Somo hili litawasaidia kuwaelewa waume zenu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Somo hili litawasaidia kuwaelewa waume zenu!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Sep 10, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Sep 10, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mwanamke asipokuwa mwangalifu wakati akimuomba mwanaume amsaidie jambo, anaweza kutengeneza mazingira ambayo yatakuwa ni njia au chanzo kizuri kwa ndoa kusambaratika. Kuna aina ya uombaji ambayo kwa maumbile ya mwanaume unaonekana kama dharau au udhalilishaji.

  Wanaume wanapokuwa wameweka mawazo yao kwenye jambo fulani, wanapotumwa na wake au wapenzi wao, huwa wanakuwa na ugumu sana kufanya walichoombwa kukifanya. Katika hali kama hii mwanamke inabidi awe mwangalifu sana anapomwambia mpenzi au mume wake afanye jambo fulani.

  Mwanaume huwa hataki kuambiwa afanye jambo ambalo tayari alikuwa amepanga kulifanya. Kama amepanga kusafisha nyuma ya nyumba, hataki kuja kuambiwa kama vile anakumbushwa. Kama mjuavyo, mwanaume huwa na hisia za ‘ubabe’ na hapendi kuambiwa kuhusu mambo ambayo yako wazi au ameyapanga kuyatekeleza.

  Sio tu kuombwa na mke au mpenzi kufanya jambo fulani, bali hata kwenye mambo mengine. Mwanaume akishamwambia mkewe kuwa anataka kufanya biashara fulani, huwa hataki kukumbushwa kumbushwa tena. Anapokumbushwa huwa anajiona kama vile amefanywa yu mtoto mdogo au hajui wajibu wake, kwa hiyo yu dhaifu. Mwanamke anapomuomba mwanaume kufanya jambo fulani, hatakiwi kulikumbushia au kama mumewe ameshapanga kufanya jambo fulani, siyo juu yake kumwambia tena na tena kuhusu jambo hilo. Kwani ni lazima watakorofishana.

  Mwanamke ambaye huwa anapenda kudai au kusikitika kwa jambo ambalo hajafanyiwa na mumewe au mpenzi wake, hata kama anatoa madai yake au masikitiko yake kwa maneno matamu vipi, ni lazima atamuudhi mpenzi wake. Kwa mfano kama mume ameshindwa kumpa mke kitu fulani au kumfanyia jambo fulani ambalo pengine aliahidi kumtendea, mwanamke anapaswa kuwa mwangalifu katika kulieleza hili.

  Kuna wanawake ambao huwa wana tabia ya kudaidai au kuonyesha kusikitishwa kila jambo fulani lisipofanywa na waume au wapenzi wao. Hali hii kwa kweli huwa inawakera sana wanaume
   
 2. s

  shalis JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hayo ni kama mambo ya kizamani eti sijui tusiwakumbushe looh mie hata sina muda huo wa kubembeleza jitu zima kam ni wajibu wake na nilisha mwambia THEN HAFANYI ni lazima nimkumbeshe... shaaaaaaah mambo ya kubembelezana wapi yapo kwa sasa? namwambi ana kama hatakia si aache kama naweza nitafanyahaya unayoyasema ni kama ka mfumo dume fulan hivi mtu unajiwekea kwa hawa wakiumesikubaliani na wewe hata kidogo kama hivyo na yeye aanze kuchunga maneno yake na jinsi anavyo kumbushia vitukitu gani bwana kila skiu ooh mfanyie hivi mwanaume wao ni mangapi wanatufanyia zaidi ni kuumiza mioyo ya watu dailykwani unadhani that will keep your man at home??lol muda wa maisha hayo yalishapita hapa ni pasu kwa pasu asipofanya majukumu yake nakumbusha kama ku react na react kuonyesha msisitizo (kama kuwaka na kikiwake bwana)"loooooh kitu gani ndoa watu kilakukicha mateso wamama mateso kulia daily tubadilike tukiwezeshwa TWAWEZAallaaaaaaaah...
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,659
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Hapo sio suala la uzamani au upya,ni suala la maumbile dada!
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  nielewavyo ni kuwa mwanadamu bila ya kuzingatia jinsia yake hapendi shuruti...........................huona kama anaburuzwa......................could be interesting how ladies react to my commentary.................
   
 5. O

  Oak Member

  #5
  Sep 10, 2011
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu unatoa post/thread nyingi kwa wakati mmoja, punguza speed watu wachangie moja ndo ulete nyingine.


  Ni ushauri tu.

  Oak
   
 6. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #6
  Sep 11, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  NImekuelewa mkuu, ahsante kwa ushauri wako...............Pamoja Daima
   
Loading...