dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,496
- 3,461
Katika hali isiyo ya kawaida Kijana Daudi Mwanjoka mkazi Kitongoji cha Majengo Ilembo Kata ya Vwawa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe alimfumania Mkewe akivunja amri ya sita (kuzini) ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa miaka minne nyumbani kwake.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Majengo Esioni Ntutule Kijalo ambaye alikua kwenye kikao cha upatanishi anaeleza kuwa mume (aliyefumania) alikua ametengana na mke tangu mwezi wa tano mwaka jana na walikuwa wanaishi pamoja japo walipanga nyumba moja.
Mwenyekiti Kijalo aliendelea kusema kua Mume ambaye aliemfumania Mkewe huyo kuwa alitengana na Mkewe kwa sababu kubwa ya ulevi wa kupindukia na kutokutoa matumizi katika familia yake.
Mwanaume aliemfumania Mke wake na Mwanaume mwingine usiku nyumbani kwao aliamua kuufunga mlango kwa nje na kumfanya Mwanaume aliefumaniwa kubaki chumbani hapo hadi asubuhi Watu walivyoitwa.
Kiongozi wa Kijiji amesema kwamba Mume huyo alipoamka asubuhi alikwenda kutoa taarifa kwa uongozi wa Serikali ya kijiji na baada ya kukaa chini na walikubaliana Mwanaume huyo aliefumaniwa na Mke wa mtu alipe shilingi laki nne kama faini, Mwanaume aliefumania amemsamehe Mke wake na sasa wanaendelea kuishi pamoja,