Sophia Simba hajui kiingereza?

Sophia Simba hajui kiingereza?

ANYWAY ATUDHIHIRISHIE LEO ONGEE NA WAANDISHI WA HABARI KIDHUNGU KWANINI HAKUJIELEZA NA KUOMBA KURA KAMA WENZAKE
NA KAMA BABA ALISEMA AENDE TU ASEME...
HATA HIVYO KABLA ALIKUWA ANALALAMA KUNA MTU KULE BUNGENI ALIMWAMBIA KUWA YEYE HAKUTAKIWA KUTUMA TENA FORM KWANI HAKUKUWA NA HIYO NAFASI YA KINA MAMA...
ANA AKASEMA NA NUKUU "kama kuna kitu hawa watu wanaangalia sana ni swala la gender kwa hiyo huyo aliyesema hivyo kakosea"
Ninachoona hapa kuna kina mama wengi walitaka kupeleka maombi ila kuna mtu aliwaambia kuwa hawatakiwi kwani nafasi ya wanawake ni 1 tu na niya mwenyekiti wa kina mama sooooooo waliwadanganya ili Sophia asipata upinzani?? sijui?? BABA nae....
 
Acheni kueneza uwongo jamani, yaani Sophia Simba kama hajui kiingereza kabisa angeweza vipi kufanya seminars, presentations na madudu kibao ya LLB pale mlimani kuanzia 1987 mpaka 1991?

Hata kama kuna kubebwa lakini asingelijua Kiingereza ingelikuwa ngumu sana kumbeba kwenye masomo yote. Lazima tuelewe LLB sio mahesabu na bila lugha kabisa huwezi kufanya la maana.

Huyo mama is not among the brightest but also she is not dull as some of you guys want us to believe.

Mkulima, hujawahi kusikia digrii za chupi wewe? isije kuwa labda alitumia kamtindo hako na ndio maana mimi sina wasi wasi , kama digrii za namna hiyo zipo sidhani kama atashindwa kutuwakilisha huko, anaweza bwana... yaani WHY ashindwe kama uzoefu wote anao wa miaka nenda rudi!!:smile-big:
 
hii issue kwamba hajui kiingereza does not ring a bell-what i think labda ni fluency ya kuflow,in her case maybe fullstops na but,but zinakuwa nyingi-hili ni tatizo la watanzania karibuni wote.Lazima tukumbuke speaking in public ni onother level na tunao academics wengi when it comes to this nerves take over.Ni wachache sana TZ who have been able to overcome this,notable one Che mkapa.
 
China, Urusi, Japan wanatumia Kingereza au lugha zao kuendesha serikali?

wewee china, urusi japan wao wnajitosheleza sawa acha mawazo mgando, ili watz tuwe front no way lazma ujue kiingereza, hizi computer utatumiaje? au tz tunao uwezo wa kutengeneza comuter siku hizi?
 
Mkulima, hujawahi kusikia digrii za chupi wewe? isije kuwa labda alitumia kamtindo hako na ndio maana mimi sina wasi wasi , kama digrii za namna hiyo zipo sidhani kama atashindwa kutuwakilisha huko, anaweza bwana... yaani WHY ashindwe kama uzoefu wote anao wa miaka nenda rudi!!:smile-big:

Wewe Kiraka wacha utani!

Unataka wabunge wetu waende kutoa huduma kule SADC?

Nafahamu madai ya digrii za chupi, in fact tulikuwa tunaita marks za chupi na sio digrii cha chupi.

Lakini nikuambie ukweli, waliokuwa wanapata marks za chupi hawakuwa wajinga kiasi cha kutokujua kiingereza kabisa. Pale walipokuwa wanakutana na miiba ndio walikuwa wanatumia vipaji vyao. Binafsi nilikuwa nasikia lakini sikuwahi kumwona msichana mjinga anapita tu eti kwasababu ya marks cha chupi.

Wakati mwingine wanaume wa Afrika tuna matatizo makubwa na dada zetu. Tunawasingizia kila baya na wakituzidi jambo tunakimbilia kusema wamependelewa.

Kwa LLB ya UDSM niliyokuwa naijua mimi miaka hiyo, kama mama Simba hajui kiingereza kabisa asingeliweza kupita. Hata marks za chupi zisingelitosha maana kuna walimu wengine wasingeruhusu hata binti afungue vifungo vyake.

Niliwahi kushuhudia akina dada wa LLB wakilia pale UDSM kwasababu wame disco mwaka wa tatu. Yaani LLB, Engineering na B.Com zilikuwa zinaongoza kwa balaa. Sasa huyo mama mjinga asiyejua kiingereza kabisa kama alipita tena bila hata kurudia mwaka, kweli nitashangaa sana.

Anaweza asiwe fluent kwenye Kiingereza ukilinganisha na wanafunzi wengine wa LLB miaka hiyo lakini kusema hajui kiingereza kabisa nafikiri ni uwongo au kijembe cha wapinzani wake tu.
 
huyu mama kwa level ya watanzania ana elimu ya kutosha kabisa labda tuzungumzie matatizo yake mengine. na kwa miaka ile elimu iliyokuwa inatolewa si kama ya sasa

school course/degree/award start date end date level

University of Dar es Salaam LLB 1989 1992 GRADUATE
Ilonga Middle School middle Education 1961 1964 PRIMARY
Kibosho Secondary School O-Level Education 1968 1969 SECONDARY
MekanForbidant College-Sweden Information Studies 1982 1982 CERTIFICATE
University of Dar es Salaam Certificate in Law 1982 1987 CERTIFICATE
University of Zimbambwe Postgraduate Diploma in Women's Law1996 1996 POSTGRADUATE
New Hemphshire University Master of Science on Economic Development MASTERS DEGREE
NBC Secretarial College Pitman's secretarial Certificate CERTIFICATE

source: BUNGE website
 
Wadau msimlaumu spika au naibu wake kwa kumwondoa sophia kujieleza wakati wa kuomba kura za sadc huyu mama hajui kiingereza kabisa kwa hiyo chama kimelinda aibu""funika kombe mwanaharamu apite""

sababu ya kutojieleza ni kuwa katika kundi lake (wanawake) hakuwa na upinzani
 
Labda ungefafanua zaidi nini maana ya Sophia hajui kiingereza kabisa?

Huyu mama amesoma bachelor of law (LLB) pale mlimani miaka ya 80. Sasa kama hajui kiingereza kabisa angewezaje kumaliza masomo hayo?

Naelewa huyo mama aliingia mlimani kama mature student na alikuwa ana struggle na shule lakini kama alimaliza kwa vyovyote hawezi kushindwa kiingereza cha kujieleza. Kumbuka miaka hiyo faculty ya sheria ilikuwa inachukua wanafunzi wacahcahe wenye uwezo (kama 60 kwa mwaka) na mwanafunzi akichemsha tu, ilikuwa inakuwa ngumu sana kumaliza.

Anaweza asiwe na kiingereza kizuri sana lakini sio cha kushindwa kabisa kujieleza.

Kwa kuongezea tu huyu Mama kasoma post graduate nje ya nchi..sasa huko alikuwa anatumia lugha gani? Isitoshe ameongoza ma delegations chungu nzima kwenye mikutano ya kimataifa huko nako alikuwa bubu?
Tuache kuwa na nongwa wakati wote!
 
Pengine tatizo lipo katika uwezo wa kujieleza kwa kutumia Kiingereza.
 
China, Urusi, Japan wanatumia Kingereza au lugha zao kuendesha serikali?

Kwa Tanzania kiongozi wa nchi lazima ajue kiingereza maana ni lugha inayoeleweka na mataifa kibao. Sisi serikali yetu inaendeshwa kwa kuombaomba kwa wakubwa usifananishe na China, Urusi, au Japan hizi nchi kubwa jamani.. kama unadhani nakudanganya hebu jaribu nenda kakae barabarani uingereza ukiomba msaada kwa wapita njia kwa kiswahili kama utapata kitu. Lakini ukijua kiingereza ni rahisi kumueleza mtu kwamba "pliz give me moskwito nets then go to songea because you can dig ureniam":nono:
 
Kwa kuongezea tu huyu Mama kasoma post graduate nje ya nchi..sasa huko alikuwa anatumia lugha gani? Isitoshe ameongoza ma delegations chungu nzima kwenye mikutano ya kimataifa huko nako alikuwa bubu?
Tuache kuwa na nongwa wakati wote!

Kuna watu wengi wamesoma Chguo Kikuu lakini uwezo wao wa kuongea na kuelewa lugha ya kiingereza ni mdogo ajabu. Kuna watu wamesoma nje ya Tanzania(kwenye nchi zinazotumia lugha ya Kiingereza) lakini uwezo wao wa kuongea na kuelewa lugha ya kiingereza ni mdogo sana.

Hata sasa nenda kwa watanzania wanaoishi Uingereza unaweza kukuta wengine hata kiingereza bado mgogoro.

Lakini ili kuiwakilisha Tanzania, uwezo wa kuongea kiingereza si kitu kikubwa sana, kikubwa ni uwezo wa kichwa chako kufikiri, kuchanganua, kupima na kuamua. Naweza kusema tukiangalia yaliyopita huko nyuma haya yote ni matatizo kwa Sofia Simba. Hayuko mentally matured kuwa na public office au kuwa representative wa nchi. Kama kigezo ni merit na qualification, i do not think she does.

Kuna watu wanaongea kiingereza vizuri sana lakini IQ yao ni extremely low, wapo wengi tu. Kiingereza si kigezo kizuri cha uwezo wa mtu kufanya kazi.

Tuna mifano mzuri tu hapa Tanzania, Nani kati la Lau Masha na Mrema alikuwa waziri mzuri wa mambo ya ndani? Nani anaweza kuonge kiingereza vizuri?
 
Nakumbuka kuna wakati fulani waliwahi kumuita Dr alipokuwa wizara ya afya wenye taaluma ya wakaja juu Dr ikafa kifo cha mende, hivyo kujua kiingereza au la kwa ccm si hoja ila kuna umuhimu wa kufuatilia sehemu nyingine alizosoma asije akawa pure kihiyo hatupeleki watu kukaa tu tunataka wenye uwezo wa kuchaganua mambo internationally, lakini alikuwa waziri wa utawala bora pale ni kiswahili atakutana na mzungu gani
 
kwani kiswahili hajui? Hii nchi lugha ya taifa ni kisw

Kwa sasa uwaziri unatolewa kutokana na mapenzi ya anayeteua. Bila shaka kiswahili anajua, lakini kama kujua kiswahili ndio kigezo basi watanzania wengi sana wangeweza kuwa mawaziri.

Zamani ili mtu uteuliwe kuwa waziri, TISS walikuwa wanafanya scrutiny kubwa. Sasa ni tofauti, lakini wote wanajua kuongea kiswahili. Lakini tumesikia kuwa wengine ni mafisadi, wengine vihiyo, wengine ni wazi kabisa wanaingia kutokana na mteuaji kuamua tu na sio kutokana na uwezo wao.
 
Nakumbuka kuna wakati fulani waliwahi kumuita Dr alipokuwa wizara ya afya wenye taaluma ya wakaja juu Dr ikafa kifo cha mende, hivyo kujua kiingereza au la kwa ccm si hoja ila kuna umuhimu wa kufuatilia sehemu nyingine alizosoma asije akawa pure kihiyo hatupeleki watu kukaa tu tunataka wenye uwezo wa kuchaganua mambo internationally, lakini alikuwa waziri wa utawala bora pale ni kiswahili atakutana na mzungu gani

Si wazungu wote wanaojua kiingereza. Na anaweza kujua kiingereza vizuri sana lakini asiwe na uwezo wa kuchanganua hoja, kujieleza hata kuwa articulate. Angalia utendaji wake utawala bora, sikiliza kauli zake alizoongea hapo ndio unaweza kujua uwezo wake.
 
kwani wanakwendaga kule kuongea au kusikiliza tu? yaanai kukaa na kusema YES..YES..KILA KITU :doh::doh:YES
Ndio maana walimtoa kwenye kujieleza. Ila jamani aibu nyingine ziwe za hapa kwetu tu, bora hata wangempa cheo kingine hapa ndani kuliko kwenda kutuaibisha huko nje??? Hawa m..wa sijui wanataka tukiwa nje ya nchi tuone aibu ya kutaja taifa tunalotoka kwa aibu ya kuwa na mwakilishi ambae hajui lugha achilia mbali hana uwezo wa kuwakilisha mawazo yenye kujenga nchi. ONE DAY YES!!!!!
 
Kuna watu wengi wamesoma Chguo Kikuu lakini uwezo wao wa kuongea na kuelewa lugha ya kiingereza ni mdogo ajabu. Kuna watu wamesoma nje ya Tanzania(kwenye nchi zinazotumia lugha ya Kiingereza) lakini uwezo wao wa kuongea na kuelewa lugha ya kiingereza ni mdogo sana.

Hata sasa nenda kwa watanzania wanaoishi Uingereza unaweza kukuta wengine hata kiingereza bado mgogoro.

Lakini ili kuiwakilisha Tanzania, uwezo wa kuongea kiingereza si kitu kikubwa sana, kikubwa ni uwezo wa kichwa chako kufikiri, kuchanganua, kupima na kuamua. Naweza kusema tukiangalia yaliyopita huko nyuma haya yote ni matatizo kwa Sofia Simba. Hayuko mentally matured kuwa na public office au kuwa representative wa nchi. Kama kigezo ni merit na qualification, i do not think she does.

Kuna watu wanaongea kiingereza vizuri sana lakini IQ yao ni extremely low, wapo wengi tu. Kiingereza si kigezo kizuri cha uwezo wa mtu kufanya kazi.

Tuna mifano mzuri tu hapa Tanzania, Nani kati la Lau Masha na Mrema alikuwa waziri mzuri wa mambo ya ndani? Nani anaweza kuonge kiingereza vizuri?

Mkuu nakubaliana na wewe,kwa mfano tu..kuna watangazaji flani wa Redio1 hapa bongo illiyokua kwenye jengo refu kabisa mjini wanajua sana Kingereza ila walisoma chuo flani walichemsha vibaya sana na hawakugraduate na hadi leo hawana vyeti wamebaki kutangaza tu hapo mawingu.
So kuna watu hawajui kingereza cha kuongea sana ila kuandika wako poa!
Ila kwakweli kingereza ni muhimu sana kwa ulimwengu wa sasa,i wonder serikali inasema tutumie kiswa hadi University?are they serious?
 
MAFISADI WANAANGALIA MASLAHI SIYO UJUZI WAJAMENI
:A S angry:
 
Si wazungu wote wanaojua kiingereza. Na anaweza kujua kiingereza vizuri sana lakini asiwe na uwezo wa kuchanganua hoja, kujieleza hata kuwa articulate. Angalia utendaji wake utawala bora, sikiliza kauli zake alizoongea hapo ndio unaweza kujua uwezo wake.
HAPA bongolander,u is missing the point,mzungu wa barabarani kutojua kingereza does not affect anything,hata wewe mswahili kama hujui kiswahili maadam maisha yako ni ya kula tu uta survive the point ni kwamba huyu bibie carries the hope of tanzanians on her shoulder na katika omba omba yetu(misaada)inabidi awa convince donors sasa kama hawezi kuji express what next-one example MREMA akiwa waziri aliwasili GENEVA miaka hiyo akiwa na assistant ambaye ni fluent in both english and french-huyu assistant hakuwa na off sababu lazima awe by the side of mrema.Hapa ina maana serikali ilingia gharama ya bure sababu kiongozi wake fluency katika lugha ina mgogoro
 
sophia simba anaogopewa ni mbabe hii inaonyesha wababe wa ccm watakavyombuluza spika makinda
 
Back
Top Bottom