Soma upate mawili matatu: Kwa umri huu, haya nambo yafuatayo Nimeyashuhudia na kuyapitia

Ndondocha mkuu

JF-Expert Member
Feb 17, 2014
2,354
2,763
Wakuu habari za majukumu mbalimbali ya ujenzi wa Taifa.
Ni miezi kadhaa sijaleta thread hapa, tangu nilete ile thread ya jinsi nilivyopoteza 1.8M ndani ya siku chache.

Leo nimekuja tushare mambo mbalimbali ambayo nimeyapitia na nimeyaona hadi umr huu, yanaweza kukufundisha au kukupa exposure zaidi katika hii dunia..

a) kuna kipindi nilikuwa na matatzo fulani ya kifamilia ambayo yalihitaji maombi ikiwemo kuombewa na watumishi wa mungu, niliweza kumtafuta mchungaji mmoja maarufu kidogo katika mkoa niliopo, nilimsimulia yote, nilimuamini sana, lakini aliishia kuniomba ela akisema nimpatie kama sadaka ndani ya bahasha, aliishia kuramba elfu 50 yangu, tangu wakati huo sina imani na watu wanaojiita wachungaji.

b) kuna wakati niliibiwa simu yangu ambayo nilinunua katika kipindi kifupi kwa shilingi laki nne, niliumia sana, nilimtafuta mtaalamu haweze kunisaidia kuipata, mara ya kwanza naendq kwa mganga, aliniaminisha nitaipata simu yangu, huku akinipa mifano ya majiran ambao walipita kwake na kupata vitu vyao, alifanikiwa kuramba elfu 40000 yangu na simu sikupata, tangu wakati huo siwaamini tena hawa waganga hasahasa katika swala la kupata simu iliyopotea.

c) wakuu kuna kipindi nilikuwa navolunteer katika taasisi flani ya elimu bila ya malipo yoyote, lakini swala lililonishangaza ni kuona watumishi ambao wameajiriwa na serikali na wanamshahara mzuri sana wanakuja kunikopa, sio kunikopa bila riba yoyote na kukaa na ela kwa muda mrefu na kuja kuongeza deni juu ya deni, haohao wanakopa milioni 8 ,o au 15 benki lakini hawakukumbuki hata kwa elfu 5 au 10, lakini wakubanwa wanakuazima bila ya huruma, wanachukulia mtu kwa age ya 25'S huna majukumu wakati ni muda sahihi wa mtu kujipanga kimaisha.

d) Wakuu katika umri huu , niliweza kupoteza ela 1.8M kwa muda mfupi sana , ela ambayo niliitafuta kwa miezi zaidi ya 6, niliumia sana, nilikata hadi tamaa,ila kwa muda wa miezi ileile sita nilitengeneza zaidi ya ile hela. Hapa nilijifunza pesa inahitaji nidhamu sana.

e) Wakuu katika swala la kuazima watu ela nimegundua watu wengi sio waaminifu kabisa, unaweza mpa mtu 70000 akakuahd mwsho wa mwez nitakupa lakini ikifika anakupa40000 na ahadi kibao alafu kati ya mwezi anakuazima tena 80000. Au mtu anakuazma elfu 10 harudishi, anajisahau anapata shida kubwa anakuazma laki 1, binafs kwasasa siwez kukupatia. Katika hili nimejifunza unapoahd kumlipa mtu ela yake jitahd umpe ontime, sjida haziishi.

Asante Jf HOME OF GT
 
Ngoja mimi nisaidie kufupisha kwa wazembe wa kusoma:

1. Usiwaamini mitume na manabii. Wengi wanataka sadaka tu na hawatatui matatizo.

2. Usiwaamini waganga wa kienyeji. Wengi ni waongo.

3. Hela inahitaji nidhamu.

4. Kukopa harusi kulipa matanga. Usikopeshe watu hovyo hovyo.

Mengine mtaongezea 😁
 
WAKUU,
TUSIPENDE KUTOA PESA KWA MTU/WATU IKIWA HAKUNA FAIDA/MANUFAA YOYOTE KWA UPANDE WETU.

IFIKIE HATUA KILA MTU AJIPATIE MAHITAJI YAKE PASIPO KUWANYONYA/KUWADHULUMU WENGINE KIUCHUMI NA KIJAMII.
 
Azimisha pesa kiasi kidogo sana tena sana (1/20 ya pato lako na 1/10 ya tatizo lake) ambacho hata ukicheleweshewa au kutolipwa kabisa haita athiri chochote kwako hii itasaidia kutovunja ukaribu baina yenu na ifanye kama umesaidia tu tatizo lake lakini kwa kutomuambia kama umetoa msaada,hutojuta tena.
 
Wakuu habari za majukumu mbalimbali ya ujenzi wa Taifa.
Ni miezi kadhaa sijaleta thread hapa, tangu nilete ile thread ya jinsi nilivyopoteza 1.8M ndani ya siku chache.

Leo nimekuja tushare mambo mbalimbali ambayo nimeyapitia na nimeyaona hadi umr huu, yanaweza kukufundisha au kukupa exposure zaidi katika hii dunia..

a) kuna kipindi nilikuwa na matatzo fulani ya kifamilia ambayo yalihitaji maombi ikiwemo kuombewa na watumishi wa mungu, niliweza kumtafuta mchungaji mmoja maarufu kidogo katika mkoa niliopo, nilimsimulia yote, nilimuamini sana, lakini aliishia kuniomba ela akisema nimpatie kama sadaka ndani ya bahasha, aliishia kuramba elfu 50 yangu, tangu wakati huo sina imani na watu wanaojiita wachungaji.

b) kuna wakati niliibiwa simu yangu ambayo nilinunua katika kipindi kifupi kwa shilingi laki nne, niliumia sana, nilimtafuta mtaalamu haweze kunisaidia kuipata, mara ya kwanza naendq kwa mganga, aliniaminisha nitaipata simu yangu, huku akinipa mifano ya majiran ambao walipita kwake na kupata vitu vyao, alifanikiwa kuramba elfu 40000 yangu na simu sikupata, tangu wakati huo siwaamini tena hawa waganga hasahasa katika swala la kupata simu iliyopotea.

c) wakuu kuna kipindi nilikuwa navolunteer katika taasisi flani ya elimu bila ya malipo yoyote, lakini swala lililonishangaza ni kuona watumishi ambao wameajiriwa na serikali na wanamshahara mzuri sana wanakuja kunikopa, sio kunikopa bila riba yoyote na kukaa na ela kwa muda mrefu na kuja kuongeza deni juu ya deni, haohao wanakopa milioni 8 ,o au 15 benki lakini hawakukumbuki hata kwa elfu 5 au 10, lakini wakubanwa wanakuazima bila ya huruma, wanachukulia mtu kwa age ya 25'S huna majukumu wakati ni muda sahihi wa mtu kujipanga kimaisha.

d) Wakuu katika umri huu , niliweza kupoteza ela 1.8M kwa muda mfupi sana , ela ambayo niliitafuta kwa miezi zaidi ya 6, niliumia sana, nilikata hadi tamaa,ila kwa muda wa miezi ileile sita nilitengeneza zaidi ya ile hela. Hapa nilijifunza pesa inahitaji nidhamu sana.

e) Wakuu katika swala la kuazima watu ela nimegundua watu wengi sio waaminifu kabisa, unaweza mpa mtu 70000 akakuahd mwsho wa mwez nitakupa lakini ikifika anakupa40000 na ahadi kibao alafu kati ya mwezi anakuazima tena 80000. Au mtu anakuazma elfu 10 harudishi, anajisahau anapata shida kubwa anakuazma laki 1, binafs kwasasa siwez kukupatia. Katika hili nimejifunza unapoahd kumlipa mtu ela yake jitahd umpe ontime, sjida haziishi.

Asante Jf HOME OF GT
Hapo kwenye namba uno yaani moja umeweka neno muhimu sana.

Kikubwa achana na kuamini wachungani. Muamini Mungu pekee. Na mtumiahi yeyotewa Mungu anayekuomba pesa ili akuombee huyo ndiye aliyenenwa na Yesu kwenye Mathayo kwamba shetty anaweza kuja kama malaika wa nuru na watumishi wake wakaja kama watumishi wa haki.

Formula ya Mungu ni kwamba AMEKUPA KIPAWA BURE NA UTOE BURE
 
Amina
 
Ngoja mimi nisaidie kufupisha kwa wazembe wa kusoma:

1. Usiwaamini mitume na manabii. Wengi wanataka sadaka tu na hawatatui matatizo.

2. Usiwaamini waganga wa kienyeji. Wengi ni waongo.

3. Hela inahitaji nidhamu.

4. Kukopa harusi kulipa matanga. Usikopeshe watu hovyo hovyo.

Mengine mtaongezea
Mimi nitazungumzia suala la imani; watu watambue kuwa, mtu yeyote anaweza kuongea na Mungu moja kwa moja muda wowote. Kwa habari ya maombi, hii ni imani kutoka ndani ya moyo wako, kikubwa ni imani juu ya hicho unachoomba. Lakini pia tunapaswa kutambua, muda muafaka wa kujibiwa maombi yako anaujua Mungu, kwa maana kuwa hachelewi wala hawahi; muda wowote atakaokujibu ni sahihi. Tusiwe wabinafsi; tusiangalie upande wetu tu, bali mapenzi yake yatimizwe.
 
Umeeleweka mkuu
 
Back
Top Bottom