Special thread: Kampeni za mgombea Urais wa CHADEMA/UKAWA nchi nzima kuelekea 25 Oktoba, 2015

Watanzania ni akina nani?

Mbona sisi tulio wengi chaguo letu ni Lowassa?

Au wewe na hao ambao hamumtaki Lowassa ni Watanzania wa wapi? Huku mitaa ya Tanzania jina kuu ni Lowassa, Lowassa!!!!!!!!!

Mimi, mke wangu na watoto wangu kura zetu zote ni kwa Lowassa!

Kwakweli sisi katika kikundi chetu hapa kazini kila mtu ni magufuli .hapa kazi tu
 
Hii mada ni fupi sana, akiongea kwenye mikutano inayoendelea Tabora, lowassa amesikika akisema, "Kwa mfano mkinichagua kuwa rais, nitaanza na elimu, elimu itakuwa bure na hakutakuwa na michango michango kama michango ya pen mashuleni,". Halafu ongeza na ile ya juzi ya "ccm oyee" utajua kuwa mheshimiwa ni kama anatimiza matakwa ya mbowe tu kupiga kampeni, kiukweli kuweka neno "kwa mfano mkinichagua" ni dhahiri anajua kuwa hawezi kuchaguliwa. Pia lowassa ameonyesha kukata tamaa kabisaa, hana sura ya mtu mwenye uhakika wa kile anachokipigania. Hawa mashabiki mje kwa wingi hapa kuchangia kwa matusi na kejeli.

Vikao vya harusi
 
Ninawashangaa sana hawa nyumbu wanaomtukana Dr Slaa eti hana ubavu mbele ya Lowassa mpaka kufikia hatua ya kumsahau mtu aliewajengea chama miaka yote na kuanza kummkumbatia mtu ambae hata jina la mke wake analisahau na mtu ambae hawezi kudumu dakika kumi jukwaani

Lowassa ni kam baiskeli ya miti tu ambayo inategemea mteremko kutembea, lakini ikifika kwenye mlima inabidi ipaki. Na Slaa ni bonge la pikipiki lenye horse power kubwa.

Tayari tumeishaanza kuona dalili za kuchoka kwa Lowassa, anashindwa kuhutubia majukwaani anatuambia twende kwenye website ambayo yeye mwenyewe haikumbuki.

Slaa sasa kaamua kurudi nyumbani, hapa sasa ndio mwisho wa chadema kwani hawawezi tena kupata mtu kama Slaa, kwa sababu Lowassa baada ya uchaguzi atapumzika kwani atakua kachoka mno na hataweza tena kuongea na watu.

Mungu Ibariki Tanzania

Napata taabu sana kubishana na watu wenye uelewa finyu. Itoshe tu kusema kwa kifupi kwamba: CHADEMA NI TAASISI, CCM NI TAASISI. Mtu yeyote awaye hawezi kuwa juu ya taasisi. Viongozi huingia na kutoka. CCM ina umri wa miaka zaidi ya 50 na waasisi wake karibu wote walishatangulia mbele ya haki lakini CCM ipo tena imara. Lowassa hawezi kuidhoofisha CCM kama vile ambavyo Slaa hawezi aslani kuidhoofisha Chadema.
 
nitakua nawaletea ratiba ya mgombea wa ukawa edward lowasa kila siku..

leo tar 9/9/2015
KILOSA

saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika turiani mvomero

saa 5.00 hadi saa 6.30 mchana mkutano utafanyika dumila morogoro vijijini

saa 8.00 hadi 9.30 alasiri mkutano utafanyika ngerengere morogoro

saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika morogoro mjini
 
Ana jeuri ya kuhutubia kote huko?

Huyu mtu asijetufia jukwaani huyu
 
nitakua nawaletea ratiba ya mgombea wa ukawa edward lowasa kila siku..

leo tar 9/9/2015
KILOSA

saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi mkutano utafanyika turiani mvomero

saa 5.00 hadi saa 6.30 mchana mkutano utafanyika dumila morogoro vijijini

saa 8.00 hadi 9.30 alasiri mkutano utafanyika ngerengere morogoro

saa 10.00 hadi 12.00 jioni mkutano utafanyika morogoro mjini

Samahani ndg kongwa lini hususa kibaigwa nijuze
 
Back
Top Bottom