Bawabu wa pili
Senior Member
- Nov 14, 2025
- 147
- 432
Aliyekuwa Gavana wa Nairobi na Mfanyabiashara maarufu Nchini Kenya, Mike Sonko, amerejea tena kwenye ulingo wa siasa baada ya kusajili rasmi chama chake kipya, National Economic Development Party (NEDP), kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027.
Sonko aliondolewa katika nafasi ya Gavana wa Nairobi mwaka 2020 baada ya mchakato ulioanzishwa na Bunge la Kaunti ya Nairobi, kutokana na madai kwamba alikiuka sheria na kanuni za utawala wa kaunti, ikiwemo malalamiko kuhusu ukosefu wa uwazi katika matumizi ya fedha za umma na udhibiti duni wa rasilimali za kaunti.
Akipewa cheti cha usajili kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Sonko alisema chama chake kinajikita katika mageuzi ya kiuchumi na kuboresha ustawi wa Wakenya.
Sonko amewahimiza Wakenya kutoka makundi yote vijana, wazee na wafuasi wa vyama mbalimbali kujiunga na harakati hiyo mpya anayoitaja kama jukwaa la ujenzi mpya wa taifa.
Alisisitiza kuwa NEDP inalenga kuwa mshirika muhimu katika kuunda Serikali ijayo na kuchochea mabadiliko ya kiutawala na kiuchumi nchini.
“Hiki ndicho chama cha kuangalia. Tunajenga harakati itakayochangia kuunda serikali ijayo. Msingi wetu ni mageuzi ya kiuchumi, maendeleo, na kuboresha maisha ya Wakenya. Tunakaribisha kila mtu kuanzia Gen Z hadi wazee, kutoka matabaka yote ya kisiasa, yeyote anayetamani kuona mabadiliko nchini. Tushikamane na tufanye kazi pamoja,” alisema Sonko
Hatua yake ya kuzindua chama kipya inakuja wakati ambapo pia Naibu Rais wa zamani, Rigathi Gachagua, ameanzisha chama chake kipya, hatua ambayo imezua mjadala kuhusu mpangilio mpya wa kisiasa unaojengwa kuelekea uchaguzi wa 2027.
Wachambuzi wa masuala ya siasa nchini Kenya wamesema, uibukaji wa vyama hivyo vipya unaonekana kama dalili ya kuundwa kwa majukwaa mapya ya ushawishi hasa katika maeneo kama Mlima Kenya na taifa kwa ujumla.