MNEC MLAO AMKAANGA TUNDU LISSU, ASEMA NI MPOTOSHAJI.
Alhamisi, Jan 26, 2023.
Misungwi, Mwanza.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Cde Ramadhani Mwinshehe Mlao (MNEC) amewasili Jijini Mwanza akitokea mkoani Shinyanga ambako amekuwa na muendelezo wa ziara Kanda ya ziwa kuelekea katika maadhimisho ya miaka 46 ya CCM na kupokelewa na wanachama wa chama cha mapinduzi katika ofisi za CCM mkoa wa Mwanza.
Katika ziara ameweza kufika wilayani Misungwi ambapo kupitia mkutano mkubwa wa Hadhara MNEC Mlao amempongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Kazi anayoendelea kufanya kuhakikisha watanzania wanapata maendeleo lakini pia amekemea vikali wanasiasa wanaopotoshaji na wanaosema uongo juu ya kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia ambapo amesema;
"Yupo mtu mmoja jana kafanya mkutano wa hadhara pale Dar es Salaam na waziwazi amewadanganya watanzania kuwa bei ya kilo ya Nyama na Maharage ni sawa Tanzania kitu ambacho ni uongo sote tunajua bei ya nyama kilo ni Tsh 8000-9000 huku Maharage bei ni Tsh 3500-4000 hapo tunaona utofauti mkubwa hivyo mtu huyu anapaswa kupuuzwa kwa upotoshaji huo"
Aidha MNEC Mlao ameweza kushiriki katika zoezi la upandaji miti katika Hospital mpya ya wilaya ya Misungwi sambamba na kupandisha Bendera katika Shina namba tano kata ya Misungwi na kuzungumza na mwenyekiti wa shina Ndgu Juma Malangu ambapo amemshukuru sana MNEC Mlao kwa kuthamini na kutambua kazi kubwa ya chama inayofanywa kwenye mashina ya CCM.
Pia MNEC Mlao amesisitiza wanachama wa chama cha mapinduzi kuelekea maadhimisho ya miaka 46 ya CCM kuendelea kukijenga chama katika maeneo yao yote na kuwajuza kuwa uimara wa CCM utatokana na namna ambavyo tutaendelea kufanyakazi za chama kwa kujitolea vyema kuhakikisha idadi ya wanachama inazidi kukuwa sambamba nakufuatilia vyema utekelezaji wa ilani.
#MimiNiNyinyi
Imetolewa na:
JOSHUA KANDUMILA.
KATIBU WA UVCCM MKOA WA MWANZA.