Mimi naamini ni mpito tu huo.
Kabla ya mwaka 1994, Brasil ilishinda kombe la dunia mwaka 1970.
Kwa maana hiyo, mwaka 1974, 1978, 1982, 1986, na 1990 Brasil haikushinda kombe la dunia. Hiyo ni miaka 24.
Mwaka 1994 wakashinda, mwaka 1998 wakafika fainali lakini wakashindwa kwenye fainali, mwaka 2002 wakashinda tena.
Kwa hiyo, kwa mara tatu mfululizo Brasil walifika fainali na wakashinda mara mbili kati ya hizo tatu.
Haya mambo ya mipito ni kawaida sana.
Hata Wajerumani mara ya mwisho kushinda kombe la dunia ilikuwa 1990 na hawakushinda tena mpaka 2014. Miaka 24 hiyo.