Somo gani litolewe watu waache kukosoa hovyo Serikali

huyu jamaa anaakili za ajabu hata nashindwa kumshangaa, kwahiyo hata kama dereva anaingia shimoni tutulie tu hadi tuingie ndo tumwambie kuna jiwe lilikuwepo pale angelikwepa!!

ama kweli ujinga ni ugonjwa mbaya sana.
haya ngoja wasubiri muda wake uishe wamkosoe...mimi sio mkosoaji hata hivyo.
Somo linapatikana kwa awamu ya nne..dereva yule alipigiwa kelele sana..lakini gari lilifika na kelele hazikusaidia.Na leo hii abiria wake wanampongeza kwa umalidadi wake wa kuongoza gari kuliko huyu wa sasa.

Sasa kwa nini kwa sasa tusiache kupiga kelelele na tukasubiri mwisho wa safari.??

Tulimpatia gari kwa kumwamini kuwa ana lesseni ..sasa kelele za nini??
 
Utafikaje wakati dereva mwenyewe hajui wapi tunaenda?
Wakati tunamkabidhi gari si tulijua ataliendesha kwenda wapi??

Mm nadhani tumuache aendeshe...mwisho wa Safari tuta-tathimini uendeshaji wake na wenye maamuzi itakuwa ni sisi.
 
Mkuu kama huwa unasubiri kwanza ufike unakokwenda ndio ujue kama dereva ni mzuri au mbaya basi utakuwa na matatizo pia. Na kama uko hivyo unaweza usifike mwisho wa safari ukafia njiani.... kukosoa ni kuonyesha kasoro ilipo ili wahusika warekebishe mapungufu na kuboresha panapohitajika. Sasa ukisubiri mpaka muda utakapoisha ukikosoa itasaidia nini? Mhubiri mmoja alisema ukiona mtu anataka kuingia kuogelea na viatu jukumu lako ni kumweleza kuwa huwezi kuogelea na viatu, usisubiri azame ndio uanze kusema hukupaswa kuingia na viatu, hapo utawekwa kwenye kundi la wanafiki. Kwa mtu yeyote makini gari ikianza safari tu utamjua dereva makini na asiye na umakini na ndio maana wakatoa namba za simu za maofisa usalama ili kama kuna tatizo toa taarifa usisubiri ufike kwanza, unaweza usifike..... Kukosoa kuna lengo la kukuimarisha na utambue unapokosea, huwa hatugombani na kioo kinapotuonyesha uchafu uliopo usoni. Lengo kuu ni kujengana Tanzania ni yetu sote..... Mwisho hilo neno "tukufu" Nyerere alilikataa kwenye utawala wake likaibuka enzi za mzee Mwinyi, Mkapa akalikataa tena. Kwa Kikwete halijasikika kabisa naona linaibukia ngwe hii tena.... Utukufu ni wa Mwenyezi Mungu pekee.
Uko sahihi mkuu kwa maoni yako.. Ila;

Usisahau kuwa siri ya gari anaijua dreva...na siku zote lengo la dreva ni kufikisha abiria wake salama..

Sasa, suala la kupitisha gari kwenye mashimo au kupitia njia usiyo ifahamu siyo sababu inapaswa kuchuliwa na kumpigia kelele...hii inaweza kumpunguzi dreva hali ya kujiamini na mwisho akapoteza mwelekeo wa safari...

Hivyo kelele zetu zitakuwa hazija tusaidia...

Zaidi ya kumsifia ili aongeze ufundi wake na safari iende..makosa yake tutayaeleza mwisho wa safari....
 
Binafsi nashindwa kuelewa, nilitarajia baada ya sheria ya makosa ya mtandaoni kuanza kutumika, watu wangeacha au kupunguza ukosoaji na matusi ktk mitandao ya kijamii kwa serikali yetu Tukufu ya awamu ya Tano.

Sasa kila kipita huku na kule kwenye mitandao ya kijamii...nakuta watu ni matusi tu..

Pamoja na kuwa kuna kesi nyingi tu na wengi bado wanafuatiliwa lakini bado watu hawajaacha tu..

Najiuliza tu!!, nn kifanyike watu waelewe kuwa serikali hii Tukufu inahitaji ifanye kazi na watu waone matokeo na si kupigiwa kelele ambazo zimepigwa miaka yote na hazijaleta manufaa yoyote?

Binafsi suala kukosoa naliunga mkono ila lingefaa zaidi liwe linafanyika baada ya muda wa uongozi kuisha...

Huwezi kujua huyu dreva ni mzuri au mbaya wakati bado hujafika unako kwenda...

Hivyo binafsi naona ni vyema hukumu au ukosoaji ukakafanyika baada ya safari..na siyo njiani.

Ndyo maana wengine wanamsifia dreva aliye pita kuwa alikuwa mzuri kuliko huyu....... wakati, alipokuwa anaendesha walikuwa wanamlalamikia sana.

Somo lililobaki na bora kabisa ni lile la pyu pyu pyu. Hili litaeleweka tu.
 
kukosoa hakutaisha kamwe,hasi tarajie kwenye nchi ya demokrasia watu wapo huru kuongea ili mradi hawatukani ..mbegu wayano ipandikiza kwa hii kamatakamata kufunga midomo ,ikikuwa itasumbua sana taifa
Mm binafsi nijiuliza sana...tangu sheria ya mitandao ianzishwe, no changes..watu awanaendelea kufanya yao tu, na wengine wako ndani na wengine wanakamatwa...

Somo gani litolewe watu waelewe...japo muda nao unaenda kuisha..
 
Binafsi nashindwa kuelewa, nilitarajia baada ya sheria ya makosa ya mtandaoni kuanza kutumika, watu wangeacha au kupunguza ukosoaji na matusi ktk mitandao ya kijamii kwa serikali yetu Tukufu ya awamu ya Tano.

Sasa kila kipita huku na kule kwenye mitandao ya kijamii...nakuta watu ni matusi tu..

Pamoja na kuwa kuna kesi nyingi tu na wengi bado wanafuatiliwa lakini bado watu hawajaacha tu..

Najiuliza tu!!, nn kifanyike watu waelewe kuwa serikali hii Tukufu inahitaji ifanye kazi na watu waone matokeo na si kupigiwa kelele ambazo zimepigwa miaka yote na hazijaleta manufaa yoyote?

Binafsi suala kukosoa naliunga mkono ila lingefaa zaidi liwe linafanyika baada ya muda wa uongozi kuisha...

Huwezi kujua huyu dreva ni mzuri au mbaya wakati bado hujafika unako kwenda...

Hivyo binafsi naona ni vyema hukumu au ukosoaji ukakafanyika baada ya safari..na siyo njiani.

Ndyo maana wengine wanamsifia dreva aliye pita kuwa alikuwa mzuri kuliko huyu....... wakati, alipokuwa anaendesha walikuwa wanamlalamikia sana.
Mtu akiwa anakupiga risasi akuue, halafu kuna mtu mwingine ana uwezo wa kuzuia huyo anayekupiga risasi asikupige risasi,halafu mtu wa tatu akasema "usizuie huyu michosho apigwe risasi, subiri kwanza apigwe risasi halafu ndiyouje usemekwamba kumpiga risasi ni kitu kibaya.

Hapoutaonaje,utaona kuachiwa wewe upigwe risasi ni sawa?
 
Somo linapatikana kwa awamu ya nne..dereva yule alipigiwa kelele sana..lakini gari lilifika na kelele hazikusaidia.Na leo hii abiria wake wanampongeza kwa umalidadi wake wa kuongoza gari kuliko huyu wa sasa.

Sasa kwa nini kwa sasa tusiache kupiga kelelele na tukasubiri mwisho wa safari.??

Tulimpatia gari kwa kumwamini kuwa ana lesseni ..sasa kelele za nini??
...nani aliempa gari? mbona nasikia alisemaga aliomba awashe tu mkamuachia akalie na siti mbele ya usukani...na mkamuacha aliondoe pasi kujiandaa.

ila bwana mdogo kama unataka kukaa kimya kaa kimya tu hakuna wa kukupangia, usiwapangie na hao wanaopiga kelele ni haki yao si wamechangia ela ya mafuta na hata gari likiharibika wao pia itawaladhimu kugharamia matengenezo, wanauchungu na gari lao hao.

waaaaaache.
 
Binafsi nashindwa kuelewa, nilitarajia baada ya sheria ya makosa ya mtandaoni kuanza kutumika, watu wangeacha au kupunguza ukosoaji na matusi ktk mitandao ya kijamii kwa serikali yetu Tukufu ya awamu ya Tano.

Sasa kila kipita huku na kule kwenye mitandao ya kijamii...nakuta watu ni matusi tu..

Pamoja na kuwa kuna kesi nyingi tu na wengi bado wanafuatiliwa lakini bado watu hawajaacha tu..

Najiuliza tu!!, nn kifanyike watu waelewe kuwa serikali hii Tukufu inahitaji ifanye kazi na watu waone matokeo na si kupigiwa kelele ambazo zimepigwa miaka yote na hazijaleta manufaa yoyote?

Binafsi suala kukosoa naliunga mkono ila lingefaa zaidi liwe linafanyika baada ya muda wa uongozi kuisha...

Huwezi kujua huyu dreva ni mzuri au mbaya wakati bado hujafika unako kwenda...

Hivyo binafsi naona ni vyema hukumu au ukosoaji ukakafanyika baada ya safari..na siyo njiani.

Ndyo maana wengine wanamsifia dreva aliye pita kuwa alikuwa mzuri kuliko huyu....... wakati, alipokuwa anaendesha walikuwa wanamlalamikia sana.

Hii sio serikali tukufu....

Unajua maana ya ukosoaji?

Halafu ukute huyu mtu ni mwenye elimu ya chuo kikuu.
 
Ukosoaji uwe na kipimo kisizidi na kutweza utu wa mtu na kutotukanisha na kudharaulisha na kuonekana ni kinyaa au takataka huo sio ukosoaji bali uchochezi yani kosa umeliona badala ya kutoa wazo mbadala unatukana utu wa kiongozi na kumdharaulisha mbele ya wananchi wa Tanzania hili ndilo jambo ambalo halitakiwi lakini kwa serikali ambay n sisi wenyewe inahitaji njia mbadala na mawazo ya kuzidi kuipeleka nchi mbele sio matukano na dharau kwa viongozi hivo kujiona sio lolote na mwisho kutengeneza mzuio wa mawasiliano bora kati ya kiongozi na mwananchi
 
Back
Top Bottom