"Mtu" huyo huyo nido aliyemshauri vibaya Raisi wetu kuwa kuanzia Septemba mwaka huu wahamishe wizara zote na ziwe zimehamia Dododma. Na Raisi wetu aliapiza asiye hamia Dodoma kabla yake hata pata mshahara. Lakini cha kushangaza hakuna hata wizara yeyote iliohamia Dodoma na hakuna waziri yeyote aliekatwa mshahara. Sijui hawa mawaziri wanamwekea mgomo Raisi wetu!
Raisi alikuja na agenda nzuri ya kusafisha jiji mwishoni mwa wiki, lazima "mtu" huyo kamshawishi Raisi wetu kuachana na kusafisha mji, mji wetu bado umetta na taka taka.
Raisi alikuja na ajenda nzuri ya kuboresha mahospitali Tanzania, lakini "mtu" huyu kamshawishi tena Raisi wetu kuachana na hospitali. Eti Muhimbili imeshapata "mahitaji" yote na tuachane na Hospitali ya Temeke, Mwananyamala na hospitali nyingine zote Tanzania.
Huyu mtu anae mfidi raise wetu nashauri ni jipu na atumbuliwe.