Asante kwa kunifafanulia kwa undani jambo hili....ki ukweli naweza kukiri kuwa ni uvivu wa kufuatilia lakini nimefurahi sana hawa jamaa kupata uhuru......nimekuwa nikikutana nao wengi wao Kenya na kuwahurumia jinsi ambavyo unaweza kufeel kuwa mkimbizi katika nchi yako.......sasa kingine.....mbona Kenya imekuwa mstari wa mbele sana katika ukombozi wao....nikinyanyua ramani yangu naona Kenya ndio imepakana nao kwa kiasi kidogo sana ukilinganisha na Uganda, DRC, CAR na hata Ethiopia....nini Kenya inataka hapa......
Ni kweli Kenya walijitoa Muhanga kuhakikisha hawa jamaa wanapata uhuru, Zipo sababu nyingi saana, Ya kwanza ni BIASHARA, kenya iliamini South Sudan Huru watanufaika nayo saana kibishara, Hili halina ubishi, baada ya kutiliani saini makubaliano ya amani haikuchukua miezi wakenya walianza kumiminika South Sudan kwa wing Mwishoni mwa mwaka 2009 kulikuwa na Wakenya zaidi ya elfu kuninatisa wanafanya kazi kwenye mashirika ya kutoa misaada, makampuni binafsi, na wengi walianzisha biashara zao nyingi tuLingine makampuni mengi ya kesnya yalikimbilia Kusini mwa sudan na kufungua maofisi yao, mfano mzuri ni Kenya Commercial Bank KQ na mengineyo
Kingine Kenya wanataka wawe ndio wanasafirisha mafuta yote ya kusini mwa sudan, ili kufanikisha hili wameshaanza/wako mbioni kujenga bandari Mpya ya LAMU pamoja na reli itakayofika JUBA na Ethiopia, Hili nadhani raisi Kibaki tayari ameshalibariki na watakuwa kwenye maandalizi ya mwisho. kuna uwezekano mkubwa Likajengwa BOmba la Mafuta kutoka South Sudan mpaka bandari mpya la Lamu
Kumbuka kwamba Geography ya kenya pia imesaidia wao kunufaika tangu huu mgogoro unaanza mpaka unakwisha, mashirika mengi yanayotoa misaada kusini mwa Sudan makao yao makuu yapo Nairobi, wanatumia saana viwanja vyao vya ndeke kusafirisha misaada pamoja na mahitaji mengine. Silaha pia zote zinazotumiwa na Jeshi la SPLAA zinanunuliwa/ zilikuwa zinanunuliwa na Wakenya, kama utakumbuka kuna Meli iliyokuwa imebeba silaha ilitekwa na maharamia wa kisomali, Wakenya wakasema silaha ni za jeshi lao kumbe ilikuwa danganya toto. Pia viongozi karibu wote wa ngazi za juu wa SPLAA na familia zao walikuwa wanaishi Nairobi. Garang yeye alikuwa na makazi Ethiopia ila mara nyingi hata Nairobi, na Kampala alikuwa anafika kila mara kwa ajili ya logistic
Hawa jamaa walikuwa washirika wakubwa saana wa UGANDA na mara nyingi JOHN Garang alikuwa na makazi kampala lakini baada ya Garang kufa kwa ajali hawana imani kabisa na Mseveni wanahisi/hata mke wa Garang alishasema hawa jamaa ndio waliomuuwa Garang, Hata jana sikumuona M7 labda alikuja baadae
Hope kwa haya maelezo utapata mwanga kidogo