KERO Ukiwa na mkopo Songesha hupati mkopo benki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

nusu kaputi

Member
Feb 1, 2014
42
98
Songesha na mikopo mingine ya simu imepelekea watumishi kunyimwa mikopo wanapoenda bank kukopa, na hii ni kutokana na mamlaka zinazosimamia mikopo kuweka utaratibu wa madaraja high risk, risk na low risk katika kadiri mteja anaposongesha.

Hilo limetokea leo mimi mwenyewe nilipoenda bank na kuingia kwenye mfumo wa ESS Utumishi, bank walivyoingia na kutumia mkopo ukawa rejected, nikaenda Voda nikawalipa Songesha yote lakini bado mfumo ulisoma high risk.

Nawashauri wale ambao hamjaingia kwenye hili jini songesha msijaribu, mbeleni litawaleta shida.

Mamlaka zinasimamia Mikopo hili la simu hasa mikopo ya Nivushe, Songesha, Gold, Bustisha ziwe na term of condition, yaani taratibu za mwanachama kukubali.
 
Mikopo yote inayopitia kwenye simu kama Songesha nyuma yake kuna bank. Kwa mfano. Songeshahutolewa na TCB. Na hii mikopo yote husajiliwa kwenye credit bureau.

Credit bureau ni Database ya wakopoja. Kadri unavyokopa na kulipa hii database ina kupa rates ambazo wakopeshaji wanaweza kuzitumia kufanya assesment kama unakopesheka au la.

Cha msingi siyo kuacha kukopa, ila ni kukopa na kulipa kwa wakati.
 
Unataka kusema Mteja wa Vodacom Songesha anaweza kuwa na Deni linaloweza kuathiri kukopeshwa na Benki?

Kivipi jambo hilo likahusiana?
Kama hili halipo basi ni hatari sana na pengine wamechelewa tu kunganisha. Kwenye mikopo, inatakiwa system iliyokuwa intergrated, yaani ukitaka kukopa institution A, wawe na uwezo wa kuona kama umeshakopa au una mkopo sehemu nyingine zote zinazokopesha. Bila kuwa na uwezekano wa namna hii, mtu mmoja anaweza kukopa sehemu nyingi na akakimbia na fedha. Ndiyo maana nchi zilizoendelea kuna kitu kinaitwa credit rating, yaani ni namna ya kuonyesha mkopaji ni mtu wa aina gani, ana mikopo mingi? Ana tabia ya kulipa madeni?
 
Mikopo yote inayopitia kwenye simu kama Songesha nyuma yake kuna bank. Kwa mfano. Songeshahutolewa na TCB. Na hii mikopo yote husajiliwa kwenye credit bureau.

Credit bureau ni Database ya wakopoja. Kadri unavyokopa na kulipa hii database ina kupa rates ambazo wakopeshaji wanaweza kuzitumia kufanya assesment kama unakopesheka au la.

Cha msingi siyo kuacha kukopa, ila ni kukopa na kulipa kwa wakati.
Tatizo wengi wanadhani kampuni za Simu ndizo zinakopesha

Hawaelewi Kwa hiyo mtu akopa halipi anabadili line akikiona mjanja kumbe deni ni la Benki na liko pale pale siku akitaka kukopa Benki Ndipo atakiona Cha Mtema Kuni ataambiwa hakopesheki

Dawa ya deni kulipa
 
Songesha Iko Chini ya Tanzania Commercial Bank ni kitengo Cha Cha benki ukikopa ni sawa na umekopa benki record zako linaonyesha ulikopa benki ya Tanzania Commercial bank na hulipi
Aaagh wapi kuna mahali walisema hivyo wakati wanakukopesha au hujui kuna haki ya mkopiaji pia?
 
SONGESHA na MIKOPO mingine ya simu Mimi mwenyewe nilipoenda bank na kuingia Kwenye mfumo wa ess utumishi, bank walivyoingia na kutumia mkopo ukawa rejected, nikaenda voda nikawalipa SONGESHA yote lakini Bado mfumo ulisoma high risk.
Kwa maana hiyo ulikuwa unadaiwa Songesha ila hutaki kuwalipa Vodacom . Badala yake ukaenda kukopa kwingineko ili nao usiwalipe.
Nawashauri wale ambao hamjaingia Kwenye hili jini SONGESHA msijalibu mbeleni litawaleta shida
Kama ambavyo Vodacom wameshauri wakopeshaji wenzao wasikukopeshe maana una udhaifu wa kutolipa deni.
Mamlaka zinasimamia Mikopo hili LA simu hasa Mikopo ya nivushe,SONGESHA,Gold,bustisha ziwe na term of condition,Yani taratibu za mwanachama kukubali
Ina maana Songesha walikukopesha hela bila wewe kukubali?

Hukuwa umeomba, au uliomba ila "haukukubali"?

Hela hiyo uliyosongobekwa kwa lazima ulitumia au hukutumia?
 
Back
Top Bottom