Soma upate mawili matatu: Mhitimu mambo ninayopitia kipindi hiki katika harakati zangu

Ndondocha mkuu

JF-Expert Member
Feb 17, 2014
1,464
2,000
Habari yenu wanaJF

Poleni na Majukumu ya kila siku, Leo nimekuja kusimulia mawili matatu nayopitia katika harakati zangu nishare nanyi ndugu zangu.

Wanajf mimi Ni muhitimu wa BSc Education(Mathematics and geography) , kama post zangu nyingi zilivyojieleza huko nyuma. Nilihitimu mwaka 2019 November, nilijaribu walau Kuomba tempo katika sekondari mbalimbali hapa mjini Songea lakini sikufanikiwa kupata kwa wakati ule, (labda kwavile Sikua hata na vyeti vya Masomo yangu).

Nilifanikiwa kufungua tuition centre ya Muda wa Likizo December, Nilifanikiwa kupata wanafunzi wa kutosha kwa Kipindi kile ikizingatia nilifanya promotion ya kutosha, mwaka 2020 niliendelea kufundisha tuition centre mbalimbali Nikipata kipato walau cha kununulia mswaki na matumizi mbalimbali, niliweza kufundisha hata Watoto wa Wakubwa wa Mkoa majumbani Mwao.

Muda wa Likizo ya corona nilijichanganya katika kazi ngumu ya kuopoa na kuchimba mchanga kwasababu hata tuition hazikuruhusiwa tena, ilibidi nijivue kutoka mwalimu hadi mchimba mchanga, ni muda ambao nimejifunza mengi sana na nimekutana na wengi sana.

Ipo siku ambayo Nilipata mteja wa mchanga ambaye alikuja kuchukua mchanga kwa tractor ukizingatia tractor haliwezi kubinua ilibidi nichukue Buku ya kushushia mwenyewe, nilipokua nikishusha nyumbani kwa boss nilishangazwa kuona naitwa "teacher" na msichana Mdogo aliyetokea ndani kwa boss Ni mtoto wa boss, nilishusha mzura hadi machoni nikijua atahisi kanifananisha lakini aliita tena kwa msisitizo,.

Hakuamini kuniona pale, Mzee wake alishangaa kuitwa vile, Nilimwambia hujambo Dogo, nikachukua changu nikatembea.

Ipo siku nilipeleka mchanga site nilishangaa kukutana na headmaster wa Shule fulani niliyofanyia field akiwa ndio muhusika inabidi anipatie Pesa, nilifanya maujanja hatimaye hakuweza Nitambua.

Nilikua napakia mchanga wa mwenzangu sikumoja ( nipate 2000 ta haraka) nilishangaa boss akiletwa na bodaboda ambaye nilikua nikimkimbizia Mathematics O-level, alishangaa aliniita mkuu vipi tena? Nilipandisha mzura nikamtazama Nikamwambia Tutaongea boss.

Leo hii nimepeleka mchanga sehemu nimeshangaa kukuta fundi Mkuu ni Dogo aliecha Shule miaka ile akiwa pale sekondari, aliniuliza Bro Upo Huku sikuhizi, Nilimwambia ndio Nipe Dili hizo Niishi.

Kuna MUDA inanibidi niulize kati ya form four tuliohitimu Pamoja hivi nani ni dereva ili walau AKIPATA trip za mchanga anikumbuke na Mimi.

Unajua HAYA maisha hayana huruma, unakuta sometimes unachimba mchanga na Mzee wangu labda mnauza mnapata 50 ,000 Ila unamwambia Basi Mzee Wewe Chukua 20000 mimi Nibaki na 30000 kwa sababu mimi bado najipanga kimaisha, lakini Mzee anakaza anataka 50% anakwambia yeye ndio kaleta gari, no way utafanyaje Sasa.

Maisha yana mengi sana ya kujifunza, unajua ukishamaliza Chuo kama hivi home nako wanajua unaenda kuajiriwa soon, Kuna Muda unamwambia Mzee nipatie hizi Mbao nikachonge kitanda anakwambia Je ukipangiwa kazi Mwanza utaenda nacho? Sasa najiulizaga na nisipopangiwa Mzee itakuaje?

Wazazi wengi wetu wanaamini WANAO tutaajiriwa, yaa Ni kweli, lakini mtuwezeshe PIA kwa Kipindi hiki ambacho hatuna KITU,.

Hakuna mtu asiyependa goodlife, "we need money to go, to do our family matters".

Wanajf kama umefanikiwa usimcheke asiefanikiwa, kama unauwezo basi muwezeshe, kwa kazi nazopiga mtu mwingine mwenye degree kama mimi anaweza kataa kabisa akiona ni kujidharirisha, lakini Naamini mafanikio hayana SIRI.

Naamini katika kusubiri million basi unapaswa utafute Buku.

Unaweza teseka DUNIANI na mbinguni PIA.
Ni Mimi Ndondocha mkuu.

Karibuni kwa mchanga mgumu Songea

0754350882
IMG_20200620_091959.jpg
v
 

Attachments

Kizibo

JF-Expert Member
Jul 3, 2018
1,482
2,000
Nikifikiriaga maisha ya chuo, najiona nilicheza Kama pele. Sijawahi kuonja hata sek 1 ya u-jobless. Nimefika tu home (mkoani kwa broo alipokuwepo, siku hiyo hiyo nikakabidhiwa mradi tuliouanzisha kwa pamoja kipindi nipo miezi ya mwisho mwisho ya chuo, nikaanza kazi siku hiyo hiyo, Hadi Leo mm ndo CEO, MANAGER, MSIMAMIZI, n.k wa mradi huo.

Sitafuti hela ya kula, bali hela ya kupiga hatua kimaisha.

Kula, kulala, kuvaa na bill Kama Kodi, umeme n.k Ni uhakika nabaki nasotea hela ya kupiga hatua kimaisha.

Asante Mungu Mkuu
 

Kizibo

JF-Expert Member
Jul 3, 2018
1,482
2,000
I'm a graduate from a certain university in Dar in 2018, Toka nasoma, Baada ya kusoma vitabu (inspirational books) nikavimba kichwa nimajiona thamani yangu sio ya kujiriwa, natakiwa mitengeneze kazi yangu mwenyewe, mimi ndio niwe boss.

Sijawahi kutembea na bahasha wala kuapply, na hata cheti sijakifata na sijui nitakifata lini
 

Bf Tulinagwe

JF-Expert Member
Dec 11, 2019
214
500
Nikifikiriaga maisha ya chuo, najiona nilicheza Kama pele. Sijawahi kuonja hata sek 1 ya u-jobless. Nimefika tu home (mkoani kwa broo alipokuwepo, siku hiyo hiyo nikakabidhiwa mradi tuliouanzisha kwa pa1 kipindi nipo miez ya mwisho mwisho ya chuo, nikaanza kazi siku hiyo hiyo, Hadi Leo mm ndo CEO, MANAGER, MSIMAMIZI, n.k wa mradi huo.

Sitafuti hela ya kula, bali hela ya kupiga hatua kimaisha.

Kula, kulala, kuvaa na bill Kama Kodi, umeme n.k Ni uhakika nabak nasotea hela ya kupiga hatua kimaisha.

Asante Mungu Mkuu
Una genetics za Kiduku lilo... hakuna asiyependa kujiajiri na kujisimamia, somtmes circumstances zinakuwia vigumu. na kama hujapata kashikashi za kujikwamua kimaisha, umetengenezewa ulaji na kaka au mjomba, You are lucky Mr. Sio busara pia kujibust kwa mafanikio yako mbele ya muhangaikaji, unazidi kumkatisha tamaa.
 

October man

JF-Expert Member
Nov 23, 2017
3,694
2,000
PHASE......01

Nina swali moja

Hizi ishu zote unazofanya kusomesha tuition, kubeba mchanga kuna lengo umeliweka mf:- tuition kuja kufungua shule yako/kutafuta Mtaji wa kufanya kitu au unafanya kwasababu ndio ujapata hiyo ajira.

PHASE..........02

AJIRA jina kubwa linalotisha likitamkwa ila si kwakila mtu, muhasibu, HR, Doctor, Engineer and something like wana haki yakupaza Title ya ajira kuwa yenye kutisha ikitajwa kwasababu ILA si kwa mwalimu....mwalimu mwalimu.

PHASE................03

Degree zinawaaibu sana Graduates, walioishia lasaba wanaona wakishindwa maisha sawa ila wakimuona Graduate kashindwa maisha hawamuelewi wanampiga pressure za kila namna I.e kasoma lakini anamaisha kama sisi.
 

Ndondocha mkuu

JF-Expert Member
Feb 17, 2014
1,464
2,000
PHASE......01

Nina swali moja

Hizi ishu zote unazofanya kusomesha tuition, kubeba mchanga kuna lengo umeliweka mf:- tuition kuja kufungua shule yako/kutafuta Mtaji wa kufanya kitu au unafanya kwasababu ndio ujapata hiyo ajira.


PHASE..........02

AJIRA jina kubwa linalotisha likitamkwa ila si kwakila mtu, muhasibu, HR, Doctor, Engineer and something like wana haki yakupaza Title ya ajira kuwa yenye kutisha ikitajwa kwasababu ILA si kwa mwalimu....mwalimu mwalimu.


PHASE................03

Degree zinawaaibu sana Graduates, walioishia lasaba wanaona wakishindwa maisha sawa ila wakimuona Graduate kashindwa maisha hawamuelewi wanampiga pressure za kila namna I.e kasoma lakini anamaisha kama sisi.
Phase 1. Nimefanya hayo Mkuu nimejiwekea Akiba ya kutosha lakini haitoshi kwa malengo niliojiwekeA
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom