Sophia simba hana hadhi ya kuwa waziri, JK kachemsha saaana!!! Nitachambua hili... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sophia simba hana hadhi ya kuwa waziri, JK kachemsha saaana!!! Nitachambua hili...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eliesikia, Nov 18, 2010.

 1. eliesikia

  eliesikia JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2010
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 423
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  WAZIRI wa zamani Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Mnyambi Simba, huko nyuma amewahi pia kutoa kauli zenye ukakasi akimshambulia mfanyabiashara (Mengi kuwa sio mwanaCCM )na mmoja wa wafadhili wa chama tawala kilichomweka waziri huyo madarakani.

  Ni huyu huyu Sophia ambaye chama chake kimekanusha matamshi aliyotatoa mbele ya kadamnasi kuwashambulia wabunge wa kuchaguliwa walio mume na mke – John Malecela na Anne Kilango Malecela.

  Ni huyu Sophia mwenye dhamana ndani ya wizara nyeti ya Utawala Bora, yenye wajibu wa kusimamia mienendo ya watumishi wa umma, iliyo chini ya Ofisi ya Rais.

  Ni Sophia ndiye anayewajibika katika kusimamia na kutekeleza kiapo chake cha utii na kumshauri vema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika masuala mbalimbali yenye maslahi kwa taifa, bila migogoro yoyote.

  Ni huyu Sophia, ambaye ndani ya chama chake, amekabidhiwa dhamana ya uenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) - wanaokiamini, kukipenda na kukitumikia chama tawala, yaani CCM.

  Ni huyu Sophia aliyedaiwa kumwangushia kipigo, aliyekuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Janeth Kahama, wakati wa mchakato na kampeni za kumtafuta mwenyekiti wa wanawake hao kwa njia ya kura.

  Ni Sophia huyu huyu, aliyewahi kukaririwa na vyombo vya habari akiwatetea wafanyabiashara wakubwa wanaotuhumiwa kwa ufisadi na kuzua gumzo na kuharibu upepo wa nchi wakati huo.

  Sophia Simba, kwangu ni mwanamama anayekurupuka. Ni Waziri asiyejipa muda wa kutafakari na kueleza anachokifahamu. Wakati mwingine nahisi anatumika ama kwa nia ovu au kwa maslahi ya taifa ili kuharibu mwelekeo ama kuwasahaulisha walalahoi kero zinazowakabili.

  Ni Sophia, aliyejaribu kucheza ngoma tofauti ya vita dhidi ya ufisadi iliyoanzishwa na viongozi wa vyama vya upinzani kabla ya kupokelewa kwa shangwe wa wakuu wa chama chake, akiwemo rais aliyemteua kushika nafasi ya uwaziri.

  Ni Sophia aliyewashangaza wasomi na wasio wasomi, pale alipojiinua na kuishambulia familia ya wanasiasa, akiwemo mkongwe, Mzee Malecela.

  Ni huyu Waziri Sophia aliyewaacha vinywa wazi wachambuzi, wajuzi na wananchi wa kawaida pale alipowashambulia kwa tuhuma mbalimbali wanasiasa wenzake.

  Ni wapi alipokuwa Sophia kiasi cha kuzikalia tuhuma nzito za wanasiasa hao na kujinasibu kwamba ndani ya chama chao cha CCM hakuna msafi, wote ni mafisadi?

  Ni imani yangu kwamba Sophia anahitaji kubanwa ili aanike tuhuma zote anazozifahamu, pengine atalisaidia taifa na kulirejesha kwenye mstari ili walalahoi waone raha na faida ya kuzaliwa juu ya ardhi ya Tanzania.

  Pamoja na yote, nina ushauri kwa mkuu wake wa kazi. Kwanza amfukuze kwa sababu amejidhihirisha kwamba hafai kuwa kiongozi wa wanyonge kwa sababu ameshindwa kusimamia mienendo ya watumishi wa umma.

  Sophia aanze kufuatiliwa, ahojiwe na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Polisi na Usalama wa Taifa.

  Ni huyu sophia Simba aliyesema (akiwambia UWT members) kuwa kama Mumeo hapendi CCM basi usimpe unyumba.. Anaonyesha wazi kuwa Ngono kwake yeye ni jambo muhimu zaidi kuliko kuendelea na misimamo sawia ya kinchi na utaifa.:A S cry:

  Ni Imani yangu kwamba kuondolewa kwa waziri huyu katika nafasi aliyonayo, kutabadili fikira zangu kwamba analipwa fadhila za mema machache aliyoyatenda wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2005(kumpitisha JK pale CCM).

  nawasilisha
  Source: freemedia:israel:
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,599
  Trophy Points: 280
  Nitashangaa sana sana jk akimrudisha huyu kilaza mwenzao uwaziri...nitashanga sanaa.....uwaziri sio size yake huyu labda secretary wa makamba pale lumumba.
   
 3. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2010
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,789
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  mkuu badala yake apewe nani anayefaa?
   
 4. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,058
  Likes Received: 4,628
  Trophy Points: 280
  huyu hawezi waza zaidi ya ngono, worst ever minister i saw inTZ history, mmmhh chaguo la JK..!!!!!! na hii yote ndio mjue WHOOOOOOOOOOOO ISSSSSSSSSS JJJJJJJJKKKKKKKKKK
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Nov 18, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Vick Kamata
   
 6. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #6
  Nov 18, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  lakini kwa uwezo wa kufikiri wa raisi huyu wa ccm hakuna la kushangaa tegemea uozo
   
 7. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #7
  Nov 18, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Pr Maji Marefu!!!:smile-big:
   
 8. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #8
  Nov 18, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Kwa CCM huyu Sophia Simba ndiye anafaa kuwa Rais. Hukumsikia JK anakwambia Makinda kafungua mlango na sasa kinamama wanaweza kutwaa nafasi ya juu kabisa.

  Kwani Sophia Simba ana tofauti gani na JK? Angalau Sophia Simba anaonekana ni imara kuliko JK.

  What matters doesn't matter in CCM!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 9. T

  Technology JF-Expert Member

  #9
  Nov 18, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  Jamani leteni mada za maana badala ya kuwashambulia watu mmoja mmoja, hii ni forum makini na sio chama cha mashoga au wasagaji
   
 10. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #10
  Nov 18, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Kwanini wewe usilete hizo unazoziona za maana. Unasubiri uletewe...mbona hiyo ndiyo tabia ya mashoga na wasagaji!!!!!!!!
   
 11. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #11
  Nov 18, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  mmmmmmmmmmmmmmmmm!
   
 12. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #12
  Nov 19, 2010
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 593
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60

  mimi nitashangaaa akimnyima uwaziri, JK neve stop to amaze me, kile ambacho waungwana wanatarajia hatafanya yeye ndio anakifanya.
   
 13. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #13
  Nov 19, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Apewe Injinia Manyanya!
   
 14. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #14
  Nov 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Si mwenzetu. Si mwana mtandao na kibaya zaidi kajitambulisha kama mpinzani wa ufisadi CCM. Hatufai!
   
 15. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #15
  Nov 19, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0

  chezea Mwanakijiji.
   
 16. M

  Mabuya Member

  #16
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 19, 2008
  Messages: 25
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 3
  umenikuna lakini umewasahau Dk Shukuru Kawambwa & Hawa Ghasia sijaona walichofanya TRL,ATCL,bandari hakuna kitu kero kero kero na utumishi wa uma ndo yale yale mauozo hata Mhe Jenista Mhagama alisha sema .wakitemwa ntafanya sherehe ntawambia venue
   
 17. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #17
  Nov 19, 2010
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  wewe kilaza pr ndo nini??????
   
 18. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #18
  Nov 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wewe ndiye kilaza kama hujui PR nini!
   
 19. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #19
  Nov 19, 2010
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,802
  Likes Received: 2,748
  Trophy Points: 280
  Kwa JK hakuna lisilowezekana, Megji -mmoja wa mafisadi wa EPA-kesharudi mjengoni! Na bado kina masha, buriani, worse still EL anaweza kupewa wizara!
   
Loading...