Mwanzoni mwa karne ya kwanza huko uyahudi alitokea kijana mdogo aliyejitokeza kupinga na kukosoa baadhi ya taratibu dini ya kiyahudi. Kutokana na umahiri wake katika kuhubiri alifanikiwa kupata wafuasi wengi na kuonekana ni tishio kwa dini na uongozi wa wakati huo.
Viongozi walikaa chini na kuona ni jinsi gani ya kumdhibiti kabla hali haijawa mbaya zaidi. Waliamua kumutengenezea mashtaka ya uongo na wakafanikiwa kuhukumu adhabu ya kifo, akauawa.
Baada ya kifo chake viongozi walisherehekea na kujipongeza kwa kumdhibiti mazushi huyo. Ajabu ni kwamba mpaka sasa zaidi ya miaka 2000 baadaye bado mafundisho na mahubiri yake ni maarufu zaidi duniani kuliko ya binadamu yeyote aliyewahi kuonekana kwenye uso wa dunia.
Kumbe kufungulia watu mashtaka ya uongo hakujawahi kuzima mahitaji ya wakati husika. Tumeona Afrika kusini, Zimbabwe nk. Tanzania je watafanikiwa na kubadili historia?