South Sudan independence photos

Sizani huko Southern Sudan kama kuna mtu mweupe! Yaani hawa jamaa ni weusi Tii!
 
0710_cartoon.jpg

0711_cartoon.jpg
nawapenda sana makatunist. ni wanafalsafa
 
South Sudan imesaidiwa saana na UGANDA,Ethiopia,Kenya, Tanzania,Eritrea, na mataifa mengi mno ya Ulaya,Sidhani kama hizi nchi zimeshawahi wabania, Kwa taarifa yako Mtoto wa kwanza wa Garang,ambaye sasa ni mwanajeshi ndani ya SPLAA, amesoma Tanzania, Uganda imewasaidia saana hawa jamaa si kwa silaha, mafunzo, Mpaka leo kaskazini mwa uganda kuna kambi kadhaa za mafunzo za SPLAA. Garang kwa safari zake za nje alikuwa anatumia ndege binafsi ya M7. Operation base ya Garang ilikuwa Ethiopia, nakumbuka kuna kipindi SPLAA walizidiwa nguvu baadaya ya Libya kumpa bashiri ndege za kivita pamoja na silaha ndogondogo, ilibidi Eritrea wapeleke wanajeshi Kusini mwa Sudan waende wakaokoe jahazi

Kumbuka sio Israel pekee hata marekani,Norway, UK; Canada na mataifa mengine walitoa msaada mkubwa saana kwa SPLAA, nakumbuka kipindi vita ilikuwa inaendelea Kulikuwa na NGO moja tu kutoka Norway ilikuwa inatoa misaada South Sudan.
Kutokana na kuonewa kwa miaka mingi, wingi wa maliasili walizonazo Nchi nyingi zilikuwa zinasaidia kwa kila namana isipokuwa china tu, cha kushangaza niliwaona jana wanatangaza wanafungua ubalozi JUBA wiki hii

Mkuu hapo kwenye red umechemsha:

1. mtoto mmoja wa kiongozi wa zamani wa SPLA kusoma tanzania ndo msaada wa ukombozi? hata kama alisoma bure? tanzania kimataifa inafungamana na siasa za nchi za kiarabu mfano kufunga ubalozi wa israel, hivyo haiwezekani eti isaidie vita dhidi ya serkali ya kiislam ya khartoum

2. Nchi za canada, ulaya na marekani zinalinda maslahi yao ya mafuta kwa kujipendekeza kwa nchi za kiarabu, kuisaidia SPLA ingeichukiza Khartoum na OIC kwa ujumla na kuhatarisha maslahi yao kwenye nchi za kiarabu. Ndo maana hata leo hakuna msimamo wowote wa maana dhidi ya Bashir na uhuni wake huko Darfur. Kumbuka raia wa S/sudan ambao baadhi yenu mnawatukana kwenye hii thread kwa ajili ya weusi wao, waliuwawa kwa mamillioni na waarabu, lakini hakuna hata nchi moja ya ulaya wala marekani wala canada au Asia au Australia iliyolaani au kutaja mauaji hayo. Dunia nzima ilikaa kimya, leo wewe unadhubutu kusema eti nchi nyingi ziliwasaidia?????? Fikiria mwenyewe reaction ya dunia kama mtoto mmoja wa palestina akiuwawa na waisrael hata kama aliuwawa kwenye harakati za kurusha mawe/mabomu. Dunia nzima itasimama na kulaani, hilo halikutokea south sudan licha ya mamillion ya watu kuuwawa kikatili, sababu ni nguvu ya mafuta ya waarabu na kete yao ya uislam.
 
Mkuu hapo kwenye red umechemsha:

1. mtoto mmoja wa kiongozi wa zamani wa SPLA kusoma tanzania ndo msaada wa ukombozi? hata kama alisoma bure? tanzania kimataifa inafungamana na siasa za nchi za kiarabu mfano kufunga ubalozi wa israel, hivyo haiwezekani eti isaidie vita dhidi ya serkali ya kiislam ya khartoum

kufunga ubalozi Israel hakuhusiani hata kidogo na vita ya ukombozi iliyokuwa inapiganwa kusini mwa Sudan, yes kulikuwa na msuguano kati ya serekali ya nyerere na israel kuhusu swala la wapalestina, kwa sasa tuna uhusiano wa kibalozi na balozi wa tanzania cairo anahudumia mpaka jerusalem, kama ubalozi wa israel nairobi unavyohudum mpaka dsm

ipo missaada mingi iliyotolewa na watanganyika kwa SPLAA, NA Si lazima kuiandika hapa, na kwa taarifa yako rais wako ndio anapigia debe south sudan iwe member wa jumuiya ya africa mashariki mapema
 
Darfur iko sudan kusini dada, halafu nimekupenda ghafla dada tunaweza kuwasiliana?

Yutong...angalia usije ukapenda jini... Kwani unamuona au umetamanishwa na avatar yake........ Mungu akusaidie uendelee kupenda penda ghafla....
 
Tusubiri, mimi sina matumaini yoyote ya maana. sana sana hapa kinachosubiriwa ni kugawana vyeo. Watatwangana sasa hivi, tusubiri. Kuna faction ambayo inasema kama hakuna democracy, hawatakubali.
Uhuru wao ni kama wa nchi nyingine za kiafrika, kuhamisha mirija kutoka kwa wazungu kuweka kwa waafrika, kama tunavyoona mafisadi, rushwa etc at the detriment of the masses.
 
Back
Top Bottom