Speaker Makinda amfuata Tundu Lissu kumfariji kifo cha babake mzazi

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,896
IMG_1705.JPG

IMG_1741.JPG

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimfariji Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu alipofika kuhani msiba wa Marehemu baba yake Mhe. Tundu Lissu mzee Agustinio Lissu Mughwai Nyumbani kwake tegeta, Dar es Salaam. Mzee Lissu alifariki Jumapili tarehe 16 Septemba, 2012, katika Hospitali ya Muhimbili, Dar es salaam na anatarajiwa kuzikwa jumamosi Singida

tu2.JPG

Spika wa Bunge akisaini kitabu cha maombolezo

Picha kwa hisani ya Mjengwa Blog
 
Anaenda kwenye msiba na blauzi yake ya kipaimara bhe! Huwa najiuliza sana huyu Mama angekuwa Mke wa Mizengo Pinda hao wajomba zetu (watoto) sijui ingekuwaje!? Nashukuru Mola ni mawazo tu.
 
Hahaha hehehe hihihihi hohohoho huhuhuhu, JF KIBOKO hata kama una stress zitaisha tu.
 
Pole zao wafiwa. Ila utamaduni wa kuvaa khanga msibani umeisha kabisa. Kesho nitawawekea yangu nikiwa hapo msibani na skin-tite na sun goggles.
 
Anaenda kwenye msiba na blauzi yake ya kipaimara bhe! Huwa najiuliza sana huyu Mama angekuwa Mke wa Mizengo Pinda hao wajomba zetu (watoto) sijui ingekuwaje!? Nashukuru Mola ni mawazo tu.

Wenzako wanaenda kwenye msiba we unajadili Blauzi aliovaa. Ndio nyie mnaoenda Msibani na Makanisani kuonyesha Viwalo vyenu na Show off. Hiyo Blauzi kali sana na bei yake mbaya labda hujui mavazi au unaiona kwa mbali?
 
Poleni familia, chama, serikali na wazalendo wote pole Mhe. Mbunge, Wakili na Kamanda wa HAKI za Wanyonge na Msema Kweli kwa Maslahi ya Taifa; tunawaombea kipindi hiki cha kuondokewa na nguzo muhimu kwenye familia, "kwa kila jambo mtangulizeni Mungu kwanza Mfanikiwe Zaidi"
 
Wenzako wanaenda kwenye msiba we unajadili Blauzi aliovaa. Ndio nyie mnaoenda Msibani na Makanisani kuonyesha Viwalo vyenu na Show off. Hiyo Blauzi kali sana na bei yake mbaya labda hujui mavazi au unaiona kwa mbali?
Tuliza mapepo Mujusi,ungesoma mistari kwa kina ili uelewe mantiki ya ujumbe. Mimi sijadili blauzi aliyovaa kwa bei au uzuri,ila akili yako ndio imekutuma hivyo.
Mantiki ya ujumbe ilikuwa ni ziko wapi enzi za wakinamama kwenda kwenye misiba wakiwa wamejisitiri kwa Kanga Kama ilivyokuwa kwenye jamii yetu? Au tamthilia ndio zinatuharibu na kupoteza tamaduni zetu!?
 
Wenzako wanaenda kwenye msiba we unajadili Blauzi aliovaa. Ndio nyie mnaoenda Msibani na Makanisani kuonyesha Viwalo vyenu na Show off. Hiyo Blauzi kali sana na bei yake mbaya labda hujui mavazi au unaiona kwa mbali?

Kwa utamaduni tuliouzoea watanzania, wanawake uenda kuhani msiba wakiwa wamevaa Khanga. Spika Makinda alisahau vipi hilo? Si ajabu huko chini amevaa kimini, bahati mbaya picha hazionyeshi!!!!

Tiba
 
Mara ya mwisho kuhudhuria misiba ya kisasa ni lini??! msipende kuropoka na kubwata alimradi muonekane mmesema..asingeenda mngeongea mbaka povu zingewatoka..Batamzinga
 
Kiongozi, tulitaka tu asione aibu kufuta utamaduni. Niliangalia msiba wa meles wa Ethiopia, au ule wa John Mills wa Ghana na unaona kabisa nchi ina utamadauni wake, watanzania tuna Khanga, tuhifadhi utamaduni wetu. It is ours and we must embrace it.

NB: Hawa hawa wakubwa ndio kila siku bungeni wanalia na maadili ya kitanzania. Utamaduni ni sehemu mojawapo, no?

Baada ya kusema hayo, kwa mara nyingine tena naomba nitoe salamu zangu za pole kwa Lissu na wanafamilia wote kwa msiba huu mkubwa. It is sad that Mzee Augustino Lissu hatokuwepo 2015 but he went knowing kupitia yeye mungu ameanza kupigania watanzania. We have Lissu. Thank you Mzee Augustino na may the Almight God grant you an everlasting peace. Amen.
 
Pole sana Mh. Lisu kwa kumpoteza Baba hasa katika kipindi hiki kigumu na chenye changamoto nyingi Baada ya kusema hayo, kwa mara nyingine tena naomba nitoe salamu zangu za pole kwa Lissu na wanafamilia wote kwa msiba huu mkubwa. It is sad that Mzee Augustino Lissu hatokuwepo 2015 but he went knowing kupitia yeye mungu ameanza kupigania watanzania. We have Lissu. Thank you Mzee Augustino na may the Almight God grant you an everlasting peace. Amen.
 
wabongo bwana asingeenda yangesemwa
sidhani kama mavazi yana tija sana dhamiri ndicho cha busara zaidi
utamaduni sio msaafu au biblia kwamba haubadiliki
huo ni uzalendo na undugu kaonyesha kuwa sio maadui bali ni washindani wa kisiasa.
 
Ona kidogo hapa
images

Kwa utamaduni tuliouzoea watanzania, wanawake uenda kuhani msiba wakiwa wamevaa Khanga. Spika Makinda alisahau vipi hilo? Si ajabu huko chini amevaa kimini, bahati mbaya picha hazionyeshi!!!!

Tiba
 
Kiongozi, tulitaka tu asione aibu kufuta utamaduni. Niliangalia msiba wa meles wa Ethiopia, au ule wa John Mills wa Ghana na unaona kabisa nchi ina utamadauni wake, watanzania tuna Khanga, tuhifadhi utamaduni wetu. It is ours and we must embrace it.

NB: Hawa hawa wakubwa ndio kila siku bungeni wanalia na maadili ya kitanzania. Utamaduni ni sehemu mojawapo, no?

Baada ya kusema hayo, kwa mara nyingine tena naomba nitoe salamu zangu za pole kwa Lissu na wanafamilia wote kwa msiba huu mkubwa. It is sad that Mzee Augustino Lissu hatokuwepo 2015 but he went knowing kupitia yeye mungu ameanza kupigania watanzania. We have Lissu. Thank you Mzee Augustino na may the Almight God grant you an everlasting peace. Amen.

Well said mkuu ... na ndio maana utaona zinaanzishwa kamati za vazi la Taifa ... ha ha ha hahaaa. Nilidhani hata vazi litakaloitwa la kitaifa linakuja automatically badala ya kubuni kitu kipya
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Sijui Makinda akiwashwa na pilipili anakuwaje usoni

Wengi wanamwona Makinda wa leo akiwa anaelekea kustaafu, mngemwona alipokua bado kijana amechanua si huyo mnayemsema.

Nampongeza sana kwa ubinadamu alio nao kuonyesha mshikamano wa watanzania, kwani wote wako katika ajira moja ni ndugu na hivyo mmoja kuondokewa na mwanafamilia ni huzuni kwa wote. Itikadi katika nafasi hii kando, maana kule mjengoni yanaishia huko.
 
Na hivyo hivyo kwa Mh. Mizengo Pinda na Wassira enzi za ujana wao walichanua sana. Haya mkuu tumekupata "Boyfriend" wa madamu Supika,maana wewe unamjua tokea akiwa amechanua.
 
Back
Top Bottom