Somo kuhusu nyoka

Kama umejenga eneo ambalo nyoka walikuwepo hapo kabla inakua kama umevamia makazi Yao..... Utawaua mara Kwa mara.

Kuna miti maalum ambayo hupandwa kama uzio... Miche yake hufanana kama mche wa kisamvu na ipo mingi tuu inauzwa mitandaoni.

Kama unavichaka au bustani za maua kuzunguka nyumba, Jenga tabia ya kumwagia oil chafu mara Kwa mara kuzunguka nyumba na njia zinazoingia nyumbani kwenu.

Kama eneo lenu lina historia ya kutembelewa na wadudu hao mara Kwa mara, ukigundua shimo lisilo la kawaida /pango hata kama ni la panya maana nyoka hawawezi kuchimba wenyewe, chukua tambara lilowanishe Kwa mafuta ya kondoo Kisha lichome juu ya shimo ambalo una mashaka nalo.

Jiwe la nyoka unaweza kujiandalia Kwa kutumia mfupa wa mnyama haswa ule wenye "porous surface". uweke jikoni uchomeke Kwa muda mrefu sana, hifadhi kama kifaa Cha huduma ya kwanza.
 
Mkuu msaidizi alikuwa sahihi kusitisha ombi la papuchi, we mwanamke umezidi ujasiri
 
Maswali yote Yale hamna hata moja lililojibika .ngoja niwe mvumilivu wajuzi wa mambo labda wapo njiani wanakuja.
 
Ha
Hapo kwenye jiwe la nyoka panahitaji ufafanuzi mkuu.
 
Kipindi nipo advance kuna mwenzetu aligongwa na kifutu dah ilikua noma sana anapelekwa hospital anaambiwa hamna dawa mpaka southAfrica aliteseka sana

Kuna muda amelala hajitambui anatema mapovu huku anaita mama nikajua anakata roho lakini Mungu ni mwema alipelekwa kwao akapata tiba maisha yakaendelea
 
Chatu alikaribia kunimeza nilipokuwa katika kijiji changu. Lakini sina muda wa kueleza .
 
Yaani wakati unapeleka mkono wako kwenda kumkamata, alikuwa ametulia tu kama vile paka anavyokuwaga anatulia anaposhikwa shingoni?
Nyoka ni mmoja kati ya wanyama ambao hushambulia pale anapohisi hatari (japo kuna vipanya road vya huko). Na moja kati ya ishara ya hatari kwa mnyama yeyote ni kiumbe kingine kupatwa na hofu. Hofu hufanya uwe na wazo moja tu kwa muda husika. Aidha upambane ama ukimbie. Nyoka kama wanyama wengine, akiona una hofu anajua utamshambulia tu lazima. Na hofu hiyo huihisi kwako kupitia mitetemo na moyo wako kwenda mbio. Iwapo utakuwa huna hofu na ukamkaribia nyoka kwa ujasiri bila kushtuka, unamuweza kirahisi sana.
 
Ha

Hapo kwenye jiwe la nyoka panahitaji ufafanuzi mkuu.
Mechanism ya kufanya kazi ya jiwe la nyoka ni ule uwezo wake wa kufyonza Kwa kua zina high binding affinity.

Sasa mfupa, huu wa mnyama wa kawaida tuu mathalan wa ng'ombe aidha ukiuchoma au ukiuchemsha kwa muda mrefu sana au kwa kutumia pressure cooker (kama umewahi andaa supu ya kongoro hadi mifupa ikalainika basi hata hiyo mifupa inafaa sana).

Kama ulichemsha hakikisha umeiva Kwa maana uroto wote umetoka, usuuze na Anika juani vizuri uhifadhi kama huduma ya kwanza.

Ukitaka kufahamu kama upo tayari kwa matumizi unakua na tabia flan hivi ya kunata nata iwe mikononi kama ukiushika mikono ikiwa imelowana au hata ukilamba hua unanasa kwenye ulimi.
 
😅 ila pamoja na yote wee dada ni gaidi... Kifutu unamkamata kama kuku..? Wakat mimi kiukweli nyoka nipo tayar kumuachia nyumba akiingia 😂
 
you make my day
 
Inahitaj ujasir sana juz nimeshika mmoja wa baridi sana ile ngozi yake unaeza jikuta umemuachia na kifo chako itakuwa kimefika
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…