Special message to Mama Janeth Magufuli

Special message to Mama Janeth Magufuli

MTAZAMO

Platinum Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,990
Reaction score
34,838
Habari mama,

Pole sana kwa msiba wa mumeo!, alikuwa great leader na wananchi wengi wanamkumbuka kwa utumishi wake ingawa ulikuwa mfupi kuliko kiongozi yeyote aliyetawala nchi yetu.

Hiyo Pole niliyotoa ni ya kawaida kwasisi binadamu maana wote tumefiwa wapendwa wetu lakini lengo kuu ni Pole kwa unayosikia na kuona kejeli na kubagazwa kwa marehemu mume wako hadharani bila woga tena kwa mambo mengine yasiyo msingi.

Sikia mama, mume wako alitimiza wajibu wake bila kujali pale alipokosea lakini wewe u hai ubavu wake ukisikia maneno magumu sana. Pengine unalazimika kuwatia moyo watoto lakini wewe mwenyewe umebeba mzigo mzito.

Imagine hata leo maneno yaliyotamkwa mbele yako! Tushukuru mama Samia walau kutuliza moyo wako baada ya maneno magumu leo lakini sio rahisi.

Endelea kuvumilia malimwengu, endelea kuipenda Tanzania! Jipe moyo kama Bikira Maria alivyojipa moyo alivyoshuhudia mwanae akiteswa na kufa msalabani!

Endelea kujipa moyo kama Bikira Maria alivyovumilia hata waliomtenda ubaya Yesu walipoeneza uzushi dhidi yake kuwa wanafunzi wake wamemwiba hakufufuka. Haikuwa rahisi ila moja ya tunu tunayojifunza juu ya Bikira Maria mara nyingi ni yote aliyaweka moyoni!

Kasome utenzi wa Bikira Maria Luka 1: 46-55 Ukutie nguvu. All shall be well 🙏
 
Acha uchochezi na uchongqnishi mleta mada. Hakuna aliyemnanga jiwe leo. Hayo ni mawazo yako tu.

Hebu mtaje mtu aliyemtaja jiwe kwa jina lake. Vinginevyo ni uzushi na uzandiki tu unaojaribu kuueneza.
 
Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,

Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu;

Kwa kuwa ameutazama Unyonge wa mjakazi wake. Kwa maana, tazama, tokea sasa Vizazi vyote wataniita mbarikiwa;

Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu, Na jina lake ni takatifu.

Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi Kwa hao wanaomcha.

Amefanya nguvu kwa mkono wake; Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao;

Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi; Na wanyonge amewakweza.

Wenye njaa amewashibisha mema, Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu.

Amemsaidia Israeli, mtumishi wake; Ili kukumbuka rehema zake;

Kama alivyowaambia baba zetu, Ibrahimu na uzao wake hata milele.
 
Back
Top Bottom