Songwe: Mwaume amfamania mke wake na kumsamehe, ni baada ya kulipwa faini ya laki nne

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,364
2,000
Katika hali isiyo ya kawaida Kijana Daudi Mwanjoka mkazi Kitongoji cha Majengo Ilembo Kata ya Vwawa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe alimfumania Mkewe akivunja amri ya sita (kuzini) ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa miaka minne nyumbani kwake.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Majengo Esioni Ntutule Kijalo ambaye alikua kwenye kikao cha upatanishi anaeleza kuwa mume (aliyefumania) alikua ametengana na mke tangu mwezi wa tano mwaka jana na walikuwa wanaishi pamoja japo walipanga nyumba moja.

Mwenyekiti Kijalo aliendelea kusema kua Mume ambaye aliemfumania Mkewe huyo kuwa alitengana na Mkewe kwa sababu kubwa ya ulevi wa kupindukia na kutokutoa matumizi katika familia yake.

Mwanaume aliemfumania Mke wake na Mwanaume mwingine usiku nyumbani kwao aliamua kuufunga mlango kwa nje na kumfanya Mwanaume aliefumaniwa kubaki chumbani hapo hadi asubuhi Watu walivyoitwa.

Kiongozi wa Kijiji amesema kwamba Mume huyo alipoamka asubuhi alikwenda kutoa taarifa kwa uongozi wa Serikali ya kijiji na baada ya kukaa chini na walikubaliana Mwanaume huyo aliefumaniwa na Mke wa mtu alipe shilingi laki nne kama faini, Mwanaume aliefumania amemsamehe Mke wake na sasa wanaendelea kuishi pamoja,
 

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
6,223
2,000
Etiii kwa nini uuee,ulawiti,upige na kuumiza kwa ajili ya mtu ambae mumekutana nae ukubwani?

Wanaume wote mnaojeruhi wagoni wenu wajinga sana,mnatudhalilisha hamna subra,hamna uvumilivu kabisa.

Ukifumania samehe.ni pigo kubwa sana kisaikolojia kwa uliowafumania.
Au kama vipi unapigapesa kama huyu.
 

Kashishi yetu

JF-Expert Member
Mar 22, 2014
2,370
2,000
"AKAWAFUNGIA NDANI KISHA AKAENDA KULALA KWAKE, ASUBUHI KULIPOKUCHA NDO AKAENDA KUSHITAKI KWA MWENYEKITI WA SERIKALI"


😔😂🤣😁 Duh. KWA hiyo jamaa lilipiga paipu usiku kucha Hadi asubuhi!!
 

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
26,157
2,000
"AKAWAFUNGIA NDANI KISHA AKAENDA KULALA KWAKE, ASUBUHI KULIPOKUCHA NDO AKAENDA KUSHITAKI KWA MWENYEKITI WA SERIKALI"


Duh. KWA hiyo jamaa lilipiga paipu usiku kucha Hadi asubuhi!!
Sasa kama umefungiwa na mlango kabisa unazan atakua alikua akifanya nini, unazan nae alikua akiomba kama Paulo na asila ili mlango ufunguke

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom