msnajo
JF-Expert Member
- Jan 20, 2011
- 3,066
- 1,142
Leo ndugu Mafuru amekanusha kauli ya Magufuli kuhusu kuwepo watumishi waliokuwa
wanalipwa milioni 40 ya mshahara..infact amesema hakuna hata aliewahi kuzidi milioni 25
Juzi tu Gavana kamkosoa Magufuli kuhusu fixed deposit
mifano ipo miingi
Kwa vyovyote 'kuna mtu ambae anam feed ' Rais taarifa hizi ambazo
'zina utata na ukakakasi'
na matokeo yake Rais anaongea mbele ya hadhara vitu vinakuja kukosolewa
na wasaidizi wake....
Ushauri wangu huyu 'mtu' Magufuli amtimue haraka sana.....
hafai kukaa karibu na Rais......atampotosha makubwa zaidi kama sio tayari kashampotosha..
Hashim Rungwe, alisema nchi inaongozwa na tabia na sio sheria! Kauli hii ukiitafakari utaelewa jambo. Mbaya zaidi watendaji waliopewa dhamana nao wameacha sheria wanatawala kwa kuangalia tabia za mkubwa wao. This is too bad! Watumishi wanaitwa vichaa majukwaani, hakuna chama wala taasisi ya kukemea. Mkuu The boss, haya unayoyaona yanadhihirisha giza totoro huko tunakoenda!