Songwe: Amuua mtoto wa mumewe akimtuhumu kupoteza ng’ombe wawili

Boran Jakutay

Senior Member
Apr 8, 2023
110
255
Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limethibitisha kumkamata Veronica Petro (24) mkazi wa Wilaya na Mkoa wa Songwe akituhumiwa kumuua mtoto wa mume wake, Mageshi Usiga (7) aliyekuwa akimlea.

Kamanda wa polisi mkoani humo, Theopista Malya, amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo baada ya mtoto huyo kupoteza ng’ombe wawili akiwa machungani mwishoni mwa mwezi Februari.

“Mtu anayeitwa Usiga Nabinilo mwenye umri wa miaka 42, aligundua kuuwawa kwa mtoto wake mwenye umri wa miaka 7 aitwaye Mageshi Usiga, na inadaiwa kwamba aliuwawa na mama yake wa kambo.

“Baada ya kufuatilia tuligundua kwamba mama huyu alimtandika mtoto huyu lakini pia alikuwa akimkanyanga maeneo ya kichwani na kifuani, ikapelekea kifo chake.

“Baada ya kuhakikisha mtoto huyo amekufa akaenda kumtupa umbali kama wa mita 352 kutoka nyumbani wanapoishi, lakini polisi walipofika walimchukua mtoto huyo na kumpeleka hospitali kwa uchunguzi kugundua sababu ya kifo chake.

“Lakini sababu iliyopelekea kumpiga mtoto huyo, tarehe 28 mwezi wa pili, huyo mtoto alikuwa machungani na ng’ombe wawili kupotea, ndiyo kilichopelekea mama huyo kumpiga mtoto hadi kumuua.

“Huyo mama kwa sasa yupo magereza kwa ajili ya kesi hiyo inayomkabili ya mauaji,” alisema kamanda Malya.

CHANZO: UFM RADIO
 
Kuna mwingine huko Arusha kamuua Mpenzi wa mama yake huku akimtoa mama yake kutoka Kwa huyo bwana uchi wa mnyama, laana
 
Huyu mtoto bado alikuwa mdogo sana, hakustahili kupewa mifugo ili akachunge akiwa peke yake bila ya usimamizi wa mtu mzima.

Kwa hiyo, hata kama angepoteza mifugo au ng'ombe wote waliopo kwenye zizi, bado hakustahili kupewa adhabu yoyote ile zaidi ya kuonywa kwa maneno tu kwa sababu kosa siyo lake, kosa lipo kwa yule aliyemkabidhi mifugo ili akachunge.

Kwa hiyo acha huyo mama yake wa kambo aliyesababisha kifo chake avune alichopanda.
 
Jamani miaka 7 kuchunga ng’ombe serikali kupitia wizara husika walikuwa wapi?yaani jamii haikumtendea haki malaika huyo.R.I.P
 
42-24=age gap 18 .Hasira za kutandikwa na mume karudisha kwa mtoto. Anyway ng'ombe hazeeki maini endeleeni kuoa vibinti vidogo na kuvipa majukumu makubwa. Hakunaga single dad duniani

R.I.P Little Angel
 
Jeshi la Polisi mkoani Songwe limekiri kumkamata Veronica Petro mwenye umri wa miaka 24, mkazi wa Wilaya ya Songwe, kwa tuhuma ya kumuua mtoto wa mume wake aliyekuwa akimlea ajulikanaye kwa jina la Mageshi Usiga mwenye umri wa miaka 7 kwa kosa la kupoteza ng’ombe wawili, wakati akiwa machungani mwishoni mwa mwezi Februari, 2023.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Theopista Malya amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo mwezi mmoja baada ya ng’ombe hao kupotea kwa kumpiga na kumkanyaga sehemu za kifuani na kichwani kisha kumtupa umbali wa mita 52 kutoka nyumbani kwao.

Je, unadhani nini kifanyike kukomesha matukio ya ukatili kwa watoto wadogo, ambayo yameonekana kutokoma?
 
42-24=age gap 18 .Hasira za kutandikwa na mume karudisha kwa mtoto. Anyway ng'ombe hazeeki maini endeleeni kuoa vibinti vidogo na kuvipa majukumu makubwa. Hakunaga single dad duniani

R.I.P Little Angel
Wivu
 
Huyu mtoto bado alikuwa mdogo sana, hakustahili kupewa mifugo ili akachunge akiwa peke yake bila ya usimamizi wa mtu mzima.

Kwa hiyo, hata kama angepoteza mifugo au ng'ombe wote waliopo kwenye zizi, bado hakustahili kupewa adhabu yoyote ile zaidi ya kuonywa kwa maneno tu kwa sababu kosa siyo lake, kosa lipo kwa yule aliyemkabidhi mifugo ili akachunge.

Kwa hiyo acha huyo mama yake wa kambo aliyesababisha kifo chake avune alichopanda.
Duu mtoto wa miaka saba
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limethibitisha kumkamata Veronica Petro (24) mkazi wa Wilaya na Mkoa wa Songwe akituhumiwa kumuua mtoto wa mume wake, Mageshi Usiga (7) aliyekuwa akimlea.

Kamanda wa polisi mkoani humo, Theopista Malya, amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo baada ya mtoto huyo kupoteza ng’ombe wawili akiwa machungani mwishoni mwa mwezi Februari.

“Mtu anayeitwa Usiga Nabinilo mwenye umri wa miaka 42, aligundua kuuwawa kwa mtoto wake mwenye umri wa miaka 7 aitwaye Mageshi Usiga, na inadaiwa kwamba aliuwawa na mama yake wa kambo.

“Baada ya kufuatilia tuligundua kwamba mama huyu alimtandika mtoto huyu lakini pia alikuwa akimkanyanga maeneo ya kichwani na kifuani, ikapelekea kifo chake.

“Baada ya kuhakikisha mtoto huyo amekufa akaenda kumtupa umbali kama wa mita 352 kutoka nyumbani wanapoishi, lakini polisi walipofika walimchukua mtoto huyo na kumpeleka hospitali kwa uchunguzi kugundua sababu ya kifo chake.

“Lakini sababu iliyopelekea kumpiga mtoto huyo, tarehe 28 mwezi wa pili, huyo mtoto alikuwa machungani na ng’ombe wawili kupotea, ndiyo kilichopelekea mama huyo kumpiga mtoto hadi kumuua.

“Huyo mama kwa sasa yupo magereza kwa ajili ya kesi hiyo inayomkabili ya mauaji,” alisema kamanda Malya.

CHANZO: UFM RADIO

Nashawishika na Mimi kusema single Mama wasioelewe, Maana wanawake hawajawahi kuweza leo watoto wa wanaume.

Wana roho Mbaya kuliko chochote
 
Back
Top Bottom