Soma upate mawili matatu: Mhitimu mambo ninayopitia kipindi hiki katika harakati zangu

Habari yenu wanaJF

Poleni na Majukumu ya kila siku, Leo nimekuja kusimulia mawili matatu nayopitia katika harakati zangu nishare nanyi ndugu zangu.

Wanajf mimi Ni muhitimu wa BSc Education(Mathematics and geography) , kama post zangu nyingi zilivyojieleza huko nyuma. Nilihitimu mwaka 2019 November, nilijaribu walau Kuomba tempo katika sekondari mbalimbali hapa mjini Songea lakini sikufanikiwa kupata kwa wakati ule, (labda kwavile Sikua hata na vyeti vya Masomo yangu).

Nilifanikiwa kufungua tuition centre ya Muda wa Likizo December, Nilifanikiwa kupata wanafunzi wa kutosha kwa Kipindi kile ikizingatia nilifanya promotion ya kutosha, mwaka 2020 niliendelea kufundisha tuition centre mbalimbali Nikipata kipato walau cha kununulia mswaki na matumizi mbalimbali, niliweza kufundisha hata Watoto wa Wakubwa wa Mkoa majumbani Mwao.

Muda wa Likizo ya corona nilijichanganya katika kazi ngumu ya kuopoa na kuchimba mchanga kwasababu hata tuition hazikuruhusiwa tena, ilibidi nijivue kutoka mwalimu hadi mchimba mchanga, ni muda ambao nimejifunza mengi sana na nimekutana na wengi sana.

Ipo siku ambayo Nilipata mteja wa mchanga ambaye alikuja kuchukua mchanga kwa tractor ukizingatia tractor haliwezi kubinua ilibidi nichukue Buku ya kushushia mwenyewe, nilipokua nikishusha nyumbani kwa boss nilishangazwa kuona naitwa "teacher" na msichana Mdogo aliyetokea ndani kwa boss Ni mtoto wa boss, nilishusha mzura hadi machoni nikijua atahisi kanifananisha lakini aliita tena kwa msisitizo,.

Hakuamini kuniona pale, Mzee wake alishangaa kuitwa vile, Nilimwambia hujambo Dogo, nikachukua changu nikatembea.

Ipo siku nilipeleka mchanga site nilishangaa kukutana na headmaster wa Shule fulani niliyofanyia field akiwa ndio muhusika inabidi anipatie Pesa, nilifanya maujanja hatimaye hakuweza Nitambua.

Nilikua napakia mchanga wa mwenzangu sikumoja ( nipate 2000 ta haraka) nilishangaa boss akiletwa na bodaboda ambaye nilikua nikimkimbizia Mathematics O-level, alishangaa aliniita mkuu vipi tena? Nilipandisha mzura nikamtazama Nikamwambia Tutaongea boss.

Leo hii nimepeleka mchanga sehemu nimeshangaa kukuta fundi Mkuu ni Dogo aliecha Shule miaka ile akiwa pale sekondari, aliniuliza Bro Upo Huku sikuhizi, Nilimwambia ndio Nipe Dili hizo Niishi.

Kuna MUDA inanibidi niulize kati ya form four tuliohitimu Pamoja hivi nani ni dereva ili walau AKIPATA trip za mchanga anikumbuke na Mimi.

Unajua HAYA maisha hayana huruma, unakuta sometimes unachimba mchanga na Mzee wangu labda mnauza mnapata 50 ,000 Ila unamwambia Basi Mzee Wewe Chukua 20000 mimi Nibaki na 30000 kwa sababu mimi bado najipanga kimaisha, lakini Mzee anakaza anataka 50% anakwambia yeye ndio kaleta gari, no way utafanyaje Sasa.

Maisha yana mengi sana ya kujifunza, unajua ukishamaliza Chuo kama hivi home nako wanajua unaenda kuajiriwa soon, Kuna Muda unamwambia Mzee nipatie hizi Mbao nikachonge kitanda anakwambia Je ukipangiwa kazi Mwanza utaenda nacho? Sasa najiulizaga na nisipopangiwa Mzee itakuaje?

Wazazi wengi wetu wanaamini WANAO tutaajiriwa, yaa Ni kweli, lakini mtuwezeshe PIA kwa Kipindi hiki ambacho hatuna KITU,.

Hakuna mtu asiyependa goodlife, "we need money to go, to do our family matters".

Wanajf kama umefanikiwa usimcheke asiefanikiwa, kama unauwezo basi muwezeshe, kwa kazi nazopiga mtu mwingine mwenye degree kama mimi anaweza kataa kabisa akiona ni kujidharirisha, lakini Naamini mafanikio hayana SIRI.

Naamini katika kusubiri million basi unapaswa utafute Buku.

Unaweza teseka DUNIANI na mbinguni PIA.
Ni Mimi Ndondocha mkuu.

Karibuni kwa mchanga mgumu Songea

0754350882
View attachment 1492611v
One day EVERYTHING WILL BE OKEY.

Naondoka na hili ""Naamini katika kusubiri million basi unapaswa utafute Buku.""

#YNWA
 
Yote haya ni uzezeta WA Sisi wenyewe wananchi ,suala ni kwamba tuna uchumi mfu nchi hii , uchumi usiozalisha ajira na economic opportunities Kwa wananchi ni uchumi mfu .
Serikali ya CCM imedumaza hii nchi na uchumi Kwa zaidi ya miaka 60 lakini bado tunaona ni kawaida Tu hatuchukui hatua ya kuwatoa hawa takataka toka kwenye madaraka ,angalia maisha yalivyo magumu sasa hivi + inflation ya bidhaa na huduma , this is death
 
Hili ni janga ,too bad wapumbav wengi wanaona kawaida Ila si kawaida na hatutakiwi kuona hili suala ni kawaida ,ni mtu mwenye mtindio WA ubongo na uvivu WA kufikiri ndio anaeweza ona kawaida na kushabikia mtu msomi mwenye fani yake kufanya kazi za kipumbav kama hizo anazofanya mtoa mada . Hili ni tatizo .
Ni misuse and poor utilization ya resources , wengi hamuelewi kwamba human resource tena skilled kama huyo mtoa mada yaani mtu mwenye fani ni resource ambayo taifa linatakiwa liitumie ipasavyo Ka inavyofaa ,sio mtu anasoma mpaka chip kikuu halafu anakuwa mchimba mchanga huo ni utaahira na uzezeta.
Hii nchi kama watu hawatakaa na kujiuliza mambo muhimu kama haya kila siku mbajadili upumbav WA Yanga Simba na uzwazwa mwingine hili Taifa halitakaa litoboe hata siku moja .

Ni Kwa nini watu wafanye kazi za kipumbav na resources zote nchii ilizo nazo ? Kwa nini watu wanaishi maisha ya kimasikini na kilofa nchi hii ? Hao wapuuz wanaowaambia mjiajiri Kwa kuchimba mchanga na kufanya hizo kazi za kis£nge wao mbona watoto wao au ndugu zao hawajawaruhusu au kuwaambia wafanye hivyo ?

Sasa hiyo mikopo na Ada zilizotumika mnatoa za nini kama si upotevu WA pesa ,yaani mtu kasimeshwa Kwa mamilioni Kwa fedha za walipa Kodi halafu was£ng£ nyie mnafurahia huyo mtu kwenda kufanya kazi za kilofa kama kuuza karanga na kuchimba mchanga , sh£nzi.
 
Nikifikiriaga maisha ya chuo, najiona nilicheza Kama pele. Sijawahi kuonja hata sek 1 ya u-jobless. Nimefika tu home (mkoani kwa broo alipokuwepo, siku hiyo hiyo nikakabidhiwa mradi tuliouanzisha kwa pamoja kipindi nipo miezi ya mwisho mwisho ya chuo, nikaanza kazi siku hiyo hiyo, Hadi Leo mm ndo CEO, MANAGER, MSIMAMIZI, n.k wa mradi huo.

Sitafuti hela ya kula, bali hela ya kupiga hatua kimaisha.

Kula, kulala, kuvaa na bill Kama Kodi, umeme n.k Ni uhakika nabaki nasotea hela ya kupiga hatua kimaisha.

Asante Mungu Mkuu
Kama anavyotueleza Robert T. Kiyosaki kwenye kitabu chake cha Rich dad's Cash flow Quadrant inaonekana wewe kwa sasa uko kwenye Self employed quadrant... Hata hivyo ili uweze kuwa financially free unatakiwa kuingia kwenye quadrants za upande wa kulia (Bussiness owner na baadae investor)... Hongera zako all the same...
 
Hili ni janga ,too bad wapumbav wengi wanaona kawaida Ila si kawaida na hatutakiwi kuona hili suala ni kawaida ,ni mtu mwenye mtindio WA ubongo na uvivu WA kufikiri ndio anaeweza ona kawaida na kushabikia mtu msomi mwenye fani yake kufanya kazi za kipumbav kama hizo anazofanya mtoa mada . Hili ni tatizo .
Ni misuse and poor utilization ya resources , wengi hamuelewi kwamba human resource tena skilled kama huyo mtoa mada yaani mtu mwenye fani ni resource ambayo taifa linatakiwa liitumie ipasavyo Ka inavyofaa ,sio mtu anasoma mpaka chip kikuu halafu anakuwa mchimba mchanga huo ni utaahira na uzezeta.
Hii nchi kama watu hawatakaa na kujiuliza mambo muhimu kama haya kila siku mbajadili upumbav WA Yanga Simba na uzwazwa mwingine hili Taifa halitakaa litoboe hata siku moja .

Ni Kwa nini watu wafanye kazi za kipumbav na resources zote nchii ilizo nazo ? Kwa nini watu wanaishi maisha ya kimasikini na kilofa nchi hii ? Hao wapuuz wanaowaambia mjiajiri Kwa kuchimba mchanga na kufanya hizo kazi za kis£nge wao mbona watoto wao au ndugu zao hawajawaruhusu au kuwaambia wafanye hivyo ?

Sasa hiyo mikopo na Ada zilizotumika mnatoa za nini kama si upotevu WA pesa ,yaani mtu kasimeshwa Kwa mamilioni Kwa fedha za walipa Kodi halafu was£ng£ nyie mnafurahia huyo mtu kwenda kufanya kazi za kilofa kama kuuza karanga na kuchimba mchanga , sh£nzi.
Pole mkuu
 
Jamaa anatupiga fix kweli..mara anasema amemaliza SUA kozi ya Agriculture mara amemaliza B.A. Education in Geography and Mathematics yaani haeleweki🤣🤣🤣
We jamaa wapi nilisema nimesomea agrculture? Mimi nilisomea ualimu, and i do now.
 
Hili ni janga ,too bad wapumbav wengi wanaona kawaida Ila si kawaida na hatutakiwi kuona hili suala ni kawaida ,ni mtu mwenye mtindio WA ubongo na uvivu WA kufikiri ndio anaeweza ona kawaida na kushabikia mtu msomi mwenye fani yake kufanya kazi za kipumbav kama hizo anazofanya mtoa mada . Hili ni tatizo .
Ni misuse and poor utilization ya resources , wengi hamuelewi kwamba human resource tena skilled kama huyo mtoa mada yaani mtu mwenye fani ni resource ambayo taifa linatakiwa liitumie ipasavyo Ka inavyofaa ,sio mtu anasoma mpaka chip kikuu halafu anakuwa mchimba mchanga huo ni utaahira na uzezeta.
Hii nchi kama watu hawatakaa na kujiuliza mambo muhimu kama haya kila siku mbajadili upumbav WA Yanga Simba na uzwazwa mwingine hili Taifa halitakaa litoboe hata siku moja .

Ni Kwa nini watu wafanye kazi za kipumbav na resources zote nchii ilizo nazo ? Kwa nini watu wanaishi maisha ya kimasikini na kilofa nchi hii ? Hao wapuuz wanaowaambia mjiajiri Kwa kuchimba mchanga na kufanya hizo kazi za kis£nge wao mbona watoto wao au ndugu zao hawajawaruhusu au kuwaambia wafanye hivyo ?

Sasa hiyo mikopo na Ada zilizotumika mnatoa za nini kama si upotevu WA pesa ,yaani mtu kasimeshwa Kwa mamilioni Kwa fedha za walipa Kodi halafu was£ng£ nyie mnafurahia huyo mtu kwenda kufanya kazi za kilofa kama kuuza karanga na kuchimba mchanga , sh£nzi.
Umeeleweka kamanda
 
Back
Top Bottom