Songea to Mwanza: Mwamba katoa chuma na kaanzisha hii route

Mwanza - Songea kupitia Dar? Hii route itakuwa balaa, hebu kaangalie atlas yako kwanza uone kutoka huku kwenda kule unapita wapi na wapi
Binafsi wa kupitia Dar ni usumbufu, wakati kuna short cut way ile ya njombe via iringa, also ni kero na uchovu usiyo na umuhimu kwa abilia.
 
Kwako wewe Ushabiki ni upi na uhalisia ni upi?
Kumpa mtu chapuo kwa mazuri pekee japo sio yake na ukayaficha madudu yake huo ndo ushabiki kwa sababu tuu una mahaba nae uhalisia ni kumpa chapuo mwenye lake bila kujali Kama una mahaba nae au chuki dhidi yake
 
Hakika ubora wa miundombinu ya barabara ikiwa mizuri hakuna kinachoshindikana.

Muda huu ni saa 22:30 basi la kampuni ya Super Feo limeondoka Singida kuelekea Jiji la miamba Mwanza.

Wale wadau wa usafirishaji mnaionaje na imekaaje hii..?

Asee kajitahidi ni parefu sana ila unatumia mda gan kufika?
 
Kumpa mtu chapuo kwa mazuri pekee japo sio yake na ukayaficha madudu yake huo ndo ushabiki kwa sababu tuu una mahaba nae uhalisia ni kumpa chapuo mwenye lake bila kujali Kama una mahaba nae au chuki dhidi yake
ukayaficha madudu yake kwani topic hapa ni ipi? Mtu mzima ufikiri kindergarten
 
Hivi hakuna route yoyote ya Mtwara - Arusha
Haipo ila wenye macho ya kuona wanaweza kuanzisha hii.

Mfano Esta Luxury huyu naona anaanza kufunguka kuna yule jamaa wa kusini Mining Nice anaweza ila wanasubiri kitu gani sijui.

Zakaria Express anaweza maana akisikia hii atakuja fasta.
 
Umeandika kitu gani hicho?

Au una maana hii.
1. Kibaoni ni kijiji chetu pale Handeni mkoani Tanga.
2. Mwenge ni kata maarufu ndani ya manispaa ya jiji la Dar.
3. Misufini ni eneo linalopakana mjini Morogoro.
4. Ginnery alimaarufu kwenye mikoa iliyolima pamba, so kulikuwa na vile viwanda vya kuchambua mbegu za pamba miaka ya 1980's vilivyopelekea eneo husika kupewa jina hilo.
5. Stendi ya zamani, nowdays kila mkoa unakuwa na stendi ya kale hapa Dar unaona kutokea ubungo.

👉🏾Sina nia mbaya ila najaribu kutaka kujua una maana gani kwa reply yako!.
Mkuu, mbona kuna kariakoo ya kinyerezi pale, magomeni ya Tanga, posta ya posta mpya na posta ya majumbasita!? Hii mitaa majina yanajirudia kila sehemu ni sawa na useme gari langu huwa ninalilaza CCM pale, maana hizo CCM zinazolaza magali na pikpik zipo nchi nzima. Kwa hiyo huyo jamaa yupo sawa tu.
 
Wewe ndiyo unatooa nje ya mada kabisa aseee...!, Hebu fuatilia kwa umakini uelewe alichoandika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom