...hata JK amempigia kampeni kiaina
"Kiaina" vipi wakati ile ilikuwa kampeni ya nje nje, kwenye mkutano wa wazi wa UWT?
Kulikuwa kuna wagombea watatu, mmoja amelenga kampeni yake kwenye ghanima aliyonayo dhidi ya mpinzani wake mkubwa kwamba yeye ana elimu, mwenzake hajasoma vizuri. Kikwete akaja kwenye mkutano wa UWT punde kabla ya kura akatangaza "chagueni msomi." Kungekuwa hakukuwa na swala la usomi katika kampeni hii, na Kikwete angesema toka awali kwamba CCM ikuze viongozi wasomi hapo tungekuwa wazushi tukisema Kikwete anamlenga mtu yeyote. Hapa Kikwete ni wazi alimpigia debe Mama Simba.
Sasa Kikwete huyu huyu mwezi jana katoka kuwakaripia wazee waliojiingiza kwenye kampeni za vijana. Kina Makamba, Kawawa, Kingunge kumbe hawakutumwa na CCM kuingilia uchaguzi wa vijana, maana Kikwete alikerwa na walichofanya, akasema:
"It's a crime (ni uhalifu), ni mbaya sana kujiingiza katika masuala ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wakati we si kijana wala mwanachama, hii ni mbaya. Ni lazima kujiuliza huyu Kikwete yuko nje ya uanachama, lakini anaweka mtu wake kwenye nafasi ya uongozi na anataka ashinde, anataka nini huyu?"
Baada ya hapo Kikwete anakuja kwenye uchaguzi wa UWT, anasema chagueni msomi, wakati tunamfahamu anaejiita msomi, aliye run campaign platform ya usomi, ni mmoja tu. Hiyo sio kampeni ya wazi hapo? Sio vizuri kuita watu majina, hususan kwa waheshimiwa kama Rais wetu, lakini jama, huu aliofanya Rais tuuiteje, sio unafiki huu? Sio unafiki?
Jakaya anampenda Sophia. Akashindwa kujizuia kwenda nusu nusu katika kum-sapoti maana dhambi nyingine bana ukishaianza ni heri tu uimalizie. Ukiamua kula nguruwe kula aliyenona. Tatizo ni kwamba nguruwe mwenyewe hajanona. Sophia Simba hana caliber ya uongozi ya kustahili Rais kutoa muhanga maadili yake kumpigia debe bila kujificha. She is simply not worth the candle.
Unam-kampeinia mtu anaesema kwamba wanawake wawezeshwe katika katika kazi zisizo za maofisini. Kwamba katika enzi hizi za mapinduzi ya teknolojia wanaume wamepoteza kazi za maofisini na ni wanawake ndio wanaweza kujiajiri. Yani, badala ya kusema wanawake inabidi wawezeshwe kushiriki katika uchumi na ajira mpya za mapinduzi ya technolojia anasema kazi za maofisini ni za wanaume! Sasa kazi za wanawake za kujiajiri ambazo sio za ofisini anazoziongelea Waziri wa Nchi ni zipi kama sio kufuma mikeka, kuhudumu kwenye majumba Oysterbay, kuuza la mnazi, kuhudumia order na mahitaji mengine ya walevi katika joints za nyama choma?
Kikwete anamu-endorse mtu anaefikiri hivyo. Kamteua ubunge, akampa wizara nyeti, kubwa kuliko. Anasimamia Usalama wa Taifa, na TAKUKURU. Wahisani wote wanaikodolea macho wizara ya utawala bora maana "good governance" ndio buzz words wanazotuimbia pay masters wetu kila kukicha. Wananchi wanaikodolea hii wizara macho tukitegemea itulindie amani, usalama na utulivu. Naombea isiwe huyu mama ndio anatoa uongozi katika mambo yote tata tata, na delicate delicate ya usalama wa nchi. Uhusiano wetu na nchi jirani ambako wakimbizi na majambazi huingilia kuua raia wa TZ, maamuzi ya kushitaki au kutoshitaki the Mkapas and the Wariobas of the world, na CCM financiers na deal cutters kama Rostam na Chenge, na maamuzi ya juzi kutuma ma spy Arusha ku-interview terror suspects kwenye misikiti, ku arrest secessionists wa Zanzibar kuhusiana na tensions za Bara na Zanzibar, maamuzi juu ya swala la mahakama ya Kadhi Mkuu. Very, very delicate issues chini ya huyu Mama Simba. Mtu anaefikiri kwamba wanawake kazi wanazoweza ni za mama ntilie.
Ndio visions za Jakaya na Sophia. Couple ya ajabu hii.