Songea ni moja ya mji ninaohusudu

Songea ni moja ya mji ninaohusudu

Mambo yetu yale vipi pande hizo,maana wengine bila mambo hizo,tutaona mji haufai kabisa?
 
Habari wakuu.

Ni miaka 5 sasa imepita tangu mara ya mwisho kuwepo katika mji wa Songea,ukweli ni moja ya miji midogo Tanzania ambao ulinivutia sana na kupenda maisha ya pale. Nimewahi ishi miji kadhaa kwa nyakati tofauti kama Mtwara mjini,Mafinga mjini,Njombe mjini,Mbeya Mjini,Tanga mjini nk. Ila songea ni miongoni mwa mji wa pekee niliopenda sio kwa majengo bali aina ya maisha ya pale.

1. Mji umepoa hakuna vurugu
2. Vyakula bei chee sana tena vingi vya asili
3. Kodi ya pango bei kitonga mno
4. Hali ya hewa sio baridi wala sio joto
5. Kuna mazao mengi ya biashara ukiwa mchakarikaji unapata cha kufanya(nimewahi uza dagaa nyasa).
6. Wenyeji wakarimu na wanapiga kazi sio wavivu kama Tanga,Mtwara.
7. Watu wa Songea wana heshima sana sio mtoto wala mkubwa.
8. Safari yake ina advanture kubwa na inavutia.

Madhaifu
1. Mji bado mdogo hauna maendeleo ya majengo mazuri
2. Sehemu ya starehe chache
3. Mzunguko wa hela kwa mjini mdogo ila ukiwa unasafirisha bidhaa utapata pesa.
4. Kuna vumbi sana
5. Nyumba nyingi ni chakavu sana

Waliokuwa Songea wekeni comment hapo je kwasasa mji upo vipi?
nilikuwa pale mwaka 2015. Mungu akipenda nitafika tena siku moja. Nilipapenda.
 
Mgosi, umefika Lushoto?
 
Masasi nakubali sana Nyama choma pale uwanja wa fisi Nyuma ya Stand kuu Mabasi. Pia ule mji ni kama uko Pwani samaki kama wote Changu, vibua, Pweza..
Ohhhh Masasi kuchele😁
Masai you eat meat at your own risk 😂
 
Songea mjini ,huwezi kusema kuna baridi kama umewahi ishi Njombe,mafinga au iringa mjini na mbeya
Songea Kuna baridi mkuu yawezekana kipind ulichoenda ulikuwa msimu wa baridi umeisha.. Unapotaja kote ni nyanda za juu kusini kunakuzidiana barid ila sio kwamba Songea hakuna baridi fanya research yako tena
 
Back
Top Bottom