SoC04 Somo la mahusiano lifundishwe shuleni ili kupunguza matatizo ya kijamii

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mwanasayansi Kalivubha

Senior Member
Feb 4, 2024
107
276
Makazini utakutana na matatizo mengi ambayo chanzo kikubwa ni mahusiano mabovui, Ukija Mtaani pia utakuta kesi nyingi chanzo kikubwa ni mahusianomabovu.

Mahusiano ni zaidi ya mapenzi kama wengi wanavyolitumia neno hilo bali hali yoyote ya kimawasiliano kati ya mtu na mtu.

Baadhi ya Afisa rasilimali watu na viongozi wengine makazini wanashindwa kuhusiana vyema na wafanyakazi wao mpaka unajiuliza hivi kipindi anaajiriwa huyu hakufanyiwa tathimini kabla?Maana majibu yake kwa asilimia kubwa yana ashiria shari tu.

Inapunguza ufanisi makazini kwa sababu ya mawasiliano mabovu

Huongeza idadi ya vifo hasa kujinyonga kwa sababu mtu anashindwa kuhusiana vyema kiasi cha kubaki na matatizo yake mpaka yanamlemea na kuamua kujiua.

Malezi ni moja ya sababu inayoweza kusababisha tatizo la kushindwa kuhusiana na jamii vizuri ila kama watu wakipewa mbinu za mahusiano toka awali kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza ufanisi kiasi cha kupunguza athari za malezi.
 
Malezi ni moja ya sababu inayoweza kusababisha tatizo la kushindwa kuhusiana na jamii vizuri ila kama watu wakipewa mbinu za mahusiano toka awali kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza ufanisi kiasi cha kupunguza athari za malezi.
Tukiwekeza kwenye kujenga taifa lenye mahusiano imara na mazuri....maendeleo ni kugusa tu. Kwanza kimsingi hayo ndiyo maendeleo menyewe kwanza. Ahsante
 
Back
Top Bottom