Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Mwanamke asipokuwa mwangalifu wakati akimuomba mwanaume amsaidie jambo, anaweza kutengeneza mazingira ambayo yatakuwa ni njia au chanzo kizuri kwa ndoa kusambaratika. Kuna aina ya uombaji ambayo kwa maumbile ya mwanaume unaonekana kama dharau au udhalilishaji.
Wanaume wanapokuwa wameweka mawazo yao kwenye jambo fulani, wanapotumwa na wake au wapenzi wao, huwa wanakuwa na ugumu sana kufanya walichoombwa kukifanya. Katika hali kama hii mwanamke inabidi awe mwangalifu sana anapomwambia mpenzi au mume wake afanye jambo fulani.
Mwanaume huwa hataki kuambiwa afanye jambo ambalo tayari alikuwa amepanga kulifanya. Kama amepanga kusafisha nyuma ya nyumba, hataki kuja kuambiwa kama vile anakumbushwa. Kama mjuavyo, mwanaume huwa na hisia za ubabe na hapendi kuambiwa kuhusu mambo ambayo yako wazi au ameyapanga kuyatekeleza.
Sio tu kuombwa na mke au mpenzi kufanya jambo fulani, bali hata kwenye mambo mengine. Mwanaume akishamwambia mkewe kuwa anataka kufanya biashara fulani, huwa hataki kukumbushwa kumbushwa tena. Anapokumbushwa huwa anajiona kama vile amefanywa yu mtoto mdogo au hajui wajibu wake, kwa hiyo yu dhaifu. Mwanamke anapomuomba mwanaume kufanya jambo fulani, hatakiwi kulikumbushia au kama mumewe ameshapanga kufanya jambo fulani, siyo juu yake kumwambia tena na tena kuhusu jambo hilo. Kwani ni lazima watakorofishana.
Mwanamke ambaye huwa anapenda kudai au kusikitika kwa jambo ambalo hajafanyiwa na mumewe au mpenzi wake, hata kama anatoa madai yake au masikitiko yake kwa maneno matamu vipi, ni lazima atamuudhi mpenzi wake. Kwa mfano kama mume ameshindwa kumpa mke kitu fulani au kumfanyia jambo fulani ambalo pengine aliahidi kumtendea, mwanamke anapaswa kuwa mwangalifu katika kulieleza hili.
Kuna wanawake ambao huwa wana tabia ya kudaidai au kuonyesha kusikitishwa kila jambo fulani lisipofanywa na waume au wapenzi wao. Hali hii kwa kweli huwa inawakera sana wanaume