Somo nililopata kupitia kwa Hayati John Pombe Magufuli

Seniweba

Senior Member
Apr 14, 2021
179
412
Leo ikiwa ni mwaka mmoja umepita tangu Rais wa awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli afariki, nimekaa chini muda fulani nikatafakari siku hii ya kumbukizi ya kifo chake, Kuna somo nimelichukua kupitia kwake. Kwa kulinganisha kipindi akiwa hai na baada ya kutuacha, somo hilo ni kutokuogopa kusemwa, kwa maana kazi ya mdomo ni kusema.

JPM anabaki kuwa kiongozi aliyekuwa na maono, maamuzi na aliyesimamia kile anachokiamini bila kujari maneno ya watu, ndiyo maana kipindi cha korona wakati dunia nzima inaenda kushoto, yeye peke yake anaenda kulia bila kujari maneno ya watu. Maana hata ungefanya Jambo zuri namna gani bado Kuna watu watakusema vibaya.

Ukiwa mchamungu wapo watakaosema, ' anajifanya mkatoliki zaidi ya papa', usipokuwa mchamungu watasema, ' Shetani amemweka mfukoni '.

Mheshimiwa akibaki nchini watasema, ' Hajui kiingereza anaogopa ataongea Nini Ughaibuni ', akitoka nje ya nchi watasema, ' huyu nae! anapenda kwenda kwa mabeberu, utadhani ndo nyumbani kwao'.

Mtu akitoa hotuba fupi, Kuna watu watajitokeza na kusema, ' Hakujiandaa', akitoa hotuba ndefu watasema, 'hajui kutunza muda'.

Kiongozi akiwa mzalendo na mwenye nia njema kwa taifa lake wapo watakaosema, ' Mzee yule alikuwa mshamba yaani hata hakuwaingiza watoto wake kwenye MFUMO, ona wanavyoteseka sasa', akiwaingiza kwenye MFUMO utasikia kelele, ' hii nchi keki ya taifa inaliwa na walewale miaka yote, baba anamwachia mtoto, mtoto anamwachia mjukuu wa baba, mjukuu anamwachia kitukuu, sisi wanyonge ndo hivyo'.

Mtu akiaga dunia katika umri mdogo wapo watakaosema, 'angefanya mengi mazuri', akifika umri wa uzee wapo watakaosema, ' miaka yake yote aliiharibu tu bila kufanya chochote'.

Mtu akisoma sana Kuna watu watasema, ' Elimu yake haijamkomboa, yaani ni hasara siyo tu kwa familia yake bali na kwa taifa', asiposoma watasema, 'kipaji anacho, tatizo shule hana'.

Akiwa mtoto mchanga watasema, ' ni malaika huyu' akiwa mtu mzima watasema, ' achana na Shetani yule'.

Kiongozi akiwa na maono kwenye vitu vinavyokuza uchumi wapo watakaosema, ' sasa ananunua ndege hizi za Nini na wakati mashuleni bado matundu ya vyoo hayatoshi' asiponunua ndege utasikia, ' utalii bila ndege zako hata haulipi'.

Mtu akiwa mkarimu kuna watu watajitokeza na kusema, 'anajitangaza' asipokuwa mkarimu watasema ' ana gundi mikononi'.

Kupitia Hayati John Pombe Magufuli, nimepata somo na kuamini ukiongozwa na maneno ya watu, itakuwa ngumu kuyafikia malengo na ndoto zako. Acha uonekane kichaa leo ili kesho wakushangae.
 
Zile 2,000,000,000,000 vipi? maana kuzihesabu mtu mmoja bila mashine mwaka unaisha bado hajamaliza.
 
Back
Top Bottom