Songea: Sita jela miaka 50 kwa kutaka kuipindua Serikali ya Tanzania ili kuanzisha Taifa la Kiislamu

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,616
Sita jela miaka 50 kwa kutaka kuipindua Serikali ya Tanzania

Hukumu hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki mbele ya Jaji Dk. Yose Mlyambina kwenye Masijala Ndogo ya Songea.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Seif Chombo, Abdallah Chombo, Mohamed Kamala, Athumani Chombo, Omary Mbonani na Rashidi Ally.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Yose alisema washtakiwa wanatuhumiwa kati ya Januari Mosi 2014 na Julai 13, 2020, kwenye maeneo tofauti wilayani Tunduru mkoani Ruvuma na maeneo mengine nchini, kwa pamoja walikula njama ya kufanya ugaidi.

Wanadaiwa kula njama kuanzisha vita ya kidini vijulikanavyo Jihad na kuwashawishi vijana kuongeza nguvu kuipindua Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuanzisha Taifa la Kiislamu kwa kutumia nguvu na machafuko.

Alisema malengo yalikuwa kuongoza kwa kutumia sheria za Kiislamu, washtakiwa walipekelekwa nchi mbalimbali zenye uongozi wa Kiislamu kwa ajili ya mafunzo zaidi ya Jihad kinyume cha sheria na taratibu za Jamhuri Muungano wa Tanzania.

"Kitendo hicho hakihatarishi tu maisha ya watu wengine, bali hata wao wenyewe, ni hatari kwa maisha yao, " alisema Jaji Yose.

Washtakiwa walifikishwa mahakamani kwa makosa mawili ya kula njama kufanya ugaidi na kushiriki vikao vya kufanya ugaidi.

Washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo kwenye Kijiji cha Lumbukule na maeneo mengine wilayani Tunduru, Mkoa wa Ruvuma ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ilidaiwa mahakamani huko kuwa washtakiwa kwa pamoja na wengine ambao hawakuwapo mahakamani, walishiriki kufanya kikao kinachohusiana na masuala ya ugaidi, kula njama ya kutaka kuanzisha Serikali ya Kiislamu kwa kutumia nguvu kwa malengo ya kuvuruga mfumo wa kisiasa, kiuchumi na kijamii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Washtakiwa hao walikana mashtaka hayo, lakini walikiri kukamatwa na waliposomewa hoja za awali, walizikana isipokuwa majina yao, wakazi wa Lukumbule, walikubali kwamba walikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi na kwamba wanaujua msikiti wa Al Malidi na wanaishi kwenye kijiji hicho tangu mwaka 2017 mpaka 2020.

Katika kesi hiyo, Jamhuri iliwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Hebel Kihaka aliyesaidiana na Tulimanywa Majigo na Edgar Bantilaki.

Washtakiwa walikuwa wakiwakilishwa na Mawakili Naomi John, Nestory Nyoni Rafael Matola, Alex Nyoni, Razaro Simba na Denis Razaro.

Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi wanne na vielelezo vitano.

Washtakiwa walijitetea wenyewe kwa kiapo na hakuna aliyekuwa na kielelezo chochote.

Miongoni mwa ushahidi uliotolewa ni kwamba serikali iliharibu kambi yao maeneo ya Lukumbule, Tunduru maeneo ya Magazini, Nanyumbu, Ntamba Swala mpakani mwa Msumbuji, Tandahimba, Newala na Masasi na Mtwara.

Ushahidi ulidai malengo ya washtakiwa yalikuwa uamuzi wote ufanyike chini ya misingi ya Quran Tukufu.

Inadaiwa viongozi wao wanaishi Ruvuma, Lindi, Mtwara na Pwani na kwamba viongozi wachache walikamatwa huku wengine wakifanikiwa kukimbilia Msumbiji.

Pia ilidaiwa wahalifu hao waliua na kuharibu vijiji ambavyo viligoma kuungana nao, walichukua mali za watu zikiwamo fedha na kuharibu mali zisizohamishika.

Hata hivyo, washtakiwa wakati wa utetezi walikana kuhusika kufanya matukio hayo.

Mahakama baada ya kusikiliza shauri hilo, ilijiridhisha kwamba upande wa Jamhuri umeweza kuthibitisha makosa dhidi ya washtakiwa bila kuacha shaka.

"Mahakama ilijiridhisha kuwa washtakiwa wote walikula njama kutaka kuipindua serikali iliyoko madarakani na walipata mafunzo.

"Kutokana na ushahidi ulioko, mahakama ilizingatia maombi ya washtakiwa kupunguziwa adhabu lakini kutokana na makosa waliyotenda, mahakama inawatia hatiani na kuwapa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka 20 kwa kosa la kwanza na miaka 30 kwa kosa la pili, adhabu zote zinakwenda kwa pamoja," alisema Jaji.

Mahakama iliwapa haki yao ya msingi kama hawakubaliani na adhabu wanaruhusiwa kukata rufani.

Chanzo: Nipashe
 
Wanadaiwa kula njama kuanzisha vita ya kidini vijulikanavyo Jihad na kuwashawishi vijana kuongeza nguvu kuipindua Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuanzisha Taifa la Kiislamu kwa kutumia nguvu na machafuko.
Wanadaiwa kula njama kuanzisha vita ya kidini vijulikanavyo Jihad na kuwashawishi vijana kuongeza nguvu kuipindua Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuanzisha Taifa la Kiislamu kwa kutumia nguvu na machafuko.
 
Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Uhujumu Uchumi na Rushwa imewatia hatiani watu 6 na kuwahukumu kwenda jela Miaka 50 kila mmja kwa kosa la kula njama ya Kupindua Serikali ya Tanzania.

Swali ,Swali je Ni kina Nani hao na walitaka Kupindua Serikali yetu lini?.

Source: Nipashe.
Screenshot_20221220-101107.png
 
Hivi kweli watu sita wanapindua serikali kwa kutumia visu? Maana hawakupatikana na silaha.

Kufanya fujo ingeeleweka.
Huwa wanaanzaga tararibu,mkichelewa ndo matokeo wanakuwa kundi kubwa sana la kigaidi kama alishabab,al queda,m23,boko haram.

Wakifikia hiyo stage wanapata wafadhili na kuanza kusumbua serikali..ndo vile unasikia mara wamevamia shule wamesomba wanafunzi na kuwateka,wamelipua soko nk

Na hapo unaambiwa kuna wengine hawajakamatwa wamefanikiwa kukimbilia msumbiji,so ni wengi.
Haya mambo sio ya kuchekea
 
Back
Top Bottom