South Africa kuna msiba au sherehe?!

South Africa kuna msiba au sherehe?!

Mandela has done enough for his people. Let him rest in peace
Mandela alifanya mengi hapa duniani.
Lakini lazima tujue kuna maisha baada ya kufa, miaka ya kuishi ni ujaliwa miaka 100, kuna moto wa milele na pepo ya milele, yote haya unayaandaa ukiwa hai, kila mtu atakufa hata wewe lakini umejaandaaje kwa ajili ya maisha baada ya kufa, .Wokovu sio dini ni kumkiri Yesu Kristo kwa kinywa kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako na kuamini kwa moyo wako wote.
Pepo unaitafuta ukiwa hai, haiko hapa duniani lakini unatafutwa duniani unaipata mbinguni.
Wokovu ni kujitoa, kuna mambo yatakugarimu ili upate nguvu ya kushinda dhambi.
Dunia ukiipenda huwezi kumpenda Mungu, mpe Yesu maisha yako sasa .a
 
Huenda ni utamaduni wao.... Kuna kabila fulani sitopenda kulitaja, misiba yao huwa ni sherehe... watu hula, hunywa na hata kucheza muziki juu ya kaburi baada ya mazishi!!!

Hamna sherehe hapo bali ni kujifariji tu.Kwa maneno mengine,wanajaribu kugeuza msiba kuwa sherehe ili kujifariji ila ukweli ni kuwa hio sio sahihi hata kidogo.
 
Hata mimi nasherekea sababu mandela kaihuisha ndoto yake ya free south africa. Na yeye akaweza kuwa presidaa na kuwaunganisha watu wake. Kaweza kuishi miaka 95 zaidi ya kawaida. Kinachofuata ni kumshukuru mungu na kusherekea mafanikio yake, wnafamily watalia lkn sie wa mbali tunasherekea maisha yake. HAkusubiri south africa imtunze, yeye kaitunzia amani south africa

Hivi unamuona Bi.Grace Machel, mke wa marehemu alivyojawa na huzuni?Ukweli ni kuwa akiwa ndugu yako wa karibu huwezi kugeuza msibs kuwa sherehe.Yule mama ukimuangalia kwenye TV anaonekana kabisa analia.Huyu ndio yuko msibani.

Msiba huu kwa wengine ni nafasi ya kujipatia umaarufu na kutaka kuandika historia tu.
 
Jamani huo ni utamaduni wao. Kwa hapa Tanzania Wanyakyusa wanacheza ngoma na kucheza nyimbo za kienyeji baada ya mazishi. Na pia wanakunywa pombe sana. Na hii inafanywa kwa siku nyingi kutegemeana na umaarufu wa marehemu. Na wakati wa kuomboleza ng'ombe wengi (kutegemeana na umaarufu wa marehemu) wanachinjwa. Lkn siku hizi haifanywi tena kwa sababu serkali imelazimisha kuwa kuomboleza kusizidi siku tano baada ya mazishi. Ni heshima kubwa sana marehemu kufunikwa na blanketi kaburini. Mzee akipewa zawadi ya blanketi hufurahi sana na kusema kushukuru kwa kusema "ahsante kwa kunizika! Inatosha sana hata kama hutakuja kuhudhuria msiba wangu". Nimeshangaa sana kusikia kuwa Mandela naye atafunikwa kaburini na blanketi badala ya bendera South Afriica.

Nasikia Wajaluo nao hucheza muziki wakati wa msiba.

Hiyo sentensi ya mwisho sijasema mie!!!
 
Hiyo ni suala la utamaduni hata hapa tanzania nimeona kuna kabila la wabarabaig huwa na utamadunia wa kushekea mtua akifariki kama mtu huyu amefanya mambo mazuri na ameishi muda mrefu. Huwa wanatabia ya kufanya sherehe inayoitwa bungeda unakuta watu wakichez na kunywa pale kaburini kushekea mambo yake mazuri aliyofanya. Nadhani ni suala la utamaduni wa jamii japo sijui utamadu wa SA nachojua kushekea ni jambo la kawaida kwa utamaduni wa jamii nyingine kwa mtu aliyefanya mambo mengi na mazuri nakuishi muda mrefu.
 
Sababu kashatumikia taifa mpaka mwisho wacha wafurahie,
 
Pamoja na kwamba kuna makabila hufanya sherehe na kucheza juu ya kaburi lakini yote hutegemea msibs umekugusa vipi. Mi nimefanikiwa kufika kwenye hiyo misiba ya kusherekea lakini wapo ambao unakuta wana huzuni kubwa sana na hawana muda wa kucheza.
kama ni mhuzuliaji wa misiba utagundua kwamba wale ndugu wa kalibu kabisa nfano Baba kafariki Mke na watoto ndo huwa wana huzuni, wengine ni furaha tu.
 
Sababu kashatumikia taifa mpaka mwisho wacha wafurahie,

Mkuu wanao furahia si ndugu wa karibu bali ni wananchi. Ni vigumu ummempoteza mtoto wako/ mpenzi wako/mama/baba halafu uwe na muda wa kucheza. Cheki mjane wa Mandela alivyo na huzuni
 
mimi nimeipenda sana hii style yao aisee , ni kujiachia tu kwa kwenda mbele ! nakuusia mleta uzi siku ukisikia wamening'oa kichwa changu au labda nimepigwa panga na wale " MAJAMBAZI WA KIWALANI " basi msilie wala nini , style ni hiyohiyo tu , sherehekeeni maisha yangu ya hapa jf .
 
Sasa jamani mtu ana miaka 95 mlitaka akae mpaka miaka mingapi?sis kwetu akifarik mzee wala hatulii maana kaish miaka mingi,lakin kijana akifariki lazima mhuzunike zaidi
 
Back
Top Bottom