia Suluhu akizungumza na Wazee wa Dar es Salaam
 
 
Huy
Huyu mtu kwa kweli anakera sana. Yani anakupasua alafu anakusimanga kama Floyd Mayweather.

Huyu kama siyo wazalendo kumtoa basi tutalimia meno hii miaka 5.

"Wazalendo " wafanye jambo.
Mbona unajitoa na kuwapa mamlaka wengine kwani wewe sio mzalendo hauwezi kufanya jambo ?

Tulime meno tu Mimi nafurahi sana , maana tulimsema sana Mzee Magu na kumtukana kama katili mpaka kuvuka mipaka katika kumsema vibaya , Mungu sasa katuletea yule ambaye tunayemtaka na anatunyoosha kisasawa .
 
Rais Samia Suluhu amesema waratibu wa vurugu waishio nje ya nchi wengi wanasumbuliwa na ugumu wa maisha, hivyo wanatafuta namna ya kujiongezea kipato kupitia mitandao.

 


"Kama madai ya wenzetu ni katiba, hakuna aliyekataa kurekebisha katiba ya nchi hii." - Rais Samia Suluhu akizungumza na Wazee wa Dar es Salaam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…